Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Helen L, M.D
Jumapili, 7 Februari 2021
Dawa na virutubisho vinavyotibu COVID-19
Tafiti zinaonyesha, dawa azithromycin, madini ya zinc, vitamini C na D na dexamethasone huwa na uwezo wa kukukinga na kutibu magonjwa ya mfumo wa upumuaji kama COVID-19 . Unashauriwa kupata vitamini C na D na madini ya zinc kutoka kwenye vyakula, endapo unahitaji dawa wasiliana na daktari wako.
Mahusiano ya COVID-19 na mfumo wa kinga mwilini
Kwa maelezo rahisi, kirusi cha COVID-19 kinapoingia mwilini huamsha mfumo wa kinga ya mwili. Kwa sababu kirusi huyu hudhuru mfumo wa upumuaji, mwitikio wa kinga ya mwili hutokea sana kwenye mfumo wa upumuaji. Mwitikio wa kinga ya mwili kwenye mapafu husababisha kuonekana kwa dalili kuu tano ambazo ni kutanuka kwa mishipa ya damu, kuongezeka kwa joto, kuvimba tishu za mapafu, maumivu ya kifua, mapafu kupoteza uwezo wa kufanya kazi. Dalili hizi hutokea kwenye kila aina ya maambukizi au majeraha yanayotokea nje au ndani ya mwili, na huashiria kuwa mfumo wa kinga mwilini unafanya kazi yake vema. Dalili zinazoweza kuambatana na mwitikio huu ni kama vile;
Homa na mwili kutetemeka
Kikohozi kikavu
Kuishiwa au pumzi na kupumua kwa shida
Uchovu wa mwili
Maumivu ya misuli au mwili
Koo kukauka
Kuchuruzika kwa kamasi
Kichefuchefu na kutapika
Kuharisha
Kirusi cha SARS-CoV-2 anayesababisha COVID-19, husababisha mwitikio mkubwa wa kinga ya mwili na hivyo huleta dalili kali zaidi za COVID-19 . Endapo mwitikio huu hauna mwisho, hupelekea kusinyaa kwa mapafu na hivyo kupoteza uwezo wa kupumua au kifo. Matumizi ya dawa zinazopambana na mwitikio wa mfumo wa kinga mwilini hupunguza kuonekana kwa dalili hizi na hivyo kufanya kazi nzuri katika matibabu.
Azithromycin
Tafiti zinaonyesha kwamba, dawa ya azithromycine (AZUMA) ina uwezo mkubwa wa kukabiliana na kirusi, ufanyaji kazi wa dawa hii kupambana na virusi ni wa namna hii;
Kwanza, huzuia kuamka kwa mfumo wa ulinzi wa mwili
Pili, hupunguza kiwango cha virusi kuingia ndani ya chembe hai
Tatu, huimarisha mwitikio wa mfumo wa kinga mwilini dhidi ya virusi vinavyo sababisha COVID-19
Nne, huongezea uwezo kinga ya mwili kutambua maambukizi ya virusi vinavyo sababisha COVID-19
Tano, kutibu maambukizi ya bakteria yanayoambatana na maambukizi ya virusi vinavyo sababisha COVID-19
Kwa kufanya mambo hayo matano hupelekea kuficha au kupunguza dalili za COVID-19. Dawa ya AZUMA ina uwezo wa kutumika kwenye matibabu ya virusi wengine pia kama Ebola, Zika, respiratory syncytial virus, influenzae H1N1 virus, enterovirus, and rhinovirus. Dawa ya Azithromycin ina uwezo wa kufanya kazi peke yake kutibu kirusi cha COVID-19 aina ya SARS-CoV-2
Madini ya zinc
Zinc ni madini muhimu katika mfumo wa kinga mwilini, madini haya hufanya kazi ya kuimarisha mfumo wa kinga, hupunguza muda wa kuugua na huzuia uzalianaji wa virusi jamii ya RNA. Madini ya zinc pia hufanya kazi ya;
Kuzuia utengenezaji wa vinasaba vya kirusi
Kuua seli za virusi
Kuongeza uondoaji wa chembe zilizokufa mwilini
Matumizi ya madini ya zinc huzuia kwa asilimia kubwa kupata maambukizi ya virusi kwenye mfumo wa hewa kama vile virusi vya homa baridi na virusi vya rhinovirus.
Tafiti bado zinaendelea kufuatilia endapo zinc inaweza kutumika pamoja na dawa ya hydroxychloroquine kama kinga na tiba ya COVID-19. Inashauriwa kupata zinc kutoka kwenye chakula kiasi kinachofikia miligramu 11 kila siku kwa wanaume na miligramu 8 kwa wanawake wasio wajawazio
Unaweza kupata kiwango kizuri cha madini ya zinc kutoka kwenye vyakula aina fulani unavyokula. Endapo una upungufu wa madini haya unashauriwa kutumia vidonge vya zinc. Wasiliana na datari wako kabla ya kutumia vidonge vya zinc.
Soma zaidi kuhusu vyakula vyenye Madini ya zinc kwa wingi kwenye makala zingine ndani ya tovuti ya ULY CLINIC
Vitamini C
Vitamini C kwa jina jingine hufahamika kama ascorbic acid, ni aina ya vitamini ambayo ina msaada mkubwa kwenye matibabu ya wagonjwa wa COVID-19 walio katika hali mbaya. Vitamini C hii hufanya kazi kama;
Kiua sumu ndani ya mwili
Kihuisho cha mfumo wa kinga mwilini
Kiimarishi cha kuta za mishipa ya damu
Watu walio na msongo mwilini kwa sababu ya ugonjwa mkali pamoja na kusambaa kwa maambukizi kwenye damu, huhitaji kutumia vitamini C ili kuimarisha mfumo wa kinga. Kwa wagonjwa ambao hawana ugonjwa mkali, unashauriwa kutumia vitamini C kutoka kwenye vyakula.
Vitamini D
Vitamini D hufanya kazi ya kuimarisha aina mbili za mfumo wa kinga mwilini yaani aina ya ‘innate immunity ’ na ‘adaptive immunity’. Vitamini D inaonekana kwenye tafiti nyingi kuwa ni kinga ya maambukizi ya mfumo wa hewa. Licha ya kuwa na umuhimu wa kukinga dhidi ya magonjwa ya mfumo wa upumuaji, bado tafiti nyingi zinaendelea kufanyika kuangalia umuhimu wa vitamini D kutumika kama kinga au tiba ya COVID-19.
Makundi ya watu wafuatao wapo hatarini kuwa na upungufu wa vitamini D na hivyo kuongeza hatari nyingine ya kupata maambukizi makali ya ugonjwa wa COVID-19
Mgonjwa wa presha ya juu
Mgonjwa wa obeziti
Wazee
Wagonjwa hawa wanapaswa kupata kiwango kizuri cha Vitaminl D kutoka kwenye chakula au vidonge. Watu wenye vihatarishi vilivyoorodheshwa hapo juu, wanapaswa kupata Vitamini D ya ziada . Kwa watu wengine ambao hawana kihatarishi wanapaswa kupata Vitamini D kwa kutoka kwenye vyakula. Wasiliana na daktari wako kwa ushauri zaidi.
Soma zaidi kuhusu vyakula vyenye vitamin C na D kwa wingi kwenye makala zingine ndani ya tovuti ya ULY CLINIC
Dawa ya dexamethasone
Dawa ya dexamethasone ni dawa iliyo kwenye kundi la dawa linaloitwa 'corticosteroid'. Dawa hizi hufanya kazi ya kupunguza mwitikio wa kinga ya mwili dhidi ya maambukizi. Kupunguza mwitikio wa kinga ya mwili husababisha kutotolewa kwa chembe za mwili za kutosha hivyo kupunguza pia dalili za ugonjwa wa COVID-19.
Dawa ya dexamethasone inashauriwa kutumika kwa wagonjwa wa COVID-19 ambao wana ugonjwa mkali na wanapumulia mashine ya oxygen. Hata hivyo matumizi ya dawa hizi huchelewesha mfumo wa kinga ya mwili kupambana na maradhi na kuongeza hatari ya kupata maambukizi ya bakteria na kuongeza hatari ya kifo. Kumbuka: Usitumie dawa yoyote ile kabla ya kuwasiliana na daktari wako.
ULY CLINIC inakukumbusha utumie virutubisho na madini kutoka kwenye chakula zaidi kutoka kwenye dawa.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
19 Julai 2023 20:41:55
Rejea za mada hii:
1.Wei XB, Wang ZH, et al. Efficacy of vitamin C in patients with sepsis: an updated meta-analysis. Eur J Pharmacol. 2020;868:172889. Inapatikana kwenye linki hii: https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/31870831. Imechukuliwa 06.02.2021
2.Fisher BJ, et al. Ascorbic acid attenuates lipopolysaccharide-induced acute lung injury. Crit Care Med. 2011;39(6):1454-1460. Inapatikana kwenye linki hii: https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/21358394.. Imechukuliwa 06.02.2021
3.Fowler AA, 3rd, Syed AA, Knowlson S, et al. Phase I safety trial of intravenous ascorbic acid in patients with severe sepsis. J Transl Med. 2014;12:32. Inapatikana kwenye linki hii: https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/24484547. Imechukuliwa 06.02.2021
4.Fowler AA, 3rd, et al. Effect of vitamin C infusion on organ failure and biomarkers of inflammation and vascular injury in patients with sepsis and severe acute respiratory failure: the CITRIS-ALI randomized clinical trial. JAMA. 2019;322(13):1261-1270. Inapatikana kwenye linki hii: https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/31573637. Imechukuliwa 06.02.2021
5.Fowler AA, 3rd, et al. Vitamin C for sepsis and acute respiratory failure–reply. JAMA. 2020;323(8):792-793. Inapatikana kwenye linki hii: https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/32096845. Imechukuliwa 06.02.2021
6.Marik PE, Khangoora V, et al. Hydrocortisone, vitamin C, and thiamine for the treatment of severe sepsis and septic shock: a retrospective before-after study. Chest. 2017;151(6):1229-1238. Inapatikana kwenye linki hii: https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/27940189. Imechukuliwa 06.02.2021
7.Kim WY, et al. Combined vitamin C, hydrocortisone, and thiamine therapy for patients with severe pneumonia who were admitted to the intensive care unit: propensity score-based analysis of a before-after cohort study. J Crit Care. 2018;47:211-218. Inapatikana kwenye linki hii: https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/30029205. Imechukuliwa 06.02.2021
8.Fujii T, Luethi N, et al. Effect of vitamin C, hydrocortisone, and thiamine vs hydrocortisone alone on time alive and free of vasopressor support among patients with septic shock: the VITAMINS randomized clinical trial. JAMA. 2020;323(5):423-431. Inapatikana kwenye linki hii: https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/31950979. Imechukuliwa 06.02.2021
9.Chang P, Liao Y, et al. Combined treatment with hydrocortisone, vitamin c, and thiamine for sepsis and septic shock: a randomized controlled trial. Chest. 2020;158(1):174-182. Inapatikana kwenye linki hii: https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/32243943. Imechukuliwa 06.02.2021
10.Iglesias J, et al. Outcomes of metabolic resuscitation using ascorbic acid, thiamine, and glucocorticoids in the early treatment of sepsis: the ORANGES trial. Chest. 2020;158(1):164-173. Inapatikana kwenye linki hii: https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/32194058. Imechukuliwa 06.02.2021
11.te Velthuis AJ, et al. Zn(2+) inhibits COVID-19 virus and arterivirus RNA polymerase activity in vitro and zinc ionophores block the replication of these viruses in cell culture. PLoS Pathog. 2010;6(11):e1001176. Inapatikana kwenye linki hii: https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/21079686. Imechukuliwa 06.02.2021
12.Xue J, Moyer A, et al. Chloroquine is a zinc ionophore. PLoS One. 2014;9(10):e109180. Inapatikana kwenye linki hii: https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/25271834. Imechukuliwa 06.02.2021
13.Calder PC, Carr AC, et al. Optimal nutritional status for a well-functioning immune system is an important factor to protect against viral infections. Nutrients. 2020;12(4). Inapatikana kwenye linki hii: https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/32340216. Imechukuliwa 06.02.2021
14.Hambridge K. The management of lipohypertrophy in diabetes care. Br J Nurs. 2007;16(9):520-524. Inapatikana kwenye linki hii: https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/17551441. Imechukuliwa 06.02.2021
15.National Institutes of Health. Office of Dietary Supplements. Zinc fact sheet for health professionals. 2020. Inapatikana kwenye linki hii: https://ods.od.nih.gov/factsheets/Zinc-HealthProfessional/. Imechukuliwa 06.02.2021
16.Myint ZW, Oo TH, et al. Copper deficiency anemia: review article. Ann Hematol. 2018;97(9):1527-1534. Inapatikana kwenye linki hii: https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/29959467. Imechukuliwa 06.02.2021
17.Kumar N. Copper deficiency myelopathy (human swayback). Mayo Clin Proc. 2006;81(10):1371-1384. Inapatikana kwenye linki hii: https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/17036563. Imechukuliwa 06.02.2021
18.Hoffman HN, 2nd, Phyliky RL, Fleming CR. Zinc-induced copper deficiency. Gastroenterology. 1988;94(2):508-512. Inapatikana kwenye linki hii: https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/3335323. Imechukuliwa 06.02.2021
19.Carlucci P, Ahuja T, et al. Hydroxychloroquine and azithromycin plus zinc vs hydroxychloroquine and azithromycin alone: outcomes in hospitalized COVID-19 patients. medRxiv. 2020;Preprint. Inapatikana kwenye linki hii: https://www.medrxiv.org/content/10.1101/2020.05.02.20080036v1. Imechukuliwa 06.02.2021
20.Aranow C. Vitamin D and the immune system. J Investig Med. 2011;59(6):881-886. Inapatikana kwenye linki hii: https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/21527855. Imechukuliwa 06.02.2021
21.Forrest KY, et al. Prevalence and correlates of vitamin D deficiency in US adults. Nutr Res. 2011;31(1):48-54. Inapatikana kwenye linki hii: https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/21310306. Imechukuliwa 06.02.2021
22.Lu D, Zhang J, et al. Link between community-acquired pneumonia and vitamin D levels in older patients. Z Gerontol Geriatr. 2018;51(4):435-439. Inapatikana kwenye linki hii: https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/28477055. Imechukuliwa 06.02.2021
23.Science M,et al. Low serum 25-hydroxyvitamin D level and risk of upper respiratory tract infection in children and adolescents. Clin Infect Dis. 2013;57(3):392-397. Inapatikana kwenye linki hii: https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/23677871. Imechukuliwa 06.02.2021
24.Fisher SA, et al. The role of vitamin D in increasing circulating T regulatory cell numbers and modulating T regulatory cell phenotypes in patients with inflammatory disease or in healthy volunteers: a systematic review. PLoS One. 2019;14(9):e0222313. Inapatikana kwenye linki hii: https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/31550254. Imechukuliwa 06.02.2021
25.Martineau AR, et al. Vitamin D supplementation to prevent acute respiratory tract infections: systematic review and meta-analysis of individual participant data. BMJ. 2017;356:i6583. Inapatikana kwenye linki hii: https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/28202713. Imechukuliwa 06.02.2021
26.Amrein K, et al. Effect of high-dose vitamin D3 on hospital length of stay in critically ill patients with vitamin D deficiency: the VITdAL-ICU randomized clinical trial. JAMA. 2014;312(15):1520-1530. Inapatikana kwenye linki hii: https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/25268295. Imechukuliwa 06.02.2021
27.National Heart Lung and Blood Institute PCTN, Ginde AA, et al. Early high-dose vitamin D3 for critically ill, vitamin D-deficient patients. N Engl J Med. 2019;381(26):2529-2540. Inapatikana kwenye linki hii: https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/31826336. Imechukuliwa 06.02.2021
28.Ross AC, et al. Dietary Reference Intakes for Calcium and Vitamin D. Washington (DC): National Academies Press (US); 2011. Inapatikana kwenye linki hii: https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK56070/. Imechukuliwa 06.02.2021
29.Siddiqi HK, Mehra MR. COVID-19 illness in native and immunosuppressed states: a clinical-therapeutic staging proposal. J Heart Lung Transplant. 2020;39(5):405-407. Inapatikana kwenye linki hii: https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/32362390. Imechukuliwa 06.02.2021
30. Arabi YM, Mandourah Y, Al-Hameed F, et al. Corticosteroid therapy for critically ill patients with Middle East respiratory syndrome. Am J Respir Crit Care Med. 2018;197(6):757-767. Inapatikana kwenye linki hii: https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/29161116. Imechukuliwa 06.02.2021
31.Stockman LJ, Bellamy R, Garner P. SARS: systematic review of treatment effects. PLoS Med. 2006;3(9):e343. Inapatikana kwenye linki hii: https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/16968120.
32.Rodrigo C, Leonardi-Bee J, Nguyen-Van-Tam J, Lim WS. Corticosteroids as adjunctive therapy in the treatment of influenza. Cochrane Database Syst Rev. 2016;3:CD010406. Inapatikana kwenye linki hii: https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/26950335. Imechukuliwa 06.02.2021
33.Horby P, Lim WS, Emberson J, et al. Effect of dexamethasone in hospitalized patients with COVID-19: preliminary report. medRxiv. 2020:[Preprint]. Inapatikana kwenye linki hii: https://www.medrxiv.org/content/10.1101/2020.06.22.20137273v1. Imechukuliwa 06.02.2021
34.Kaiser UB, Mirmira RG, Stewart PM. Our response to COVID-19 as endocrinologists and diabetologists. J Clin Endocrinol Metab. 2020;105(5). Inapatikana kwenye linki hii: https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/32232480. Imechukuliwa 06.02.2021
35.Liggins GC, Howie RN. A controlled trial of antepartum glucocorticoid treatment for prevention of the respiratory distress syndrome in premature infants. Pediatrics. 1972;50(4):515-525. Inapatikana kwenye linki hii: https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/4561295. Imechukuliwa 06.02.2021
36.Gyamfi-Bannerman C, Thom EA, Blackwell SC, et al. Antenatal betamethasone for women at risk for late preterm delivery. N Engl J Med. 2016;374(14):1311-1320. Inapatikana kwenye linki hii: https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/26842679. Imechukuliwa 06.02.2021