top of page

Imeandikwa na Daktari wa ULY CLINIC

Jumapili, 19 Aprili 2020

Thairoidi

Thairoidi

Tezi ya thairoid ni tezi yenye umbile la kipepeo iliyipo chini ya koromeo la sauti. Tezi hii ina sehemu mbili ambazo tunaweza kuzifananisha na mabawa ya kipepeo, ya kulia na ya kushoto. Kila sehemu ya tezi ya thairoid ina urefu wa sentimita 5, upana sentimita 3 na unene wa sentimita 2. Uzito wa tezi hii kwa mtu mzima ni takribani gramu 30. Sehemu ya kulia na kushoto zimeunganishwa na shingo ndogo iitwayo ismasi.

Tezi ya thairoidi ndiyo tezi pekee yenye uwezo wa kuhifadhi kwa kiasi kikubwa homoni inazo zizalisha kwani huweka akiba ya kutumia hadi kwa siku 100.

Homoni zinazozalishwa na tezi thairoidi

Tezi hii inazalisha homoni tatu ambazo ni;

• Thairoksini(T4)
• Homoni ya thairoid(T3)
• Kalisitonin(calcitonin) kwa kiasi kidogo

Uzalishaji wa homoni ya thairoksini(T4) na homoni ya thairoidi (T4) huitaji madini jotoynayoitwaa Iodine, madini haya hupatikana kwenye vyakula vinavyo patikana baharini na pia kwenye chumvi ya viwandani. (Soma Zaidi kuhusu madini haya kwenye Makala zilizo sehemu nyingine kwenye tovuti hii).

Upungufu wa madini haya mwilini heleta athari mbaya kutokana na kushidnwa kuzalishwa kwa homoni pamoja na uvimbe shingoni unaoitwa Goita.

Dosari na magonjwa ya tezi ya thairoidi

Magonjwa mbalimbali ya tezi ya thairoidi yanaweza kupelekea dosari mbili. Dosari ya kwanza ni kuzalisha homoni nyingi kupita kiasi. Dosari ya pili ni kuzalisha homoni kwa kiwango kidogo kupita kiasi.

Uzalishaji wa homoni za tezi thairoidi nyingi kupita kiasi

Magonjwa yanayopelekea kuzalishwa kwa homoni za thairoidi kwa wingi kupita kiasi.

• Ugonjwa wa Grevu
• Uvimbe kwenye tezi ya thairoidi
• Saratani ya tezi ya thairoidi
• Uvimbe kwenye tezi ya pituitari
• Kiwango kikubwa cha madini joto kupita kawaida kwenye damu

Uzalishaji wa homoni za tezi thairoidi chini ya kiwango

Dawa hali na magonjwa yanayopelekea kuzalishwa kwa homoni za thairoidi chini ya kiasi kinachohitajika;

• Upungufu wa madini moto
• Ugonjwa wa Hashimoto
• MAdhaifu ya tezi ya kuzaliwa nayo
• Matumizi ya Baadhi ya dawa

Wasiliana na daktari wako endapo umeona kuwa una dalili yoyote ile katika maelezo haya kwa ushauri na tiba

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba zaidi kwa kupiga namba za simu chini ya tovuti hii au kubonyeza hapa.

Imeboreshwa,

13 Julai 2021 18:50:47

Rejea za mada hii;

1.Principles of anatomy and physiology twelfth edition by Gerard J. Tortora and Bryan Derrickson page 661.

2.Anatomia McGraw-Hill Human Anatomy and physiology 2001 page 468

3. Teach me anatomy. The thyroid gland. https://teachmeanatomy.info/neck/viscera/thyroid-gland/. Imechukuliwa 18.09.2020

4. webMd. Throid conditions. https://www.webmd.com/women/picture-of-the-thyroid#1. Imechukuliwa 18.09.2020
bottom of page