top of page
saratani ya ulimi- ulyclinic

Imeandikwa na daktari wa ULY CLINIC

 

Saratani ya ulimi

 

Aina kadhaa za saratani zinaweza kuathiri ulimi na mara nyingi huanzia kwenye ukuta wa ngozi ya ulimi uliotengenezwa na seli za squamous. Matibabu na hatima ya saratani ya ulimi hutegemea aina ya saratani iliyoathiri ulimi. Saratani ya ulimi inayotokea sehemu za mdomo ambapo itakuwa rahisi kuonekana kwa macho huweza kutibiwa mapema mara inapoonekana na kuzuia madhara, saratani ya ulimi inayotokea nyuma karibu na koo au kwenye shina la ulimi si rahisi kuonekana na hivyo huweza kugunduliwa katika hatua za juu Zaidi wakati tatizo tayari limeshakuwa kubwa.

 

Dalili za saratani ya ulimi hutegemea hatua ya sawatani, baadhi yake ni;

​

  • Kidonda kwenye ulimi ambacho hakiponi

  • Uvimbe kwenye ulimi

  • Maumivu ya ulimi yanayoambatana na uvimbe au kidonda

  • Maumivu wakati wa kumeza chakula

  • Kumeza kwa shida

  • Mabadiliko ya sauti (kuwa na sauti kama ya farasi au sauti kukauka)

  • Maumivu kwenye taya

  • Kuhisi kitu kinakaba kwenye koo

  • Shida katika kumeza au kutafuna chakula

  • Vidonda kwenye ulimi ambavyo haviponi

  • Ganzi mdomonikutokwa na damu kwenye ulimi bila sababu

  • Uvimbe kwenye ulimi ambao hauondoki

 

Vihatarishi vya kupata saratani ya ulimi

​

Vitu vifuatavyo vinaonekana kuhusiana na saratani ya ulimi

​

  • Matumizi ya tumbaku na mazao yatokanayo na tumbaku kama sigara n.k

  • Matumizi ya pombe kupita kiasi

  • Maambukizi ya kirusi cha HPV (huambukizwa kwa njia ya kujamiana au kubusiana)

  • Kushuka kwa kinga mwilini

  • Kula vyakula visivyo na matunda na mboga za majani kwa wingi

  • Kula nyama nyekundu kwa wingi

  • Kuwa na historia kwenye familia ya saratani ya ulimi

  • Kuwa na saratani nyingine mwilini

  • Ugonjwa wa kucheua tindikali(GERD)

  • Matumizi au kuishi kwenye mazingira yenye kemikali za asbestos, sulfuric acid, na formaldehyde

  • Kutosafisha kinywa vema

 

Utambuzi na vipimo

​

Daktari atakapohisi una dalili za saratani atakuuliza kuhusu vihatarishi vya saratani pamoja na dalili zingine. Baad aya mjadala wa maswali, daktari atachukua sehemu ya nyama ya ulimi iliyo na saratani kisha kwenda kuipima kipimo cha iospy. Endapo kipimo cha biopsy kimesema kuwa una saratani basi utashauriw akuhusu kufanya vipimo vingine kuonyesha hatua ya ugonjwa au kusaidia kutoa uamuzi wa matibabu yatakayokufaa. Vipimo hivyo vinaweza kuwa CT scan au MRI

​

​

Matibabu

​

Matibabu ya saratani ya ulimi hutegemea hatua ya saratani, yapo matibabu ya upasuaji au upasuaji pamoja na dawa za chemotherapy na mionzi. Daktari atafanya upasuaji kuondoa uvimbe wa saratani au kuondoa ulimi wote endapo hatua ni za awali. Mara baada ya upasuaji utabidi kufundishwa namna ya kuwasiliana maana uwezo wako wa kuongea utaathiriwa na matibabu aina hii ya upasuaji.

​

​

Je saratani ya ulimi inatiba ya kuponya kabisa?

​

Endapo saratani imegunduliwa katika hatua  awali, jibu ni ndio, endapo saratani imegunduliwa hatua za mwishoni na imeshasambaa kwenye maeneo jirani au mbali, saratani hii haiwezi kutibika kabisa.

​

​

Kujikinga

​

​

Ni ngumu kujikinga na saratani ya ulimi, lakini endapo utafanya mambo yafuatayo unaweza kujikinga na kihatarishi cha kupata saratani hiyo;

​

  • Acha kutumia tumbaku na mazao yatokanayo na tumbaku kama sigara n.k

  • Tumia pombe kwenye kiwango kinachoshauriwa au acha kabisa

  • Ushishiriki ngono ya kuhusisha kunyonya uke au mboo (ngono kinyume na maumbile) au pima kwanza magonjwa yote ya zinaa kabla ya kufanya ngono hizi ili uepuke maambukizi ya kirusi cha cha HPV

  • Kula mlo kamili na pata matibabu unapoumwa ili kuepuka Kushuka kwa kinga mwilini

  • Kula vyakula vilivyo na matunda na mboga za majani kwa wingi na nyama nyekundu kw akiasi kidogo

  • Pata matibabu ya tatizo la Ugonjwa wa kucheua tindikali(GERD)

  • Jikinge au vaa vitu vya kukusaidia kuepukana na kemikali hizi hatari za asbestos, sulfuric acid, na formaldehyde

  • Safisha kinywa chako kila unapomaliza kula kwa kutumia dawa ya meno na kuchukutua kinywa

  • Pata matibabu mara unapopata dalili za matatizo kwenye ulimi kwa kumwona mtaalamu wa afya

​

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua uamuzi wowote ule wa kiafya

​

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri zaidi na vipimo kwa kubonyeza pata tiba au kupiga namba za simu chini ya tovuti hii

​

Imeboreshwa mara ya mwisho, 07.08.2020

​

Rejea za mada hii,

​

  1. Cancer stat facts: Oral cavity and pharynx cancer. (n.d.) https://seer.cancer.gov/statfacts/html/oralcav.html. Imechukuliwa 07.08.2020

  2. Head and neck cancers. (n.d.) http://www.nccn.org/professionals/physician_gls/f_guidelines.asp

  3. Mouth and oropharyngeal cancer: Coping. (2018, May 11) http://cancerresearchuk.org/about-cancer/mouth-cancer/living-with/coping. Imechukuliwa 07.08.2020

  4. NCI dictionary of cancer terms: Squamous cell carcinoma. (n.d.) http://cancer.gov/publications/dictionaries/cancer-terms?cdrid=46595. Imechukuliwa 07.08.2020

  5. Oral cancer. (n.d.) http://mdanderson.org/patients-family/diagnosis-treatment/cancer-types/oral-cancer.html. Imechukuliwa 07.08.2020

  6. Oral cancer facts. (n.d.) http://oralcancerfoundation.org/facts/. Imechukuliwa 07.08.2020

  7. Oral cancer incidence (new cases) by age, race, and gender. (2018, February)

    http://nidcr.nih.gov/DataStatistics/FindDataByTopic/OralCancer/OralCancerIncidence.htm.Imechukuliwa 07.08.2020

bottom of page