top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Helen L, M.D

Jumatatu, 8 Februari 2021

Acha mazoea ya kutumia dawa za maumivu jamii ya NSAIDS

Acha mazoea ya kutumia dawa za maumivu jamii ya NSAIDS

Asilimia 15 ya watumiaji wa dawa za kupunguza maumivu jamii ya NSAIDS kama Ibuprofen, Indomethacin, aspirin, naproxen n.k, wana hatari ya kupata vidonda vya tumbo vinavyopelekea kutapika damu. Tumia njia mbadala au tumia dawa za maumivu inapolazimika.


Madhara ya dawa za maumivu


Dawa za maumivu jamii ya NSAIDs huharibu ukuta wa juu ya tumbo kwa njia mbili, kwanza kwa kuwa dawa za NSAIDS huwa na asili ya tindikali, huharibu ukuta wa juu ndani ya tumbo, pili dawa jamaii hii huzuia uzalishaji wa prostaglandin, kemikali ambayo huzuia uzalishaji wa tindikali tumboni na kuongeza uzalishaji wa 'bicarbonate' pamoja na ute unaofunika ndani ya tumbo. Matumizi ya dawa za maumivu kwa muda mrefu husababisha mtumiaji kupata vidonda vya tumbo vinavyopelekea kutapika damu.


Endao una tatizo la maumivu, ni vema ukatumia njia zingine mbadala badala ya kutumia njia ya dawa hizi kwa muda mrefu. Endapo una maumivu ya wastani, usitumie dawa za maumivu zaidi ya siku mbili au tatu. Na endapo una maumivu makali, wasiliana na daktari wako kwa uwezekano wa kutumia dawa za kuzuia uzalishaji wa tindikali pamoja na dawa za maumivu ili kupunguza madhara yanayoweza kuletwa na dawa za maumivu


Tafiti zinaonyesha hatari ya watumiaji kupata tatizo la kutapika damu kutokana na matumizi ya dawa jamii ya NSAIDs ni mtu mmoja kati ya watu 100 kwa kila mwaka.


Dawa jamii ya NSAIDs


Baadhi ya dawa jamii ya NSAIDs ni;


  • Aspirin,

  • Indomethacin (indocin),

  • Ibuprofen (motrin),

  • Naproxen (naprosyn),

  • Piroxicam (feldene),

  • Nabumetone (relafen), na

  • Celecoxib (celebrex)


Kinga


Ili kukikinga na madhara ya dawa hizi ni vema ukazingatia


  • Kuacha kutumia dawa jamii ya NSAIDS kwa muda mrefu

  • Endapo unashindwa kuepuka, tumia dawa hizi pamoja na dawa za kuzuia uzalishaji wa tindikali kama omeprazole, au cimetidine n.k

  • Kupata tiba ya vidonda vya tumbo kwa kumwangamiza bakteria wa H.pyrol

  • Kutumia dawa zinazoimarisha mfumo wa ute ndani ya tumbo kama misoprostol wakati unatumia dawa hizi

  • Kutumia vyakula vinavyoongeza ute kwenye ukuta wa tumbo kama maji ya bamia

  • Kusoma makala za kiafya kuhusu masuala mbalimbali ya dawa na tiba yake


Njia mbadala za kupunguza maumivu


Jikande kwa maji ya moto au baridi. Tumia barafu au kitambaa kilichochovya kwenye maji ya moto au chupa ya maji ya moto kujikanda katika eneo lenye majeraha au maumivu. Mfano endapo una maumivu ya hedhu, tumia chupa ya maji moto kujikanda kwenye maeneo ya chini ya kitovu nah ii itasaidia kuondoa maumivu hayo


Fanya mazoezi.

Mazoezi hufanya kazi kubwa ya kukabili mfumo wa maumivu mwilini na kupunguza maumivu sugu yanayotokea kwa wagonjwa wenye magonjwa sugu kama maumivu ya maungio na misuli n.k. Unaweza kufanya mazoezi ya kawaida kwama kuogelea, kuendesha baiskeli kutembea n.k


Mazoezi ya viungo.

Kufanya mazoezi maalumu ya kuodoa maumivu katika mfumo fulani wa mwili husaidia sana kupunguza maumivu. Kuna aina kadhaa za mazoezi ya viungo yanayoweza kuondoa maumivu ya mwili ambayo utafundishwa na mtaalamu wako wa mazoezi ya viungo.


Kutuliza mwili na akili.

Endapo utajifunza kutuliza mwili na akili, kwa kupata muda wa kuingia ndani yako mwenyewe na kudhibiti upumuaji wako, unaweza kudhibiti hisia za maumivu yaliyo mwilini mwako. Hii hupelekea kuondoa au kupunguza maumivu.


Tiba muziki.

Tafiti zinaonyesha kuwa, mziki unaweza saidia punguza maumivu baada ya kufanyiwa upasuaji au baada ya kujifungua. Mziki ambao umeonekana kusababisha kupungua kwa maumivu ni ule aina ya classic. Inaonekana kuwa, kusikiliza muziki aina yoyote ile huhamisha fikra zako dhidi ya maumivu, hivyo kupungua kwa maumivu


Kukandwa (massage).

‘Massage’ hupunguza maumivu kwa kuondoa msongo kwenye misuli, maungio ya mwili na pia husaidia kuondoa akili yako kufikiria kuhusu maumivu yaliyopo.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

19 Julai 2023 20:41:33

Rejea za mada hii:

1.Musa Drini, et al. Peptic ulcer disease and non-steroidal anti-inflammatory drugs. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC5478398/. Imechukuliwa 08.02.2021

2.J L Wallace. How do NSAIDs cause ulcer disease?. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/10749095/. Imechukuliwa 08.02.2021

3.R I Russell. Non-steroidal anti-inflammatory drugs and gastrointestinal damage—problems and solutions FREE. https://pmj.bmj.com/content/77/904/82. Imechukuliwa 08.02.2021

4.M M Cohen. Role of endogenous prostaglandins in gastric secretion and mucosal defense. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/3040310/#:. Imechukuliwa 08.02.2021

5.John L. Wallace . Prostaglandins, NSAIDs, and Gastric Mucosal Protection: Why Doesn't the Stomach Digest Itself?. https://journals.physiology.org/doi/full/10.1152/physrev.00004.2008. Imechukuliwa 08.02.2021

6.Harvard health publishing. 8 non-invasive pain relief techniques that really work. https://www.health.harvard.edu/pain/8-non-invasive-pain-relief-techniques-that-really-work. Imechukuliwa 09.02.2021

bottom of page