Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Mercy M, CO
Ijumaa, 5 Machi 2021
Alfajiri ni muda mzuri wa kushiriki ngono
Tafiti zinaonyesha kuwa, kiwango cha homoni testosterone inayokupa nguvu za kiume huongezeka kwa kiasi kikubwa kati ya sa moja hadi sa tatu asubuhi. Ongezeko la testosterone alfajiri huwafanya wanaume wengi wawe na nguvu zaidi na kuchelewa kumaliza wanaposhiriki ngono asubuhi. Hii ni kweli kwa wanaume chini ya umri wa miaka 46
Uzalishaji wa homon testosterone
Homon testosterone huzalishwa kwenye tezi za Leyding zinazpatikana kwenye korodani, mwitikio wa uzalishaji huchochewa na homoni zinazozalishwa kwenye ubongo zenye jina la FSH. Homon testosterone inapozalishwa, kiwango kidogo hubadilishw akuwa estriol ambayo hufanya kazi kama testosterone.
Kazi za homon testosterone
Inafahamika kwamba, homon testosterone hufanya kazi nyingi mwilini ikiwa pamoja na;
Kuamsha hisia za kufanya ngono na nguvu za kiume
Kuongeza uzito wa mifupa
Kuhifadhi mafuta sehemu yake kwa wanaume
Kukuza misuli
Kuongeza nguvu za misuli na nguvu za kiume
Kuzalisha chembe nyekundu za damu
Kuchochea uzalishaji wa mbegu za kiume
Mahusiano ya testosterone na kazi zake kwenye tafiti
Tafiti moja iliyofanyika kwa wanaume kwa baadhi yao walipewa dawa za kupunguza kiwango cha homoni testosterone kwenye damu, wengine wakapewa homoni ya ziada zilionesha kwamba;
Wanaume waliokuwa na kiwango kidogo cha homoni waliambatana na dalili ya kuwa na misuli kidogo, kupungua kwa hamu ya kufanya ngono na uzalishaji kidogo wa mbegu za kiume
Wanaume waliokuwa na kiwango kizuri cha homoni kwenye damu, walionekana kuwa na misuli zaidi, wenye nguvu za mwili na kufurahia tendo la ndoa pamoja na uzalishaji wa kutosha wa mbegu za kiume
Vyakula vinavyoongeza uzalishaji wa testosterone na kuongeza nguvu za kiume
Vyakula vinavyoongeza uzalishaji wa homon testosterone ni vile vyenye vitamin D na madini zink kwa wingi. Vyakula hivyo ni pamoja na;
Nyama ya ngombe/nyama nyekundu
Maharagwe
Mbaazi
Chaza
Samaki wenye magamba magumu jamii ya Shellfish kama kaa
Mayai
Maziwa
Samaki tuna
Endapo una nguvu kidogo za kiume ufanyaje?
Endapo una tatizo la nguvu za kiume, jaribu kula mara kwa mara vyakula vinavyosemekana kuongeza nguvu za kiume vilivyoorodheshwa hapo juu. Na endapo umejaribu bila mafanikio ndani ya miezi mitatu, onana na daktari wako kwa uchunguzi zaidi kufahamu tatizo lako kisha upatiwe matibabu.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
6 Oktoba 2021 15:35:29
Rejea za mada hii:
1. Hypogonadism https://www.statpearls.com/ArticleLibrary/viewarticle/23268#. Imechukuliwa 05.03.2021
2. Plamen D Penev. Association between sleep and morning testosterone levels in older men. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/17520786/. Imechukuliwa 05.03.2021
3. Welliver Jr RC, et al. Validity of midday total testosterone levels in older men with erectile dysfunction. The Journal of urology. 2014 Jul 1;192(1):165-9. Imechukuliwa 05.03.2021
4. Bhasin S, et al. Testosterone therapy in men with androgen deficiency syndromes: an Endocrine Society clinical practice guideline. The Journal of Clinical Endocrinology & Metabolism. 2010 Jun 1;95(6):2536-59. Imechukuliwa 05.03.2021
5. Bremner WJ, et al. Loss of circadian rhythmicity in blood testosterone levels with aging in normal men. The Journal of Clinical Endocrinology & Metabolism. 1983 Jun 1;56(6):1278-81. Inapatikana https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/6841562/. Imechukuliwa 05.03.2021
6. Understanding How Testosterone Affects Men. https://www.nih.gov/news-events/nih-research-matters/understanding-how-testosterone-affects-men#. Imechukuliwa 05.03.2021