top of page

Saratani ya ukuta wa mfuko wa  mimba

GESTATIONAL TROPHOBLASTIC NEOPLASIA

 

Imeandikwa na madaktari wa ULY-Clinic

​

Utangulizi

​

Ni mkusanyiko wa magonjwa ya ujauzito yanayoweza kuwa saratania au yasiyo saratani. Magonjwa haya hutokea kwenye ukuta unaofunika kiumbe cha kwanza kinachofanyika mara baada ya uchavushwaji na hujulikana kama trophoblast. Ukuta huu huwa na kazi ya kukilisha kiumbe hiki kwa mara ya kwanza kinapofanyika na baadae ukuta huu huvamia kuta za ndani ya mfuko wa kizazi(endometria) na kutengeneza kondo la nyuma(placenta) linalotumika kumlisha mtoto, kumpa hewa safi ya oksigeni na kuondoa uchafu anaozalisha mtoto kwa maisha yake yote anapokuwa tumboni kwa mama.

 

Mara nyingi magonjwa ya kuta hizi huwa sio saratani lakini baadhi huwa na tabia ya kubadilika na kuwa saratani

Magonjwa yote ya kuta za ujauzito yanaweza kutibika na wakati mwingine kupona kabisa kwa asilimia mia

 

Magonjwa haya hutokea sana kwenye nchi ya ufilipino, pia kutokana na data zilizofanyika huko marekani zinaonyesha kwamba hutokea kwa mama mmoja kati ya 1000.

 

​

Dalili gani unazoweza kuonesha?

 

Dalili zake maranyingi huwa sawa na zile za ujauzito lakini huzidi kwa makali kwa sababu huzalisha kemikali aina ya HCG kwa wingi ambapo kwenye ujauzito wa kawaida huwa kwa kiwango kidogo

 

Dalili ni kama;

  • Kutapika sana

  • Kifua kuuma-saratani imesambaa kwenye mapafu

  • Maumivu ya nyonga au tumbo- kusambaa kwenye Ini

  • Manjano(kusambaa kwenye Ini na kuziba mirija inayopitisha nyongo)

  • Kutokwa na vitu kama zabibu ukeni pamoja na damu

  • Kutapika damu na kukojoa damu(dalili za ugonjwa kusambaa)

 

Vihatarishi 

  • Kupata mimba kwenye Umri zaidi ya miaka 35 au chini ya miaka 20

  • Historia ya kupata ugonjwa huu

​

Aina za magionjwa haya ni zipi?

  • Hydatidform mole

  • Invansive mole

  • Choriocarcinoma

  • Placenta site trophoblast

​

Hydatidform mole

 

Hujitokeza kwa wingi kuliko aina zingine. Tatizo hili hutokea kwenye kuta za mimba sehemu inayoitwa villae(vitu kama vidole) ambazo hutakiwa kujipenyeza kwenye ukuta wa mfuko wa uzazi na kujishikiza badala yake huvimba kwa kujaa maji na kutengeneza maumbo kama ya zabibu. Si rahisi mtoto kutengenezwa katika aina hii ya ugonjwa na hata kama kunachembe chembe za kuonesha mtoto kufanyika mtoto anayefanyika huwa mfu (asiyekuwa na uhai)

 

Kuna aina mbili za ugonjwa huu ikiwa pamoja na; complete na incomplete mole

 

Complete mole

 

Ni pale ambapo mbegu 1 au 2 kutoka kwa baba zinapevusha yai 1 la mama ambalo halina kitu ndani yake (vinasaba), hivo chembe za uhai za mtoto haziwezi kutengenezwa kwa sababu vinasaba vinatoka kwa baba tu.

 

  • Matibabu kwenye aina hii huhusisha upasuaji kuondoa chembe hizi na mgonjwa 1 kati ya 5 aliyefanyiwa upasuaji, ugonjwa huweza kujirudia tena baada ya muda/miaka flani. Ugonjwa unapojirudia huweza kuwa mbaya zaidi au kutengeneza aina nyingine yenye uwezo wa kuvamia kuta za mfuko wa kizazi na huitwa invasive mole. Aina hii huweza kubadilika na kuwa saratani lakini ni kwa asilimia chache

 

Incomplete mole

 

Mbegu mbili kutoka kwa baba huchavusha yai la mama lililo kamilika (lenye vinasaba), chembe za uhai za mtoto huonekana kwenye aina hii ingawa mtoto anayefanyika huwa hayupo hai. Tafiti zinaonesha pia aina hii huweza kubadilika na kuwa saratani

  • Upasuaji hufanyika kwa matibabu ya kuondoa uvimbe/ugonjwa huu

 

 

Invasive mole

 

Hutokana na ugonjwa wa hydatidform mole ambayo imevamia kuta za mfuko wa uzazi, mara nyingi hutokea kwa mama 1 kati ya wa5 waliofanyiwa upasuaji wa kuondolewa hydatidform mole

 

Vihatarishi vya kupata invasive mole ni nini?

 

  • Kuchelewa kupata matibabu (mda mrefu kupita kutoka siku ya mwisho kuona hedhi/damu ya mwezi ,marayingi zaidi ya miezi 4)

  • Tumbo la uzazi kuongezeka sana(kuwaa kubwa sana)

  • Umri zaidi ya miaka 40

  • Kuwa na Historia ya kuugua ugonjwa huu

 

Ugonjwa huu unapokuwa kwenye kuta za mfuko wa uzazi hutoboa mishipa ya damu na husababisha kuvia kwa damu kwenye viungo vya uzazi vilivyo kwenye nyonga na tumboni, kuvuja huku kwa damu kunaweza kutishia maisha ya mama kwa kusababisha upungufu wa damu.

 

  • Uvimbe huu huondolewa kwa upasuji

  • Uvimbe huu huweza kusambaa sehemu nyingine za mwili kama mapafu kwa mama 1 kati ya 4 wenye tatizo hili hata baada ya kuondolewa uvimbe huu kwa upasuaji

 

  

Choriocarcinoma

 

Aina hii huwa na sifa za saratani na hukua haraka na kusambaa sehemu nyingine za mwili. Choriocarcinoma hutokea kwa kwa asilimia 25 kati ya wanawake waliopata mimba kisha ikatoka yenyewe au kutolewa kwa kukusudia na pia kwenye mimba iliyotungwa kwenye mirija ya kupitisha mayai (falopian tube) badala ya mfuko wa uzazi. Robo nyingine hutokea kwa wanawake waliowahi kujifungua kawaida bila tatizo lolote.

 

Mara nyingine ugonjwa huu huweza kutokea sehemu nyingine mbali na kuta za mimba. Hutokea pia kwa wanaume maeneo ya korodani(testis), kifuani, tumboni na kwenye kiwanda cha kuzalisha mayai(ovary) kwa wanawake

 

Ugonjwa huu maranyingi huwa hautibiki kwa dawa kwa sababu dawa hushindwa kuuondoa.

 

​ 

 

Placenta site trophoblastic disease

 

Aina hii ni nadra sana kutokea. Hutokea kwenye ukuta wa ndani wa mfuko wa uzazi (sehemu ambapo kondo la nyuma hujishikiza katika mfuko wa uzazi), na hutokea baada ya kupata ujauzito au baada ya mimba kutoka, pia aina hii huweza kutokea baada ya kutokea kwa aina ile ya kwanza (hydatidform mole).

 

  • Mara nyingi huwa haina tabia ya kusambaa sehemu nyingine za mwili lakini huvamia kuta za ndani zaidi za mfuko wa uzazi

  • Ugonjwa huu pia hausikii dawa hivyo hutolewa kwa njia ya upa

 

 

Imechapishwa 3/3/2015

Imeboreshwa 7/2/2019

bottom of page