top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Helen L, M.D

Jumamosi, 30 Januari 2021

 Karanga ya Lozi huondoa wasiwasi na kuleta usingizi

Karanga ya Lozi huondoa wasiwasi na kuleta usingizi

Tumia gramu 28 sawa na karanga 12 za lozi kila siku ili kupunguza na kutibu tatizo la kukosa usingizi na wasiwasi uliopitiliza. Karanga hii huongeza kiwango cha hormoni serotonin, homoni inayokufanya uwe mtulivu na ulale usingizi mwororo.


Homoni ya utulivu na usingizi mwororo


Tafiti zinaonyesha kuwa, upungufu wa madini ya magnesium mwilini, hupunguza kiwango cha homoni serotonin, matumizi ya vyakula vyenye madini hayo kwa wingi huongeza kiasi cha homoni hiyo. Endapo kiwango cha homoni serotonin kinatolewa kwenye damu kama inavyotakiwa, dalili za wasiwasi uliopitiliza na kukosa usingizi hupungua ama kupotea kabisa. Matumizi ya karanga ya lozi (almond) huongeza kwa kisi kikubwa kiwango cha madini ya magnesium.


Matumizi ya karanga ya lozi


Karanga ya lozi huwa na kiwango kikubwa cha madini ya magnesium, endapo utatumia karanga 12, utakuwa umepata miligramu 75 za magnesium, sawa na asilimia 19 ya madini ya magnesium unayohitaji kwa siku.


Unaweza kutumia karanga ya lozi katika chakula, mfano chukua karanga 12 zikaange kisha kuzila na maziwa mgando kama mlo wako wa usiku. Au


Tafuna karanga pekea yake au kula na matunda mengine

Virutubisho na madini mengine kwenye karanga ya lozi


  • Huwa na nyuzinyuzi

  • Proteini

  • Mafuta yenye lehamu nzuri

  • Vitamin E

  • Madini ya Manganese

  • Madini shaba

  • Vitamin B2 (riboflavin)

  • Madini ya fosforasi


Maelezo ya ziada kuhusu matumizi ya lozi


Kwa maelezo zaidi namna ya kutumia karanga ya lozi kama chakula, ingia kwenye Makala zingine za namna ya kuandaa chakula cha lozi ndani ya makala hii.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

19 Julai 2023 20:41:55

Rejea za mada hii:

1. Magnesium for depression. http://www.george-eby-research.com/html/magnesium-for-depression.pdf. Imechukuliwa 28.01.2021
2. Nutritional strategies to ease anxiety. https://www.health.harvard.edu/blog/nutritional-strategies-to-ease-anxiety-201604139441. Imechukuliwa 28.01.2021
3. Peter Pribis. Effects of Walnut Consumption on Mood in Young Adults—A Randomized Controlled Trial. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC5133056/. Imechukuliwa 28.01.2021
4. Heather M. Francis, etal. A brief diet intervention can reduce symptoms of depression in young adults – A randomised controlled trial. https://journals.plos.org/plosone/article?id=10.1371/journal.pone.0222768. Imechukuliwa 28.01.2021
5. Abdulrahman Al-Sayari, etal. The antidepressant-like effect of almond oil: An additive effect with lavender oil. https://www.alliedacademies.org/articles/the-antidepressantlike-effect-of-almond-oil-an-additive-effect-with-lavender-oil-10857.html. Imechukuliwa 28.01.2021

bottom of page