Imeandikwa na madaktari na mafamasia wa ULY-Clinic
Dawa aina kundi la thiazolidinediones(TZD)
Dawa kwenye kundi hili ni kama
-
Pioglitazone
-
Rosiglitazone
Matumizi
​
Kiongezo kwenye tiba mazoezi na chakula kwa matibabu ya kisukari aina ya 2
Jinsi zinavyofanya kazi
Huongeza hisia ya homoni insulin kwenye chembe za misuli, mafuta na ini.
Taarifa kwa mgonjwa
-
Husababisha kuongezeka uzito
-
Mwili kuvimba
-
Kushuka zaidi kwa kiwango cha sukari kwenye damu zinapotumiwa na madawa mengine ya kisukari ama homoni ya insulin(ila haitokea unapotumia metformin)
-
Huweza kusababisha au kuongeza kasi ya moyo kufeli na hatari ya kutunza maji kwenye mwili
-
Michomo kwenye sinus na koo
-
Misuli kuuma
-
Kichwa kuuma
Tahadhari/madhara makubwa
Boksi jeusi Moyo kufeli sana inahusishwa na dawa ya rosiglitazone
-
Kufeli kwa ini
-
Upungufu wa damu
-
Kuisha kwa mifupa
-
Kutolewa kwa mayai kwa wanawake wanaoanza kuingia kipindi cha koma hedhi
-
Kwenye ujauzito ipo kitengo C
Kundi maalumu
Moyo uliofeli- anza kutumia kwenye dozi ndogo iliyokubaliwa. Matumizi hayatakiwi kwenye kundi la moyo kufeli dalaja la 3 au la 4
Usitumie endapo
-
Moyo kufeli daraja la 3 au la 4
-
Ugonjwa wa ini