top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Benjamin L, MD

Alhamisi, 18 Novemba 2021

Fluoride hubadili rangi ya meno

Fluoride hubadili rangi ya meno

Mtoto chini ya umri wa miaka 8 anayetumia dawa ya meno au maji yenye fluoride kwa wingi, meno yake hubadilika rangi.


Kwanini meno ya watoto chini ya miaka nane hubadilika rangi wanapotumia fluoride?


Watoto chiini ya umri wa miaka 8 wapo hatarini kutokana na kuwa kwenye kipindi cha kupata meno ya kudumu. Kipinid hiki kama atapata fluoride kwa wingi kutoka kwenye maji au dawa ya meno meno yake yatabadilika rangi. Ukali wa tatizo utategemea kiasi cha fluoride anachopata na umri wake pia.


Je vijana wadogo na watu wazima hubadilika rangi ya meno?


Hapana!


Watoto zaidi ya umri wa miaka 8, vijana wadogo na watu wazima meno yao hayawezi badilika kutokana na matumizi ya fluoride kutoka kwenye maji au dawa ya meno.


Nini cha kufanya kuzuia meno kubadilika rangi?


Unaweza kufanya mambo yafuatayo kuzua mtoto chini ya umri wa miaka nane kubadilika rangi


Fahamu kiasi cha fluoride kwenye maji unayotumia

Kama kiasi cha fluoride kwenye maji kinazidi gramu 2 kwa kila lita moja ya maji, unapaswa kutumia vyanzo vingine vya maji ili kuzuia mtoto kupata kiasi kikubwa cha fluoride kitakachopelekea meno yake kubadilika rangi.


Kutotumia dawa ya meno au kutumia kiasi cha punje ya mchele kwa watoto chini ya umri wa miaka 2

Kwa watoto chini ya umri wa miaka miwili, wanashauriwa kutotumia dawa ya meno. Tumia kitambaa safi chenye unyevu kusafisha meno ya mtoto kwa kutumia nguvu kiasi. Kama mzazi atatumia dawa ya meno yenye fluoride, anapaswa kutumia kiasi cha punje moja ya mchele na kuhakikisha kuwa mtoto hemezi dawa. Hata hivyo dawa za watoto kama zipo zinaweza tumika kulingana na maelekezo ya mtengeneza dawa na ushauri wa daktari wako.


Kutumia dawa ya meno kiasi cha punje ya mbaazi kwa watoto umri wa miaka 2 hadi 6

Kwa watoto wenye umri wa miaka 2 hadi 6 kiasi cha dawa ya meno kinachotakiwa tumika ni kile kinachofanana na punje ya mbaazi. mzazi unapaswa kumsimamia mtoto ili asimeze dawa na asukutue mdomo mara baada ya kupiga mswaki.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

27 Novemba 2021, 08:07:27

Rejea za mada hii:

1. CDC. https://www.cdc.gov/fluoridation/faqs/dental_fluorosis/index.htm. Imechukuliwa 18.11.2021

2. DenBesten, Pamela, and Wu Li. “Chronic fluoride toxicity: dental fluorosis.” Monographs in oral science vol. 22 (2011): 81-96. doi:10.1159/000327028

3. Aoba T, et al. Effects of fluoride on matrix proteins and their properties in rat secretory enamel. J Dent Res. 1990;69:1248–1250.

4. Richards A. Nature and mechanisms of dental fluorosis in animals. J Dent Res. 1990;69(spec No):701–705. discussion 721.

5. Giambro NJ, et al. Characterization of fluorosed human enamel by color reflectance, ultrastructure, and elemental composition. Caries Res. 1995;29:251–257.

bottom of page