Mwandishi:
Dkt. Eligius L, MD, MMed, PhD, FTAAS, FCPath
Mhariri:
Dkt. Mangwella S, MD
Ijumaa, 8 Oktoba 2021
Chanjo za UVIKO-19
Mwili una uwezo asili wa kutengeneza kinga dhidi ya vimelea wa maradhi inayomlinda mtu baada ya maambukizi ya awali. Kwa kuwa kinga asili dhidi ya kirusi cha COVID-19 hudumu kwa muda mfupi, unashauriwa kupata chanjo ili kuuwezesha mwili wako kutengeneza kinga ya muda mrefu itakayokuepusha na ugonjwa mkali wa UVIKO-19. Makala hii imeandikwa katika vipengele vifuatavyo;
Mlipuko wa UVIKO-19
Umbile la SARS-CoV-2
Sehemu za chanjo
Utengenezaji wa chanjo
Chanjo dhidi ya UVIKO-19
Utengenezaji wa haraka wa chanjo dhidi ya UVIKO-19
Ukweli kuhusu chanjo dhidi ya UVIKO-19
Changamoto kuhusu utengenezaji wa chanjo dhidi ya UVIKO-19
Kusoma kuhusu historia ya chanjo ya kwanza dhidi ya mlipuko wa ndui miaka ya 1790 bofya hapa
Mlipuko wa UVIKO-19
Wagonjwa wa mwanzo wenye UVIKO-19 walianza kuonekana tarehe 17.11.2019 mji wa Wuhan, jimbo la Hubei huko China
31.12.2019 taarifa rasmi iliripotiwa ofisi ya Shirika la Afya Duniani (WHO) huko China
30.01.2020 - Shirika la Afya duniani ilitangaza kuwa UVIKO-19 ni Dharura ya Afya ya Jamii ya Hatari Kimataifa
11.02.2020 – Kirusi kisababishacho UVIKO-19 kiliitwa aina ya pili ya virusi vya korona vinavyosababisha homa kali ya mapafu (SARS-CoV-2)
11.03.2020 - UVIKO-19 ulitangazwakuwajanga la dunia
Umbile la kirusi cha SARS-CoV-2
Gamba la nje
Protini
S, protini inayochomoza
M, protini ya utando
E, protini ya gamba
N, protini ya ndani
Kinasaba:
+ssRNA
Ukubwa wa watatizo
Takwimu za dunia: Hadi tarehe13 Septemba 2021
Watu 224,511,226 wamethibitishwa kuwa na maambukizi ya virusi vya korona
Afrika = 5,820,211
Tanzania = 1,367
Watu 4,627,540 wamefariki kwa UVIKO
Afrika = 140,247
Tanzania = 50
Sehemu za chanjo
Antigeni ya chanjo
Virusi vilivyoondolewa makali
Virusi vilivyouawa
Protini za virusi
Vekta za virusi (virusi vibebaji)
Vinasaba (RNA na DNA)
Viungo vya kuifanya chanjo iwe salama na yenye ufanisi
Kihifadhi
Kiimarishaji
Ute
Kisaidizi
Hatua za kutengeneza chanjo za UVIKO-19
Hatua ya uchuhguzi
Kubainisha sehemu ya kirusi inayofaa kuchochea utengenezaji wa kinga
Majaribio ya awali
Majaribio kutumia wanyama ili kutathmini usalama na ufanisi wa chanjo katika kutoa kinga dhidi ya ugonjwa
Majaribio kwa binadamu
Majaribio awamu za I-III
Uchambuzi na kupitishwa na mamlaka za udhibiti
Kutengeneza chanjo kiwandani kwa kuzingatia kanuni stahiki za uzalishaji chini ya usimamizi mkubwa wa ubora
Aina za Chanjo za UVIKO-19
Kuna aina mbalimbali za chanjo zinazotokana na nini kilichotumika kutengeneza chanjo, aina hizo ni kama vile;
Chanjo inayotoka kwenye virusi vya korona vilivyopunguzwa makali
Chanjo inayotoka kwenye virusi vya korona vilivyouawa
Chanjo inayotoka na protini za kirusi cha korona
Chanjo kutoka kwenye vekta za virusi
Chanjo Kutoka kwenye vinasaba (RNA na DNA) ya kirusi
Chanjo kutoka kwenye virusi vilivyopunguzwa makali
Virusi hivi vinapoingia mwilini huzaliana pasipo kuleta madhara makubwa kama kirusi halisi.
Faida zake
Teknolojia ya kuvidhoofisha ipo
Inawezesha utengenezaji wa kinga ya mwili ya antibodi na pia kinga iletwayo na chembe hai
Ubaya wake
Kwa nadra virusi vinaweza kugeuka na kusababisha ugonjwa
Siyo chanjo nzuri kwa watu wenye udhaifu wa kinga ya mwili
Inahitaji kuhifadhiwa katika jokofu la nyuzijoto za chini
Aina ya chanjo ya UVIKO kwenye kundi hili
Hakuna iliyoidhinishwa mpaka sasa
Virusi vilivyouawa
Virusi vinaondolewa uhai wake kwa kuondoa vinasba. Haviwezi kuzaliana lakini vinaweza kuchochea utengenezaji wa kinga ya mwili
Faida zake
Teknolojia ya kuviua ipo, Ni rahisi kutengeneza
Haiwezi kusababisha ugonjwa
Inaweza kutumika kwa watu wenye udhaifu wa kinga ya mwili
Haihitaji kuhifadhiwa katika jokofu la nyuzijoto za chini
Ubaya wake
Inahitaji kurudiwa ili iweze kutoa kinga ya kutosha
Aina ya chanjo hii ya UVIKO-19 kwenye kundi hili
Sinovac
Sinopharm
Chanjo za vekta za virusi
Hutumia virusi salama ambavyo haviwezi kusababisha magonjwa
Virusi hutumika kubeba sehemu ya kinasaba iliyo na msimbo (code) wa kijenetiki wa kutengenezea protini za kirusi cha UVIKO
Inapotumika huagiza chembe hai za aliyechanjwa kutengeneza protini husika na hizi huchochea utengenezaji wa kinga
Faida zake
Teknolojia ya kutengeneza ipo
Inawezesha utengenezaji wa kinga ya mwili ya antibodi na pia kinga iletwayo na chembe hai
Ubaya wake
Maambukizi ya nyuma ya aina hiyo ya vekta inaweza kupunguza uwezo wake wa kuchochea utengenezaji wa kinga
Ni ngumu kutengeneza
Aina ya chanjo hii ya UVIKO-19 katika kundi hili
AstraZeneca
Johnson and Johnson
Sputnic V
Chanjo za protini za virusi
Hizi hutumia vipande vya protini visivyo na madhara au ganda la protini ambalo hufanana na virusi vya UVIKO-19 ili kutoa kinga ya mwili.
Faida zake
Inafaa kwa watu wenye udhaifu wa kinga ya mwili
Haina chembe hai ya virusi vya UVIKO hivyo haiwezi kusababisha madhara
Haihitaji kuhifadhiwa katika jokofu la nyuzijoto za chini
Ubaya wake
Ni ngumu kutengeneza kwa uasabu utambuzi wa aina ya protini ya kutumia ni mgumu na huchukua muda mrefu
Inahitaji kisaidizi kuongezewa nguvu ya kuchochea utengenezaji wa kinga na pia inahitaji kurudiwa ili kinga ya kutosha itengenezwe
Aina ya chanjo hii ya UVIKO-19 kwenye kundi hili
Novovax
Chanjo za vinasaba za virusi
Hutumia vinasaba vya kirusi cha UVIKO (DNA or RNA ) ili kuchochea utengenezaji wa kinga. Kinasaba kinapoingizwa mwilini kinaelekeza chembe hai za mwili kutengeneza protini husika za virusi vya korona zinazochochea mfumo wa kinga kutengeneza kinga dhidi ya kirusi.
Faida zake
Haina chembe hai ya virusi vya UVIKO hivyo haiwezi kusababisha madhara
Teknolojia ya kutengeneza ipo
Inawezesha utengenezaji wa kinga ya mwili ya antibodi na pia kinga iletwayo na chembe hai
Ubaya wake
Inahitaji kuhifadhiwa katika jokofu la nyuzijoto za chini
Inahitaji marudio ili kinga ya kutosha iweze kutengenezwa
Aina ya chanjo hii ya UVIKO-19 katika kundi hili
Pfizer-BioNTech
Moderna
Chanjo za UVIKO hadi 24.09.2021
Hadi sasa, kuna chanjo kadhaa ambazo ziko kwenye hatua mbalimbali za uvumbuzi ikiwa ni pamoja na:
185 kwenye utafiti wa mwanzo (pre-clinical phase)
117 kwenye majaribio kwa binadamu (clinical phase)
Chanjo 7 zimeidninishwa na Shirika la Afya duniani na zikawekwa kwenye mpango wa COVAX
Chanjo zilizopendekezwaTanzania ni Pfizer BionTech; Moderna; Johnson & Johnson/ Jansen; Sinovac; Sinopharm
Chanjo zilizoidhinishwa kwa matumizi huko Marekani ya Kaskazini (USA) ni Pfizer BionTech; Moderna; Johnson & Johnson/Jansen
Chanjo za UVIKO zilizoorodheshwa na WHO kwa matumizi ya dharura
Chanjo dhidi ya UVIKO zilizopendekezwa na Wizara ya Afya kwa matumizi nchini Tanzania
Utoaji wa chanjo za UVIKO hadi sasa
Dozi za chanjo ya UVIKO zilizotolewa hadi 13.09.2021
Dozi 5,534,977,637 zimetolewa
1.07 billion (13.7% ya watu duniani) wamepata chanjo kamili dhidi ya UVIKO-19
Utengenezaji wa haraka wa Chanjo dhidi ya UVIKO-19
Kuwepo kwa taarifa za tafiti za utengenezaji wa chanjo dhidi ya SARS and MERS zimerahisisha kufupishwa sana kwa hatua ya uchunguzi wa chanjo ya UVIKO-19. Maendeleo ya teknolojia kwa sasa pia yamesaidia kuwapa wanasayansi uwezo mkubwa na ubunifu katika utengenezaji wa chanjo na kufupishwa kwa baadhi ya hatua za majaribio kwa binadamu ili kupambana na dharura ya janga hili duniani.
Ukweli kuhusu chanjo dhidi ya UVIKO-19
Ni salama na zenye ufanisi
Zina uwezo wa kuzuia au kupunguza vifo na kulazwa hospitalini
Zina uwezo dhidi ya baadhi ya anuwai za korona ikiwa ni pamoja na kirusi aina ya Delta
Zinapunguza hatari ya kueneza maambukizi ya SARS-CoV-2
Chanjo dhidi ya UVIKO-19:
HAZINA chipu za kufuatilia watu
HAZISABABISHI waliochanjwa kuwa na dalili za smaku mwilini
HAZISABABISHI matatizo ya uzazi (ugumba na kupoteza nguvu za kiume) kwa waliochanjwa
HAZIBADILISHI vinasaba vya mtu aliyechanjwa
Changamoto za chanjo dhidi ya UVIKO-19
Maadili
Usambazaji unaweza usizingatie haki za baadhi ya wahitaji.
Ufanisi wa chanjo
Uwe wa kiasi gani?
Ufanisi kwa wazee na watoto
Utengenezaji na usambazaji hautoshelezi mahitaji
Ufanisi kupungua kwa baadhi ya anuwai
Wapotoshaji ni tishio kwa matumizi ya chanjo dhidi ya UVIKO-19
Baadhi ya watu wana uelewa usio sahihi kuhusu chanjo za UVIKO19
Baadhi ya watu kukosa mwelekeo bayana na chanya
Baadhi ya watu kusambaza taarifa za kuogopesha
Baadhi ya watu wanaamini nadharia-njama
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
8 Oktoba 2021 18:45:15
Rejea za mada hii:
1. WHO Coronavirus Disease (COVID-19) Dashboard [Internet]. WHO (World Heal. Organ. 2021. Available from: https://covid19.who.int/. Cited 3 Jan 2021.
2. Kashte, S, et al. COVID-19 vaccines: rapid development, implications, challenges and future prospects. Human Cell 34, 711–733 (2021). https://doi.org/10.1007/s13577-021-00512-4
3. FDA Takes Key Action in Fight Against COVID-19 By Issuing Emergency Use Authorization for First COVID-19 Vaccine [Internet]. FDA. 2020. Available from: https://www.fda.gov/news-events/press-announcements/fda-takes-key-action-fight-against-covid-19-issuing-emergency-use-authorization-first-covid-19.
4. WHO issues its first emergency use validation for a COVID-19 vaccine and emphasizes need for equitable global access [Internet]. World Health Organ. Available from: www.who.int/news/item/31–12–2020-who-issues-its-first-emergency-use-validation-for-a-covid-19-vaccine-and-emphasizes-need-for-equitable-global-access.