top of page
Sayatika-ulyclinic

Imeandikwa na daktari wa ULY CLINIC

​

Sayatika

 

Utangulizi

​

Sayatika ni maumivu ya mwili yanayoanzia kwenye mshipa mkubwa wa neva ufahamikao kwa jina la neva ya sciatic. Mshipa huu huanzia kwenye maeneo ya chini ya mgongo maeneo karibu na kiuno kwa nyuma na kwenda  kwenye mguu. Kila upande wa mwili wa binadamu una mshipa wa neva ya sciatic.

​

Mshipa wa sciatic huongoza kazi muhimu za kuitikia maumivu, kupeleka taarifa za misuli kujongea n.k. mtu mwenye maumivu ya sayatika huhisi maumivu kwenye eneo chini ya mgongo yanayosambaa upande mmoja wa tako, paja hadi magotini au mpaka kwenye kanyagio la mguu na wakati mwingi maumivu hayo yanaweza kuwa makali unapokaa, kukohoa, kupiga chafya au kuamshwa tu unapokuwa unakaa.

 

Dalili za sayatika

​

Dalili za sayatika huonekana ghafla na huweza kudumu kwa muda wa siku chache au wiki kadhaa. Dalili hizo ni;

​

  • Maumivu makali yanayoanzia chini ya mgongo upande mmoja yanayosambaa kuelekea matakoni, na kwenye mguu mmoja upande wa nyuma

  • Maumivu yanaweza kuwa kiasi, makali au wakati mwingine kuhisi kama umepigwa shoti ya umeme

  • Maumivu huweza kuzidishwa endapo mtu atakaa, kupiga chafya au kukohoa

  • Huweza kuambatana na ganzi kwenye mguu, mguu kuwa dhaifu au kuhisi vitu vinachomachoma kwenye mguu mmoja

 

Endelea kusoma kwa kubonyeza  visababishi, vihtarishi, vipimo, matibabu, matibabu ya nyumbani, madhara na kinga

​

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma makala hii.

 

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushairi na Tiba, bonyeza Pata Tiba au piga namba za simu chini ya tovuti hii.

​

Rejea za mada hii,

​

  1. Evaluation of low back pain in adults. http://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 08.08.2020

  2. Spinal manipulation in the treatment of musculoskeletal pain. http://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 08.08.2020

  3. Acupuncture for pain. National Center for Complementary and Alternative Medicine. http://nccam.nih.gov/health/acupuncture/acupuncture-for-pain.htm. Imechukuliwa 08.08.2020

  4.  Lumbosacral radiculopathy: Pathophysiology, clinical features and diagnosis. http://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 08.08.2020

  5. Sciatica. American Academy of Orthopaedic Surgeons. http://orthoinfo.aaos.org/topic.cfm?topic=a00351. Imechukuliwa 08.08.2020

  6. Levin K, et al. Acute lumbosacral radiculopathy: Prognosis and treatment. http://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 08.08.2020

  7. Sciatica. Merck Manual Professional Version. https://www.merckmanuals.com/professional/musculoskeletal-and-connective-tissue-disorders/neck-and-back-pain/sciatica. Imechukuliwa 08.08.2020

bottom of page