Utangulizi
​
Inafamahika kuwa watanzania zaidi ya milioni 23 wanatumia mtandao wa internet kutafuta huduma mbalimbali zikiwemo huduma za afya, hii ni kutokana na taarifa za tafiti za mamlaka ya mawasiliano Tanzania ya mwaka 2017 zilizochapishwa kwenye tovuti ya reuters.com. Tafiti hiyo pia inaonyesha kuwa mwaka 2016 watumiaji wa internet walikuwa milioni 16 na hivyo kila mwaka matumizi ya internet yanaongezeka kwa wastani ya watu milioni 5 hadi 8
​
Kati ya watumiajimilion 23 wa internet, asilimia 82 ya watumiaji hao wanapata huduma za internet kwa kutumia simu ya mkononi na zinazobaki ni watumiaji wa kompyuta.
Kuongezeka kwa matumizi ya internet kwa watanzania huashiria vitu vingi ikiwa ni watu kutafuta suluhisho la mambo mbalimbalikwa njia ya mtandao, kutafuta dawa, elimu n.k
​
Wakati gani tuliopo sasa?
Tupo karne ya 21 Kwa sasa, Dunia ipo kwenye kizazi kinachoitwa kizazi cha Taarifa (information age) ambacho ni kizazi kinachofanya vitu kutokana na taarifa zilizo kwenye mtandao zinazohusu maisha yao ya kila siku, watu wamekuwa wakiuliza kila kitu kwenye mtandao, mfano namna ya kupika chakula aina fulani, namna ya kuendesha gari, nini husababisha maumivu ya kichwa, chakula gani cha kula wagonjwa wa kisukari n.k. Ingawa kwa nchi nyingi za Afrika ikiwa pamoja na Tanzaniia bado tupo nyuma kidogo hasa kutumia tekinolojia kwenye mambo ya Afya, tunaamini siku chache za usoni teknolojia itachukua nafasi yake kwa kiasi kikubwa. Hili linadhihirishwa kwa idadi ya watu wanaotumia simu za mkononi kutafuta taarifa na masuala mbalimbali kwenye mtandao.
​
Uly clinic hapo awali ilikuwa ikiitwa ugonjwa lugha yetu kwa kifupi ilianza mwaka 2015 kama ugonjwa lugha yetu ambapo dr mangwella sospeter kwa kuona wagonjwa wake wanapata shida kuelewa mambo ya kiafya akaamua kuanzisha tovuti ili kuwasaidia waweze kusoma makala mbalimbali kwa lugha ya Kiswahili lakini hakuweza kufikia malengo ya kusambaza taarifa hizo kwa watu wengi kwa sababu mbalimbali. Mwaka 2018 jina la tovuti lilibadilishwa kuwa kuwa kifupi cha Ugonjwa Lugha Yetu Clinic (ULY CLINIC) .
​
Uly clinic Kwa sasa ina application inayoitwa uly clinic inayopatikana google play store ambapo mtumiaji anaweza kuiweka kwenye simu yake na kupata huduma mbalimbali za kiafya kulingana na matakwa ya mabadiliko ya watumiaji na Dunia.
Ni nini malengo ya uly clinic
Uly clinic malengo yake ni kutoa elimu ya Afya kwa wanajamii wa Tanzania na sehemu zote wanapozungumza kiswahuli kwa lugha ya Kiswahili, na kuwawezesha watumiaji wa huduma za afya kupata huduma hizo kwa kirahisi kutoka kwa wataalamu waliobobea kwenye huduma hizo. Mfano mgonjwa kuweza kupata daktari kutoka kwenye eneo la karibu alilopo, Kuulizia nakupata huduma za dawa,kuulizia na kupata huduma za maabara na vipimo, kuulizia na kupata huduma za nesi n.k kupitia simu yake ya mkononi au kompyuta.
​
Tunafanyaje kazi na watu wengine?
Uly clinic tunashirikiana na wataalamu wa afya ikiwa pamoja na madaktari, wafamasia, wauguzi, wataalamu wa lishe n.k katika kutengeneza makala na kutoa elimu ya afya ambayo ni salama na inaendana na tafiti za hivi karibuni ili kumpa mtumiaji huduma bora kulingana na wakati. Endapo kuna mtu anahitaji kufanya kazi nasi kutoa makala za elimu anakaribishwa, pia wanaofanya kazi kwenye tovuti ya uly clinic wanaweza kutoa huduma zao kupitia application ya uly clinic ambayo inapatikana gogogle play store. Matumizi ya tovuti na application ya uly clinic ni bure, Unaweza kutumia Forum ya afya au blog kutoa elimu ya afya kwa jamii ili kufanya watu wafahamu mambo mbalimbali na waweze kukutafuta kwa huduma zako. Pia mtaalamu anaweza kutoa ujumbe mfupi ambao utaonekana kwa wateja kupitia tovuti na application ya uly clinic. Kusoma zaidi namna unavyoweza kunufaika kama ukitumia tovuti na application ya uly clinic kutoa huduma za afya bonyeza linki hii hapa
Unawezaje kujipatia kipato ukiwa uly clinic?
Kwa kuwa tunatoa huduma za afya kwa jamii, kipato ni zawadi ambayo unaweza kupata kutoka kwenye matunda ya miti uliyoipanda. Kwa wanaoshirikiana nasi wanaweza kufaidika kwa njia tofauti ikiwa pamoja na kutangaza biashara zao, mfano kusajili famasi zao bure kwenye applicaton ya uly clinic ili watumiaji wa application hiyo waone huduma na kutafuta huduma toka kwao, hivyo hivyo wanaotoa huduma za tiba hospitali au kama mtu binafsi wanaweza kutumia huduma zetu kutoa huduma, kupokea appointment, kuandika dawa, kushauri, kuwauzia product na kupokea malipo kupitia application hii.
​
Unawezaje kupata wateja wengi zaidi wa bidhaa yako kupitia application yetu?
Kwa kuwa application yetu ina watumiaji wengi, data zinaonyesha kuwa tovuti yetu inatembelewa na watu zaidi ya mia moja kwa siku, hivyo kwa kutumia tovuti yetu unaweza kuuza product au kutoa huduma yoyote. Kwa kuandika makala ambayo itasomwa kisha mwisho wa makala likawekwa jina loko na kitufe kinachomwelekeza mteja apate huduma zako, basi mteja atawasiliana na wewe moja kwa moja ili kupata huduma.
​
Uly clinic endapo utaandika makala nzuri tutakusaidia kuitangazakwa kuweka mashindano ambayo yatafanya watu wasome makala hizo kwa kuwapa zawadi mara watakaposhinda maswali watakayoulizwa kwenye tovuti.
​
Nani anaweza kujiunga kufanya kazi nasi?
Ili kuzingatia usalama wa mtumiaji na matakwa ya Wizara ya afya, wale wanaotakiwa kutoa huduma ni wataalamu wa afya tu, hivyo lazima uwe na leseni ambayo inakutambulisha kuwa umeruhusiwa kufanya kazi za afya na vyeti vya kitaaluma. Uly clinic tunashirikiana na wizara ya afya katika kuhakikisha kuwa wanaotoa huduma katika tovuti hii ni wataalamu tu na wamesomea kutoa huduma hizo.
​
Mambo mengine tunaweza kukufadhiri kamamtaalamu wa afya ni nini?
Uly clinic tunaweza kukusaidia kuandika kitabu na kuchapisha ili kukiuza, vitabu vinaweza kuhusu huduma mbalimbali za kiafya, ikiwa pamoja na lishe, kisukari, Shinikizo la damu la juu na Ukimwi, Ujauzito, Kutunza mtoto, N.k. Mtu ambaye anahitaji kuandika vitabu atafadhiriwa na kuandikishana mkataba nasi.
​
Namna gani unaweza kujiunga nasi kuwa mnufaika
Kujiunga nasi ingia kwenye tovuti sehemu imeandikwa fanya kazi nasi kisha bonyeza sehemu imeandikwa jisajili hapa na kisha tuma taarifa zako, Unaweza kutuma email pia kupitia email zilizo chini ya tovuti yetu.
​
Kuna nafasi ya kujiunga kama mmiliki?
Endapo unataka kuwa mmiliki wa application na tovuti hii unakaribishwa.
Ukiwa una maswali zaidi usisite kutuuliza kupitia mawasiliano yetu
Karibu sana uly clinic.
​
Dr. Mangwella sospeter, MD
CEO uly clinic
Kurasa zetu za facebook zinatembelewa na kuonywa na watu wengi kila siku
Kurasa zetu za facebook zinatembelewa na kuonywa na watu wengi kila siku
Kurasa zetu za facebook zinatembelewa na kuonywa na watu wengi kila siku
Kurasa zetu za facebook zinatembelewa na kuonywa na watu wengi kila siku