top of page

Mwandishi:

Dkt. Mangwella S, MD

Mhariri:

Dkt. Benjamin L, MD

Jumatano, 15 Septemba 2021

Chai ya ndizi mbivu

Chai ya ndizi mbivu

Kwa kula ndizi mbivu utapata virutubisho kama vitamin B6, potassium, magnesium, manganese na shaba. Hata hivyo chai ya ndizi mbivu na maganda yake huwa na vitamin B6, potassium na tryptophan kwa wingi kiasi cha kuweza kukupa usingizi, kuthibiti shinikizo la damu na kuondoa sumu mwilini.


Chai ya ndizi


Chai ya ndizi hutengenezwa kwa kuchemsha vipande vya ndizi iliyosafishwa vema kwenye maji kisha kuvitoa na kunywa maji yake. Chai hii inaweza tengenezwa kwa kutumia ndizi iliyomenywa au isiyomenywa. Chai ya ndizi isiyomenywa huhitaji muda mrefu kupikwa kutokana na kuwa na nyuzinyuzi nyingi, hata hivyo huwa na virutubisho vingi zaidi haswa vitamin B6 na potassium. Unaweza tia mdalasini au asali ili kuongeza radha, lakini pia unaweza kunywa bila kuweka viungo hivyo.


Kwa ujumla chai ya ndizi huwa na baadhi ya virutubisho vifuatavyo;

  • Vitamin B6

  • Potassium

  • Magnesium

  • Manganese

  • Copper

  • Nishati kidogo


Virutubisho ambavyo hupotea kwa kutengeneza chai ya ndizi ni Vitamin C. Kwa kutumia cha ya ndizi unapata faida zifuatazo;


  • Kuondoa sumu mwilini

  • Huondoa gesi tumboni

  • Huimarisha usingizi

  • Huimarisha afya kwa ujumla


Huondoa sumu mwilini


Kutokana na kuwa na na viuaji sumu asilia kama dopamine na gallocatechin vinavyoondoa sumu mwilini, kunywa chai ya ndizi huweza kukukinga na magonjwa sugu kama vie maradhi ya moyo na mishipa ya damu. Ili kupata faida zaidi, kunywa chai ya ndizi yenye maganda yake.


Kupunguza hatari ya kupata magonjwa sugu


Madini potassium na magnesium yameonekana kwenye tafiti mbalimbali kupunguza kwa asilimia 27 zaidi hatari ya kupata shinikizo la damu, magonjwa ya moyo na mishipa ya damu kama vile kiharusi. Ili kufata zaidi hizi, utapaswa kutumia mara kwa mara chai hii.


Huimarisha usingizi


Chai ya ndizi ina virutubisho vya potassium, magnesium na tryptophan kwa wingi ambavuo hufanya kazi nzuri yakukupa usingizi haraka na wa muda mrefu. Hufanya kazi hiyo kwa kulegeza misuli, kuongeza uzalishaji wa homon melatonin, ni homon muhimu ya usingizi.


Huondoa gesi tumboni


Kwa kuwa ina madini potassium kwa wingi yanayosaidia kurekebisha uwiano wa maji, shinikizo la damu na madini mwilini, kutumia chai ya ndizi huondoa tatizo la gesi tumboni kutokana na kupotea kwa uwiano wa chumvi na maji. Hufanya hivi kwa kuongeza utolewaji wa madini chumvi kupitia mkojo.


Hatua za kuandaa chai ya ndizi isiyo na maganda

  • Weka maji vikombe viwili hadi vitatu kwenye sufuria ya kuchemshia chai kisha yachemshe

  • Menya ndizi yako kisha ondoa vipande vya mwishoni

  • Weka ndizi kwenye maji yanayochemka

  • Punguza moto kisha acha ichemke kwa muda wa dakika 5 hadi 10

  • Ongeza mdalasini na asali (kama utapenda)

  • Ondoa ndizi kisha weka chai yako kwenye kikombe tayari kwa kunywa kunywa(unaweza hifadhi chai iliyobaki kwenye chupa ila isikae zaidi ya masaa 24)


Hatua za kuandaa chai ya ndizi yenye maganda

  • Weka maji vikombe viwili hadi vitatu kwenye sufuria ya kuchemshia chai kisha ya chemshe

  • Safisha ndizi yako kwenye maji safi yanayotiririka kuondoa uchafu wote na kemikali zisizotakiwa

  • Ondoaa miishio yake kisha kata iwe kwenye vipande viwili

  • Weka vipande hivyo kwenye maji yanayochemka

  • Punguza moto ili ichemke na moto mdogo kwa muda wa dakika 15 hadi 20 6. Ongeza mdalasini na asali kama utapenda

  • Ondoa ndizi kwenye chai yako kisha weka chai yako kwenye kikombe na kuinywa (unaweza kuhifadhi chai iliyobaki kwenye chupa ila isikae zaidi ya masaa 24)

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

6 Oktoba 2021, 15:37:13

Rejea za mada hii:

Food Data Central. https://fdc.nal.usda.gov/fdc-app.html#/food-details/173944/nutrients. Imechukuliwa 15/09/2021

Cao Y, et al. Magnesium Intake and Sleep Disorder Symptoms: Findings from the Jiangsu Nutrition Study of Chinese Adults at Five-Year Follow-Up. Nutrients. 2018 Sep 21;10(10):1354. doi: 10.3390/nu10101354. PMID: 30248967; PMCID: PMC6212970.

Heizhati M, et al. Decreased serum potassium may disturb sleep homeostasis in essential hypertensives. Hypertens Res. 2019 Feb;42(2):174-181. doi: 10.1038/s41440-018-0131-4. Epub 2018 Nov 16. PMID: 30446708; PMCID: PMC8075976.

Maggini S, et al. Selected vitamins and trace elements support immune function by strengthening epithelial barriers and cellular and humoral immune responses. Br J Nutr. 2007 Oct;98 Suppl 1:S29-35. doi: 10.1017/S0007114507832971. PMID: 17922955.

Mary J. Brown, et al. Vitamin B6 Deficiency. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK470579/. Imechukuliwa 15/09/2021

Nieman DC, et al. Bananas as an energy source during exercise: a metabolomics approach. PLoS One. 2012;7(5):e37479. doi: 10.1371/journal.pone.0037479. Epub 2012 May 17. PMID: 22616015; PMCID: PMC3355124.

Wang X, et al. Flavonoid intake and risk of CVD: a systematic review and meta-analysis of prospective cohort studies. Br J Nutr. 2014 Jan 14;111(1):1-11. doi: 10.1017/S000711451300278X. Epub 2013 Aug 16. PMID: 23953879.

Shinichi Someya, et al. Antioxidant compounds from bananas (Musa Cavendish). https://www.sciencedirect.com/science/article/abs/pii/S0308814602001863. Imechukuliwa 15/09/2021

Lee S, et al. Effect of different cooking methods on the content of vitamins and true retention in selected vegetables. Food Sci Biotechnol. 2017 Dec 12;27(2):333-342. doi: 10.1007/s10068-017-0281-1. PMID: 30263756; PMCID: PMC6049644.

Iain Campbell MD FRCA. Physiology of fluid balance. https://www.sciencedirect.com/science/article/abs/pii/S1472029909002215. Imechukuliwa 15/09/2021

Rabinowitz L, et al. The central nervous system in potassium homeostasis. Front Neuroendocrinol. 1993 Jan;14(1):1-26. doi: 10.1006/frne.1993.1001. PMID: 8477870.

Abbasi B, et al. The effect of magnesium supplementation on primary insomnia in elderly: A double-blind placebo-controlled clinical trial. J Res Med Sci. 2012 Dec;17(12):1161-9. PMID: 23853635; PMCID: PMC3703169.

Clausen T. Na+-K+ pump regulation and skeletal muscle contractility. Physiol Rev. 2003 Oct;83(4):1269-324. doi: 10.1152/physrev.00011.2003. PMID: 14506306.

Fukushige H, et al. Effects of tryptophan-rich breakfast and light exposure during the daytime on melatonin secretion at night. J Physiol Anthropol. 2014 Nov 19;33(1):33. doi: 10.1186/1880-6805-33-33. PMID: 25407790; PMCID: PMC4247643.

Bravo R, et al. Tryptophan-enriched cereal intake improves nocturnal sleep, melatonin, serotonin, and total antioxidant capacity levels and mood in elderly humans. Age (Dordr). 2013 Aug;35(4):1277-85. doi: 10.1007/s11357-012-9419-5. Epub 2012 May 24. PMID: 22622709; PMCID: PMC3705114.

Malik VS, et al. Sugar-sweetened beverages, obesity, type 2 diabetes mellitus, and cardiovascular disease risk. Circulation. 2010 Mar 23;121(11):1356-64. doi: 10.1161/CIRCULATIONAHA.109.876185. PMID: 20308626; PMCID: PMC2862465.

Kokubo Y, et al. Dietary magnesium intake and risk of incident coronary heart disease in men: A prospective cohort study. Clin Nutr. 2018 Oct;37(5):1602-1608. doi: 10.1016/j.clnu.2017.08.006. Epub 2017 Aug 12. PMID: 28843443.

Aburto NJ, et al. Effect of increased potassium intake on cardiovascular risk factors and disease: systematic review and meta-analyses. BMJ. 2013 Apr 3;346:f1378. doi: 10.1136/bmj.f1378. PMID: 23558164; PMCID: PMC4816263.

Newberry SJ, et al. Effects on Chronic Disease Outcomes and Risks [Internet]. Rockville (MD): Agency for Healthcare Research and Quality (US); 2018 Jun. Report No.: 18-EHC009-EF. PMID: 30125063.

Seth A, et al. Potassium intake and risk of stroke in women with hypertension and nonhypertension in the Women's Health Initiative. Stroke. 2014 Oct;45(10):2874-80. doi: 10.1161/STROKEAHA.114.006046. Epub 2014 Sep 4. PMID: 25190445; PMCID: PMC4175295.

bottom of page