Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Sospeter M, MD
10 Juni 2020, 14:57:04
Kushusha shinikizo la damu pasipo kutumia dawa
Kuna njia nyingi unaweza tumia kushusha shinikizo la damu endapo hutaki tumia dawa;
Kwa kula vyakula vyenye mboga za majani kwa wingi, matunda na mbegu. Fuata ushauri wa mlo maalumu kama ilivyoelezewa katika makala hii. Kumbuka kwenye makala hii imeelezewa taarifa za awali tu, taarifa zaidi zinapatikana kwenye makala zingine za ULY CLINIC
Mlo Maalumu wa kushusha shinikizo la damu
Kula matunda (Milo mitano kwa siku)
Tumia matunda yenye ukubwa wa kati au tumia robo kikombe cha matunda ya kukaushwa
Tumia mboga za majani ( milo mine hadi mitano kwa siku)
Unaweza kutumia kikombe kimoja cha mboga za kijani ambazo hazijapikwa au nusu kikombe kilichopikwa au nusu kikombe cha juisi ya mboga za majani
Tumia mbegu za mimea isiyokobolewa( Kula mara saba hadi nane kwa siku)
Tumia slesi moja ya mkate usiokobolewa au tumia kikombe kimoja cha mbegu zisizokobolewa au nusu kikombe cha ugali au wali uliopikwa
Tumia kwa kiasi vitu vifuatavyo
Mafuta kiasi(mara 2 hadi tatu kwa siku); mfano tumia maziwa kiasi cha mililita 250 au kikombe kimoja cha maziwa mgando yenye mafuta kiasi au kikombe kimoja na nusu cha samli yenye mafuta kiasi
Nyama ya steki( Mara mbili kwa siku); Inaweza kuwa nyama ya ng’ombe isiyo na mafuta, nyama ya kuku, samaki au ndege alochunwa ngozi kuondoa mafuta, nyama ya kitimoto ilotolewa ngozi yenye mafuta.
Tumia mbegu, karanga na maharagwe( mara nne hadi tano kwa siku); tumia nusu kikombe au mililita 14 za mafuta ya karanga
Mafuta na mafuta ya wanyama
Tumia mafuta ya magarini kijiko kimoja cha chakula au mayonaizi kijiko kimoja cha chakula au liviko viwili vya saladi au kijiko kimoja cha mafuta ya mimea
Tumia vyakula vyenye kolestro kiasi; tumia sehemu nyeupe ya mayai mawili ambayo hayajakaangwa na yakienyeji
Tumia kwa kiasi nyama nyekundu
Tumia gramu 85 mara tatu kwa wiki
Vinywaji vyenye sukari na vile vya kusindikwa(tumia mara tano kwa wiki)
Tumia sukari kijiko kimoja cha chakula au jamu kijiko kimoja cha chakula au nusu mililita 14 za juisi ya limao yenyesukari.
Punguza kiasi cha chumvi
Usile chumvi zaidi ya miligramu 2400 kwa siku
Vidokezo vya kuangalia na kuzingatia kiwango cha chumvu kwenye vyakula;
Angalia lebo za vyakula viavyouzwa madukani kuona kiwango cha chumvi, kasha zingatia kiwango cha chumvi unachotakiwa kula, usile kuliko kawaida unayotakiwa kwa siku.
Zuia kula vyakula vilivyosindikwa, vilivyofungashwa, maharagwe ya kukaushwa, mbaazi au kunde zilizokaushwa
Chagua kula vyakula vyenye kiwango kidogo cha unsaturated fat au venye chumvi ya sodiamu kwa kiasi au supu yenye chumvi kiasi.
Zuia kula mboga za majnai zilizosindikwa au zilizoongezewa chumvi
Usitumie chumvi wakati unakula
Tumia viungo na viungo asilia kuimarisha radha asilia ya chakula
Usiweke chakula chumvi kabla ya kuonja
Kula viazi vyenye chumvi kiasi kama bisibisi, au nyama au kitimoto au vyakula vilivyosindikwa
Mazoezi
Jihusishe kwenye mazoezi ya wastani na makali yaaerobiki mara tatu hadi nne kwa siku kwa wastani wa dakika 30 hadi 40 kwa kila zoezi. Mfano wa mazoezi ya aerobiki ni kama;
Kuendesha baiskeli
Kutembea
Kucheza
Kupalilia bustani
Kucehza gofu
Kukimbia
Kuogelea
Kucheza tenisi au mpira
Punguza uzito
Punguza uzito kwa kuongea na daktari wako namna gani upungue na upunguze uzito kiasi gani.
Acha kuvuta sigara
Zuia kiwango cha pombe unachokunywa kwa siku- kwa wanaume wasinywe zaidi ya mililita 60 kwa siku na wanawake si zaidi ya mililita 30 kwa siku. Soma zaidi kuhusu kiwango cha pombe kinachoruhusiwa kwenye makala za ulyclinic
Uwe na muda wa tafakuri
Pata muda wa tafakuri kwa kufanya maombi, kufanya yoga. Kuutuliza mwili na akili hufanya kupungua kwa shinikizo la damu.
Jipime shinikizo la damu ukiwa nyumbani
Ongea na daktari kukuelezea maana ya shinikizo lako la damu na pia ongea naye ujue ni nini matarajio ya matibabu ya shinikizo lako la damu na endpao matibabu yameshusha shinikizo la damu kwa kiwango kinachotakiwa kwako. Jifunze namba ya kupima shinikizo la damu kwa kubofya hapa
Kama una shida ya kukosa hewa wakati wa kulala, hakikisha unatumia mashine ya kukusaidia kupata hewa vema kila siku.
Soma zaidinamna ya kuandaa milo maalumu kwa kubonyeza kwenye menyu upande wa kushoto au chini ta maelezo haya
Imeboreshwa,
6 Oktoba 2021, 11:08:38
ULY Clinic inakushauri siku zote usichukue hatua yoyote ile inayoathiri afya yako bila kuwasiliana na daktari wako.
Wasiliana na daktari wa ULY CLinic kwa kubonyeza 'Pata Tiba' au kutumia namba za simu chini ya tovuti hii kwa elimu suhauri na Tiba
Rejea za mada hii,
​
-
Beckett NS, Peters R, Fletcher AE, et al; HYVET Study Group. Treatment of hypertension in patients 80 years of age or older. N Engl J Med. 2008;358(18):1887-1898.PubMedGoogle ScholarCrossref. Imechukuliwa 09.06.2020
-
SHEP Cooperative Research Group. Prevention of stroke by antihypertensive drug treatment in older persons with isolated systolic hypertension: final results of the Systolic Hypertension in the Elderly Program (SHEP). JAMA. 1991;265(24):3255-3264. ArticlePubMedGoogle ScholarCrossref. Imechukuliwa 09.06.2020
-
Institute of Medicine. Clinical Practice Guidelines We Can Trust. Washington, DC: National Academies Press; 2011. http://www.iom.edu/Reports/2011/Clinical-Practice-Guidelines-We-Can-Trust.aspx. Imechukuliwa 09.06.2020
-
Staessen JA, Fagard R, Thijs L, et al; The Systolic Hypertension in Europe (Syst-Eur) Trial Investigators. Randomised double-blind comparison of placebo and active treatment for older patients with isolated systolic hypertension. Lancet. 1997;350(9080):757-764.PubMedGoogle ScholarCrossref. Imechukuliwa 09.06.2020
-
Hsu CC, Sandford BA. The Delphi technique: making sense of consensus. Pract Assess Res Eval. 2007;12(10). http://pareonline.net/pdf/v12n10.pdf. Accessed October 28, 2013.Google Scholar. Imechukuliwa 09.06.2020
-
Institute of Medicine. Finding What Works in Health Care: Standards for Systematic Reviews. Washington, DC: National Academies Press; 2011. http://www.iom.edu/Reports/2011/Finding-What-Works-in-Health-Care-Standards-for-systematic-Reviews.aspx. Imechukuliwa 09.06.2020
-
https://www.uptodate.com/contents/high-blood-pressure-in-adults-beyond-the-basics?topicRef=4415&source=see_link. Imechukuliwa 10.06.2020
-
https://www.uptodate.com/contents/high-blood-pressure-diet-and-weight-beyond-the-basics.Imechukuliwa 10.06.2020
-
Hypertension. https://jamanetwork.com/journals/jama/fullarticle/1791497. Imechukuliwa 11.06.2020
-
Dash Diet- 365 Days of Low Salt, Dash Diet Recipes For Lower Cholesterol, Lower Blood Pressure and Fat Loss Without Medication ( PDFDrive.com )