Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, M.D
Mhariri:
Dkt. Adolf S, M.D
Jumapili, 23 Julai 2023
Aina za PEP zinazotumika
Dawa za PEP zinazotumika huwa na mchanganyiko wa dawa ambao ni tenofovir na emtricitabine na raltegravir au na dolutegravir au na darunavir na ritonavir.
Aina za PEP
Kuna aina kadhaa za PEP zilizopendekezwa kutumika ambayo huwa na mchanganyiko wa dawa mbalimbali. Mchanganyiko huo umeelezewa hapa chini:
1. Mchanganyiko unaotumika mwa vijana wadogo na watu wazima wenye afya
Tenofovir disoproxil fumarate (TDF)(300 mg) na emtricitabine (F)(200 mg) mara moja kwa siku
Na
Raltegravir (RAL)(400 mg) mara mbili kwa siku au mbadala wake ni Dolutegravir (DTG)(50 mg) mara moja kwa siku
2. Mchanganyiko mbadala unaotumika kwa vijana wadogo na watu wenye afya
TDF (300 mg) na F (200 mg) mara moja kwa siku
Na
Darunavir (DRV)(800 mg) na ritonavir (RTV)(100 mg) mara moja kwa siku
3. Mchanganyiko kwa ajili ya watoto chini ya miaka 11
Zidovidune (AZT) na lamivudine (3TC) kama uti wa mgongo
Na
Lopinavir yenye Ritonavir (LPV/r)
4. Mchanganyiko mbadala unaotumika kwa vijana wadogo na watu wenye afya
Mchanganyiko kwa watu wazima unaopendekezwa na Shirika la Afya Ulimwenguni ni:
Tenofovir na amivudine (3TC) au emtricitabine (FTC) kama uti wa mgongo
Na
Ritonavir yenye lopinavir (LPV/r)
Dozi ya kila dawa
Tenofovir disoproxil fumarate (TDF)(300 mg) mara moja kwa siku
Emtricitabine (200 mg) mara moja kwa siku
Raltegravir (400 mg) mara mbili kwa siku
Dolutegravir (50 mg) mara moja kwa siku
Darunavir (800 mg) Mara moja kwa siku
Ritonavir (100 mg) mara moja kwa siku
Lamivudine 300mg mara moja kwa siku au 150 mg mara mbili kwa siku
Lopinavir yenye ritonavir 800mg/200mg mara moja kwa siku
Vifupisho vya dawa
Unaweza kuandikiwa vifupisho vifuatavyo kumaanisha dawa za PEP za kufubaza maambukizi ya Virusi vya UKIMWI.
TDF- Tenofovir disoproxil fumarate
F- Emtricitabine
RAL- Raltegravir
DTG- Dolutegravir
DRV- Darunavir
RTV- Ritonavir
AZT- ZIdovudine
3TC- Lamivudine
LPV/r- Ritonavir yenye lopinavir
Dawa Muunganiko
Tenofovir disoproxil fumarate (TDF)(300 mg) mara moja kwa siku na Emtricitabine (F)(200 mg) mara moja kwa siku hupatikana kama muunganiko wa dawa inayoitwa Truvada.
Dozi ya PEP hutumika kwa muda gani?
Nchi nyingi zinatumia mwongozo wa Shirika la Afya Ulimwenguni na CDC kutoa PEP kwa angalau siku 28. Kwa Tanzania pia PEP inatumika kwa siku 28 mfululizo. Uamuzi wa ogezeko la idadi ya siku za kutumia PEP hutolewa na daktari endapo kuna sababu za msingi zimetokea kwa mgonjwa.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 08:22:02
Rejea za mada hii:
1. How Do I Prescribe PEP?. CDC. https://www.cdc.gov/hiv/clinicians/prevention/prescribe-pep.html. Imechukuliwa 23.07.2023.
2. WHO. PEP GUIDELINES. https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/145719/9789241508193_eng.pdf;jsessionid=85389E4ABFE9273A6C4D7B73442F74C8?sequence=1. Imechukuliwa 23.07.2023.
3. Tanzania Standard Treatment Guideline @2021.