Mwandishi:
Dkt. Sospeter B. MD
Mhariri:
Dkt Salome A, MD
Jumatatu, 31 Julai 2023
Gono huonekana baada ya muda gani?
Gono au gonorea ni ugonjwa wa zinaa unaoambukizwa, husababishwa na bakteria mwenye jina la Neisseria gonorrhea. Gono huathiri ngozi laini kwenye njia ya uzazi ikiwa pamoja na shingo ya uzazi, kizazi, mirija ya falopio kwa wanawake na mrija urethra kwa wanaume na wanawake.
Kimelea wa gono pia huweza athiri kinywa, koo, macho na puru (kifuko cha kutunzia kinyesi kwa muda kilico karibu na njia ya haja kubwa).
Gono huonekana muda gani tangu kuambukizwa?
Wanawake wengi na baadhi ya wanaume wanapopata gono huwa hawaonyeshi dalili yoyote ile, endapo dalili zitaonekana huonekana siku 2 hadi 21 tangu siku ya kushiriki ngono.
Dalili za gono
Dalili na viashiria vya gono kwa wanawake ni pamoja na;
Kutokwa na ute mzito wa kahawia au njano ukeni
Hisia za kuungua au maumivu wakati w akukojoa au kujisaidia haja kubwa
Kupata hedhi isiyo kawaida
Kutokwa damu katikati ya vipindi vya hedhi
Mijongeo ya misuli na maumivu ya tumbo la chini ya kitovu
Dalili za gono kwa wanaume
Kutokwa na uchafu wa njano au kijani kwenye kilele cha uume
Maumivu au hisia za kuungua wakati wa kukojoa au kujisaidia haja kubwa
Kukojoa mara kwa mara
Kuvimba korodani au maumivu ya korodani
Utambuzi
Utambuzi wa gono kwa wanaume na wanawake ni kwa kupitia kipimo cha sampuli ya mkojo. Kipimo cha ute pia kinaweza kufanyika kwa wanawake na wanaume kwa kutoa ute ukeni au kwenye uume au kwenye puru.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
1 Agosti 2024 18:38:43
Rejea za mada hii:
1. Lytle-Barnaby R. Sexually Transmitted Diseases: An Overview. Dela J Public Health. 2016 Apr 18;2(2):26-31. doi: 10.32481/djph.2016.04.009. PMID: 34466839; PMCID: PMC8389050.
2. Sexually Transmitted Infections. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK560808/. Imechukuliwa 31.07.2023
3. Gono. ULY CLINIC. https://www.ulyclinic.com/magonjwa-na-saratani/Gono. Imechukuliwa 31.07.2023