top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Helen L, M.D

Jumamosi, 16 Januari 2021

Fungua dirisha wakati unasafiri

Fungua dirisha wakati unasafiri

Vimelea vya maradhi ya mfumo wa upumuaji kama kifua kikuu, mafua, COVID 19 n.k huambukizwa kwa njia ya hewa wakati unasafiri na watu wengi. Mgonjwa akipiga chafya, akikohoa au kucheka hutoa vimelea wanaokaa kwenye hewa kwa masaa kadhaa. Epuka maambukizi haya wakati wa safari kwa kufungua dirisha au kuwasha kiyoyozi wakati wote ili kutoa hewa chafu nje.


Kwanini ufungue dilisha au kuwasha kiyoyozi wakati wote unapokuwa kweney chombo cha usafiri wa umma?

Kufungua dirisha unapokuwa kwenye chombo cha usafiri wa umma, ikiwa pamoja na basi, treni au gari aina yoyote inayosafirisha mtu zaidi ya mmoja, husababisha ongezeko la mzunguko wa hewa kati ya nje na ndani. Ongezeko la mzunguko wa hewa husaidia kubeba na kutoa vimelea nje ya chombo cha usafiri na hivyo kupunguza hatari ya kupata maradhi ya mfumo wa upumuaji


Mtu aliye na vimelea vya maradhi ya mfumo wa upumuaji anapoongea, kupiga chafya au kukohoa hutoa vimelea kupitia matone yanayotoka kwenye mfumo wa upumuaji. Vimelea walio kwenye matone, baadhi yake huweza kuishi kwenye hewa na wengine huangukia kwenye vitu vya karibu na mwili wa mtu aliye karibu. Endapo utavuta hewa, kugusa maeneo yaliyoangukiwa na matone na kisha kuweka mikono yako kwenye macho, pua au mdomo utapata maambukuzi ya vimelea hao.


Vimelea ambao wanaweza kuishi kwenye hewa ni kama;

 • Kirusi Adenovirus, husababisha mafua

 • Kirusi influenza, husababusha mafua

 • Kirusi Rhinovirus, husababisha mafua

 • Bakteria Bordetella pertussis husababisha kifaduro

 • Bakteria wa kifua kikuu anayeitwa Mycobacterium tuberculosis

 • Kirusi Measles, husababisha surua

 • Kirusi varicella-zoster, husababisha mkanda wa jeshi na tetekuwanga

 • Kieusi cha COVID 19, usabaisha ugonjwa wa COVID 19


Mambo ya kufanya ili kuzuia maambukizi


Zuia hatari ya kuambukizwa au kuambukiza maradhi ya mfumo wa upumuaji wakati unasafiri usafiri wa umma kwa kuzingatia mambo yafuatayo;


 • Fungua dirisha wakati wote wa safari na waombe abiria wengine pia wafanye hivyo

 • Funika kinywa chako kwa kitambaa au tishu au mkunjo wa kiwiko cha mkono unapokuwa unakohoa au kupiga chafya. Baada ya kutumia tishu, tunza ili kuitupa sehemu salama.

 • Endapo umekaa na mgonjwa mwelekeze adhibiti kusafirisha vimelea, mwambie atumie barakoa, kitambaa au mkunjo wa kiwiko cha mkono.

 • Endapo unaumwa magonjwa ya mfumo wa upumuaji, kaa nyumbani mpaka upone ndipo usafiri ili kuwalinda watu wengine

 • Endapo wewe ni mgonjwa na ni lazima kusafiri, safari umevaa barakoa huku umebeba vitakasa mikono, tishu au vitambaa vya kutosha. Usitumie kiganja cha mkono kuzuia kikohozi, usishike shike vitu karibu nawe ili kuzuia kuwaambukiza watu wengine

 • Nawa mikono yako unapotaka kula kitu, kugusa uso wako na mara baada ya kutoka kwenye usafiri wa umma

 • Usitumie vifaa pamoja na mgonjwa kama maji, vyombo vya kulia, wakati wote wa safari

 • Tembea na kitakasa mikono endapo unasafiri kwenye usafiri wa umma ili kutakasa mikono mara unaposhika vitu ambavyo havina usalama, au epuka kula au kiweka mikono usoni kabla ya kunawa mikono

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

19 Julai 2023 20:41:55

Rejea za mada hii:

1. Disease of the respiratory system. https://www.cdc.gov/disasters/disease/respiratoryic.html#. Imechukuliwa 15.01.2020
2. Airborne and Direct Contact Diseases. https://www.maine.gov/dhhs/mecdc/infectious-disease/epi/airborne/index.shtml. Imechukuliwa 15.01.2020
3. S A Baker. Airborne transmission of respiratory diseases. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/10152447/. Imechukuliwa 15.01.2020
4. How are respiratory viruses transmitted?. https://www.aappublications.org/content/35/1/1.2. Imechukuliwa 15.01.2020
5. Diseases Transmitted by Respiratory Routes. https://www.gov.nl.ca/hcs/files/publications-diseasecontrol-dcresp.pdf. Imechukuliwa 15.01.2020
6. BAKER SHIRLEY. A. Ph.D. etal. Airborne transmission of respiratory disease. https://journals.lww.com/jcejournal/abstract/1995/09000/airborne_transmission_of_respiratory_diseases.15.aspx. Imechukuliwa 15.01.2020

bottom of page