Imeandikwa na daktari wa ULY CLINIC
​
Uchafu wa bluu, kijani na bluu- kijani kweye nguo
​
Makala hii imejikita kuzungumzia tatizo la ngozi lijulikanalo kama intertrigo au demataitizi ya maeneo ya mikunjo ya mwili
​
Intertrigo ni moja ya ugonjwa wa ngozi, husababishwa na michomo inayotokea kwenye maeneo ya mikunjo ya mwili na yenye misuguno kama vile maeneo ya kwapa, kinena, maeneo ya maungio ya mapaja na kiwiliwili, maeneo ya siri. Maeneo kati ya kidole na kidole n.k
Ugonjwa huu wa ngozi unaweza ambatana na dalili za kuchafua nguo za ndani kwa rangi ya bluu, bluu-kijani au kijani katika maeneo mbalimbali. Rangi hiyo inaweza kuonekana kwenye nguo kama chupi, brazia, kola au maeneo ya kwapa ya shati. Dalili hizi hutokea pale tu endapo ugonjwa wa intertrigo umeambatana na maambukizi ya bakteria jamii ya pseudomonas aeruginosa.
​
Dalili za Intertrigo
​
Dalili za intertigo huwa pamoja na;
​
Kuchafua nguo za ndani na uchafu wa rangi ya bluu, kijani na blue kijani kweye maeneo yenye mikunjo kama yalivyotaja hapa chini na kuwa na Harara kwenye ngozi (kwa watu wenye rangi nyeupe, ngozi huonekana yenye rangi nyekundu au kahawia) katika maeneo yenye misuguno na mikunjo au yanayotunza unyevu ambayo ni;
​​
-
Katikati ya vidole vya miuu
-
Kwapani
-
KWenye kinena
-
Chini ya tumbo
-
Kwenye mikunjo ya shigo
-
Maeneo katikati ya matako
-
Maeneo chini ya matiti
​
Viamshi vya Intertrigo
​
Viamsha ugonjwa huu kwenye maeneo yaliyotajwa hapo juu ni;
-
Joto
-
Unyevunyevu
-
Misuguano
-
Kukosekana kwa mzunguko wa hewa
​
Maeneo yenye ugonjwa huu huweza vamiwa au kuambukizwa na vimelea na vijidudu kama fangasi jamii ya candida, bakteria, virusi. Hii ndio maana wagonjwa wenye intertrigo
​
Namna ya kujikinga
​
Unaweza kufanya mambo yafuatayo kujikinga na tatizo hili la Intertrigo
-
Fanya ngozi ya maeneo ya hatari kupoa kwa ubaridi na kuwa makavu
-
Usivae nguo za kubana kama tight na chupi, viatu vya kubana na brazia
-
Vaa nguo zinazofyonza unyevuunyevu kama vile nguo za pamba, usivae nguo za nailoni au zingine zilizotengeneza kiwandani
-
Punguza uzito endapo unauzito mkubwa kupita kiasi(obeziti)
-
Baada ya mazoezi oga na jikaushe mara moja, kausha nywele na kikaushio cha umeme, pia kausha maeneo chini ya matiti na kwapa
​
Matibabu ya intertrigo
​
Kwa waonjwa walio wengi, utashauriwa kufanya yawe makavu na kuacha wazi maeneo yenye shida ili yapate hewa safi. Kwa wagonjwa ambao wanapata miwasho hupewa dawa jamii za corticosteroid, kwa wale wenye maambukizi katika maeneo hayo, dawa zingine za antibakteria na fangasi hutumika.
​
Soma makala nyingine zaidi inayofanana na hii kwa kubonyeza hapa
​
ULY CLINCI inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa uchauri zaidi na tiba endapo una tatizo hili
​
Kuendelea kupata tiba au ushauri zaidi kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC tumia namba za simu au bonyeza pata tiba chini ya tovuti hii
​
Imeboreshwa, 25.10.2020
​
Rejea za mada hii,
​
-
Family doctor. Intertrigo. https://familydoctor.org/condition/intertrigo/#. Imechukuliwa 25.10.2020
-
JPMA.Intertrigo. https://jpma.org.pk/article-details/4645. Imechukuliwa 25.10.2020
-
WebMD. Intertrigo. https://www.webmd.com/skin-problems-and-treatments/guide/intertrigo-symptoms-causes-treatment-risk_factors. Imechukuliwa 25.10.2020
-
Mayoclinic. Intertrigo. https://www.mayoclinic.org/skin-rash/sls-20077087?s=6#. Imechukuliwa 25.10.2020