Mwandishi:
Dkt. Mangwella S, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
Jumanne, 14 Septemba 2021
Chai ya kitunguu swaumu na tangawizi
Mbali na kuongeza kinga ya mwili, kuondoa sumu mwilini, kuzuia saratani, kudhibiti sukari na shinikizo la damu na kushusha kiwango cha lehemu kwenye damu, chai ya kitunguu swaumu na tangawizi humwezesha mwanaume kufanya ngono kwa muda mrefu zaidi. Tumia mazao haya kila siku kwa afya yako.
Faida za chai ya kitunguu swaumu na tangawizi
Kuna tafiti nyingi za kuaminika zimefanyika kuchugnuza umuhimu wa kitunguu swaumu na tangawizi kwa binadamu. Tafiti hizo zimeonyesha matokeo mazuri ya viungo hivi. Faida zake baadhi zimeelezewa hapa chini;
Huondoa sumu mwilini
Kitunguu swaumu na tangawizi hufahamika kwa uwezo wake wa kuondoa sumu mwilini kwa kupunguza michomo ya kinga ya mwili. Michomo kinga ya muda mrefu (sugu) mwilini kutokana na kinga za mwili huambatana na magonjwa mbalimbali sugu kama vile magonjwa ya moyo na saratani mfano saratani ya kongosho, saratani ya tezi dume na titi)
Vitunguu swaumu na tangawizi huwa na viuaji sumu vyenye nguvu zaidi na hivyo huweza kudhibiti kuamka kwa michomo kinga.
Huongeza kinga mwilini
Chai ya kitunguu swaumu na tangawizi ina uwezo wa kupunguza michomo kinga, kuua virusi, bakeria na vimelea wengine wanaosababisha maradhi kwa kuimarisha mfumo waking ya mwili. Ili kupata faida hii, tumia mara kwa mara viungo hivi.
Hukinga chembe hai dhidi ya majeraha
Sumu ya oksijeni huweza kudhuru chembe hai na kuharibu mfumo wa kinga ya mwili wako.
Mwili huwa na mfumo wa kinga kudhibiti sumu ya oksijeni, kwa kutumia vimeng’enya kama superoxide dismutase na glutathione peroxidase. Vimeng’enya hivi hufanya kazi ya kuweka uwiano wa sumu ya oksijeni mwilini. Hata hivyo kama mfumo huu umelemewa na sumu ya oksijen husababisha kuharibiwa kwa chembe hai.
Tafiti zinaonyesha kuwa kitunguu swaumu na tangawizi husaidia kupunguza sumu ya oksijeni ikiwa pamoja na sumu kali zaidi yenye jina la malondialdehyde.
Tafiti zinaonyesha kuwa kunywa chai ya kitunguu swaumu na tangawizi kwa mwezi mmoja hupunguza kiwango cha malondialdehyde na kuongeza vimeng’enya muhimu vya kuharibu sumu ya oksijeni (superoxide dismutase na glutathione peroxidase)
Huimarisha uwezo wa kiakili
Huimarisha uwezo wa kiakili na fikra
Matumizi ya mara kwa mara ya kitunguu swaumu na tangawizi huulinda ubongo na kusaidia kuongeza uwezo wa kiakili.
Tafiti zinaonyesha, watu waliotumia viungo hivi kwa muda mrefu uwezo wao wa kiakili umakini na afya kwa ujumla ilikuwa bora zaidi ukilinganisha na kundi ambalo halikuwa linatumia viungo hivi.
Hupunguza hatari ya magonjwa ya moyo
Tafiti zinaonyesha kuwa kitunguu swaumu na tangawizi husaidia kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo kwa kupunguza shinikizo la damu, kiwango cha lehemu na kudhibiti kiwango cha sukari mwilini.
Kiwango cha lehemu mbaya, sukari na shinikizo la damu hupungua hivyo kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo na kuongeza uwezo wa mwili kudhibiti kiwango sukari kwa mgonjwa wa kisukari.
Huongeza uwezo wa mwanaume kujamiana kwa mdua mrefu zaidi
Chai ya kitunguu swaumu endapo itatumika mara kwa mara na kabla ya ngono, humwongezea mwanaume uwezo w akushiriki tendo la ndoa kwa muda mrefu na hivyo humwongezea nguvu za kiume. Ili kupata amatokeo mazuri zaidi, inashauriwa kutengeneza chai ya kitunguu swaumu kwa kutumia kijiko kimoja cha kitunguu swaumu na tangawizi kisha kunywa kabla ya kushiriki ngono.
Unapaswa kutumia pia vyakula vya kiafya haswa nafaka zisizokobolewa (kama mahindi, na karanga) masaa kadhaa kabla ya kunywa chai hii na kushiriki ngono.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
30 Juni 2023 19:22:32
Rejea za mada hii:
Shi, Xiaoming et al. “Garlic Consumption and All-Cause Mortality among Chinese Oldest-Old Individuals: A Population-Based Cohort Study.” Nutrients vol. 11,7 1504. 30 Jun. 2019, doi:10.3390/nu11071504
Khandouzi, Nafiseh et al. “The effects of ginger on fasting blood sugar, hemoglobin a1c, apolipoprotein B, apolipoprotein a-I and malondialdehyde in type 2 diabetic patients.” Iranian journal of pharmaceutical research : IJPR vol. 14,1 (2015): 131-40.
Kulkarni RA, et al. Anti-inflammatory and antioxidant effect of ginger in tuberculosis. J Complement Integr Med. 2016 Jun 1;13(2):201-6. doi: 10.1515/jcim-2015-0032. PMID: 27089418.
7 Impressive Benefits of Combining Garlic and Ginger. https://www.healthline.com/nutrition/garlic-and-ginger-benefits. Imechukuliwa 14/09/2021
Tasnim, Sara et al. “Allium sativum L. Improves Visual Memory and Attention in Healthy Human Volunteers.” Evidence-based complementary and alternative medicine : eCAM vol. 2015 (2015): 103416. doi:10.1155/2015/103416
Iranshahy, et al. “Diet therapy for the treatment of Alzheimer's disease in view of traditional Persian medicine: A review.” Iranian journal of basic medical sciences vol. 22,10 (2019): 1102-1117. doi:10.22038/ijbms.2019.36505.8694
Chen, Linlin et al. “Inflammatory responses and inflammation-associated diseases in organs.” Oncotarget vol. 9,6 7204-7218. 14 Dec. 2017, doi:10.18632/oncotarget.23208
Mirzavandi F, etal. Effects of garlic supplementation on serum inflammatory markers: A systematic review and meta-analysis of randomized controlled trials. Diabetes Metab Syndr. 2020 Sep-Oct;14(5):1153-1161. doi: 10.1016/j.dsx.2020.06.031. Epub 2020 Jun 19. PMID: 32673835.
Kwak, Jin Sook et al. “Garlic powder intake and cardiovascular risk factors: a meta-analysis of randomized controlled clinical trials.” Nutrition research and practice vol. 8,6 (2014): 644-54. doi:10.4162/nrp.2014.8.6.644
Carvalho, et al. “Effectiveness of ginger in reducing metabolic levels in people with diabetes: a randomized clinical trial.” Revista latino-americana de enfermagem vol. 28 e3369. 9 Oct. 2020, doi:10.1590/1518-8345.3870.3369
Karna, Prasanthi et al. “Benefits of whole ginger extract in prostate cancer.” The British journal of nutrition vol. 107,4 (2012): 473-84. doi:10.1017/S0007114511003308
Zhao, Lihan et al. “Efficacy based ginger fingerprinting reveals potential antiproliferative analytes for triple negative breast cancer.” Scientific reports vol. 10,1 19182. 5 Nov. 2020, doi:10.1038/s41598-020-75707-0