Imeandikwa na Daktari wa ULY CLINIC
Alhamisi, 23 Aprili 2020
Ovari
Ovari kiungo katika mfumo wa uzazi wa mwanamke ambayo huzalisha mbegu za kike (Ovam) na homoni za kike ambazo ni progesterone na estrogen na homoni zingine. Ovari imetumiwa kama kiwanda cha kuzalisha mayai ya kike na pia kama tezi mojawapo ya endokrini kwenye makal nyingi za ULY clinic.
Ovari moja ya mwanadamu ina wastani wa urefu wa sentimita 3.5, upana wa sentimita 2 na unene wa sentimita 1.
Kwa kawaida mwanamke ana ovari mbili, upande wa kulia na kutoto nje ya mfuko wa kizazi (uterasi). Kila ovari hushikiliwa kwenye mfuko wa uzazi kwa tishu inayoitwa ovariani ligamenti. Hii ni kama kamba ngumu sana inashikilia kila ovari ili ikae karibu na mfuko wa uzazi kwa ajili ya yai linapozalishwa liweze kuingia moja kwa moja kwenye mirija ya falopia.
Kazi za ovari
• Kuzalisha mayai ya kike
• Kuzalisha homoni za kike ambazo ni progesterone estrogen.
• Kuzalisha homoni za relaxin na inhibin.
Kazi za homoni ya estrogen
• Kukuza na kukomaa kwa viungo vya uzazi.
• Kurekebisha na kuwezesha mzunguko sahihi wa hedhi.
• Kuwezesha tabia za kike mfano kuota maziwa, kutanuka nyonga, sauti nyororo n.k
• Kumpa mwanamke hisia za tendo la kujamiana.
Kazi za projestroni
• Kuandaa mfuko wa uzazi kumtunza mtoto akiwa tumboni.
• Kuzuia mimba isiharibike baada ya kuundwa.
Kazi za homoni ya relaxin
Kuongeza ulaini wa mifupa na misuli ya nyonga wakati wa ujauzito ili kusaidia mtoto atoke kirahisi wakati wa kujifungua.
Kazi za homoni ya inhibin
Kuzuia kuzalishwa kwa homoni ya kuchochea mbegu za kike kukomaa inayozalishwa na tezi ya pituitari.
Magonjwa ya ovari
• Maambukizi kwenye ovari (Ophraitizi)
• Ugumba
• Endometriosisi
• Ovariani sisti
• Saratani ya Ovarian epithelia
• Uvimbe wa gemu seli za ovari
• Uvimbe usio satayani wa ovari
• Sindromu ya Polisistiki ovarian
Afya ya uzazi na umri kwa wanawake
Kadri umri wa mwanamke unavyoongezeka na uwezo wa mayai ya kike (ovari) kufanya kazi zake hupungua na hii hupelekea mwanamke kukoma hedhi. Hivyo uwezo wa uzazi kwa mwanamke hupungua kadri umri unavyoongezeka.
Mfumo wa uzazi wa mwanamke hufanya kazi kwa ufanisi wajuu zaidi akiwa na umri kati ya miaka 20 hadi 30. Anapofikia umri wa miaka 45 mabadiliko huanza kutokea katika mzungoko wa hedhi. Pia uwezekano wa kuzaa mtoto mwenye kasoro huongezeka.
Uzalishaji, urutubishaji na ukomo wa mayai ya mwanamke
Uzalishaji wa mayai kwa mwanamke huanza kabla hajazaliwa, japo kua zoezi hili hukomea katika hatua fulani mtoto anapo karibia kuzaliwa. Hivyo mtoto wa kike anapozaliwa anakua ana mayai machanga yanayoweza kufikia milioni 2. Mwendelezo wa kukomaa mayai haya huendelea pale msichana anapofikia umri wa kuvunja ungo. Japokua mengi kati ya mayai haya hufyonzwa na mwili hivyo msichana hubakiawa na mayai karabia elfu 4 anapo vunja ungo.
Kila mwezi (katika mzunguko wa mwanamke) baada ya kuvunja ungo yai moja hukomaa na kuwa tayari kurutubushwa hadi hapo mwanamke atakapofikia umri wa kukoma hedhi. Jumla ya mayai ya mwanamke yanayofanikiwa kukomaa yanakaribia 400 tu katika kipindi chote cha maisha yake. Kukoma kwa mayai ya kike huusisha hatua kadhaa na homoni kadhaa.
Urutubishaji wa mbegu za kike
Baada ya ovari kuachilia mbegu ya kike iliyo komaa (ovam), mbegu hiyo hupokelewa na mirija ya mfuko wa uzazi ( mirija ya falopia) ambamo huwa tayari kurutubishwa na mbegu ya kiume. Ovam husafirishwa kwenye mirija hii ya falopia hadi kwenye mfuko wa uzazi.
Kama ovam (mbegu ya kike) itakua imekutana na mbegu ya kiume basi kijusi kitakua kimetengenzwa na hupandikizwa kwenye ukuta wa mfuko wa uzazi na kuendelea kukua huku mtoto akiumbika.
Ikiwa mbegu ya kiume haikuwepo basi ovam haitarutubishwa badala yake mbegu hiyo hutoka kama hedhi pamoja na mabaki ya ukuta wa uzazi uliobamoka baada yakujiandaa kumtunza mtoto ila hakutengenezwa. Mabaki haya ndiyo huonekana kama damu za hedhi.
Afya ya uzazi na umri kwa wanawake
Kadri umri wa mwanamke unavyoongezeka na uwezo wa mayai ya kike (ovari) kufanya kazi zake hupungua na hii hupelekea mwanamke kukoma hedhi. Hivyo uwezo wa uzazi kwa mwanamke hupungua kadri umri unavyoongezeka.
Mfumo wa uzazi wa mwanamke hufanya kazi kwa ufanisi wajuu zaidi akiwa na umri kati ya miaka 20 hadi 30. Anapofikia umri wa miaka 45 mabadiliko huanza kutokea katika mzungoko wa hedhi. Pia uwezekano wa kuzaa mtoto mwenye kasoro huongezeka.
Wasiliana na daktari wako endapo umeona kuwa una dalili yoyote ile katika maelezo haya kwa ushauri na tiba
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba zaidi kwa kupiga namba za simu chini ya tovuti hii au kubonyeza hapa.
Imeboreshwa,
13 Julai 2021 18:42:20
Rejea za mada hii;