top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Charles W, M.D

Alhamisi, 18 Februari 2021

Homoni estrogen inahusishwa na saratani ya titi

Homoni estrogen inahusishwa na saratani ya titi

Kuvunja ungo mapema, kuchelewa uzazi wa kwanza, kutonyonyesha, kuchelewa koma hedhi na kutumia dawa za uzazi wa mpango huanika matiti yako kwenye homoni estrogen, kihatarishi cha saratani ya titi. Jenga tabia ya kujichunguza endapo una moja ya kihatarishi.


Wanawake wanaojianika ni wapi?


Kujianika katika kidokezo hiki imetumika kumaanisha kitendo la kujiweka kwa muda mrefu kwenye kiwango kikubwa cha homoni estrogen inayozunguka kwenye damu. Homoni estrogen inapokuwa kwa wingi kwenye damu huongeza hatari yakupata saratani ya titi. Wananawake wafuatao wapo kwenye kundi la wanaojianika kwenye kiwango kikubwa au kwa muda mrefu kwenye homon estrogen.


Umri wa kuvunja ungo


Kuvunja ungo mapema ni kihatarishi kimojawapo cha kupata saratani ya titi kwa wanawake wanapofikia umri kabla au baada ya komahedhi. Kuchelewa kwa koma hedhi kwa muda wa miaka miwili huhusiana pia kupunguza hatari ya saratani ya titi kwa asilimia 10. Uchunguzi unaonyesha kuwa wanawake wanaovunja ungo kabla au wakiwa na miaka 13 huwa na kihatarishi mara mbili zaidi ya kupata saratani ya titi.


Umri wa kuingia koma hedhi


Kuchelewa kuingia kipindi cha komahedhi huambatana na ongezeko la hatari ya kupata saratani ya titi. Kila mwaka mwanamke anaochelewa kuingia kipindi cha komahedhi, huongeza hatari kwa asilimia 3 zaidi na kuchelewa kwa kila baada ya miaka mitano huongeza hatari kwa asilimia 17 zaidi kupata saratani ya titi.


Idadi ya uzazi na umri wa kwanza kupata uzazi wa kwanza


Wanawake ambao hawajawahi pata uzazi wa kwanza wanahatari kubwa ya kupata saratani ya titi ukilinganisha kwa wanawake ambao wameshakuwa na uzazi zaidi ya mmoja. Kupata mimba katika umri mdogo ni kinga, wakati huo huo kupata mimba katika umri mkubwa ni kihatarishi cha kupata saratani ya titi ukilinganisha na wanawake ambao hawana watoto kabisa. Hatari ya kupata saratani ya titi hupungua kwa asilimia 20 kwa wanawake wanaopata ujauzito kwenye umri wa miaka 20, kwa asilimia 10 kwa wanawake wanaopata ujauzito kwenye umri wa miaka 30 na kwa asilima 5 kwa wanawake wanaopata mimba kwenye umri wa miaka 35.


Kunyonyesha


Ushahidi wa kitafiti unaonnyesha kuwa, kunyonyesha hupunguza hatari ya kupata saratani ya titi. Hii ni kwa sababu kunyonyesha husaidia kuzuia kurejea kwa mzunguko wa hedhi baada ya kujifungua, hivyo kupunguza matiti yako kujianika kwenye homoni mojawapo inayohusika kwenye mzunguko wa hedhi, yaani homon estrogen.


Homon testosterone


Kuwa na kiwango kikubwa cha homoni testosterone huongeza hatari ya kupata saratani ya titi kwa wanawake wanaokaribia koma hedhi na wale ambao wampo kwenye kipindi cha koma hedhi. Wanawake wenye kiwango kikubwa cha homon testosterone, wana hatari mara 2 hadi tatu zaidi ya kupata saratani kuliko wale wenye kiwango cha kawaida.
Dawa za uzazi wa mpango


Matumizi ya dawa za uzazi wa mpango zenye lego la kurejesha kiwango cha homoni estrogen na progesterone kwa wanawake walio kwenye koma hedhi, zenye jina tiba la 'Hormonal Replacement Therapy' HRT huongeza hatari ya kupata saratani, hupunguza utambuzi wa saratani ya titi mapema na huongeza hatari ya kufa mapema kwa sababu ya saratani ya titi kwa wanawake waliokoma hedhi hali ingali mfuko wao wa uzazi haujaondolewa.


Tafiti zilizofanywa kwa kuwapa wanawake homoni hizi zilisitishwa mara moja mara baada ya kuonyesha matokeo haya. Hata hivyo tafiti zingine zinaonyesha kuwa, matumizi ya dawa za HRT zenye homon estrogen tu kwa wanawake ambao hawana mfuko wa uzazi, hupunguza hatari ya saratani kwao na huwa haizuii kutambuliwa kwa saratani wala kuongeza hatari ya kifo. Kwa ujumla matumizi ya HRT zenye homon ya estrogen tu, huongeza hatari ya kupata saratani ya titi kwa asilimia 23, endapo utaongeza na homon progesteron hatari huongezeka mara dufu zaidi.


Vihatarishi vingine


Vihatarishi vingine ni;

  • Kuwa na historia ya saratani ya titi jingine

  • Kuwa na historia ya saratani ya titi kwenye familia ya wazazi wako

  • Kuwa na historia ya saratani ya titi kwa ndugu wa damu

  • Kunywa pombe kupita kiasi

  • Kuwa na uzito mkubwa kupita kiasi au ugonjwa wa obeziti

  • Kupigwa na mionzi hatari

  • Kutofanya mazoezi na

  • Kutokula mlo wa kiafyaULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi


Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

19 Julai 2023 20:41:21

Rejea za mada hii:

1.Ruth C Traviset al. Oestrogen exposure and breast cancer risk. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC314432/. Imechukuliwa 18.02.2021

2.Cancer. https://www.who.int/news-room/fact-sheets/detail/cancer. Imechukuliwa 18.02.2021

3. Hsieh CC et al. Age at menarche, age at menopause, height and obesity as risk factors for breast cancer: associations and interactions in an international case-control study. Int J Cancer. 1990;46:796–800

4.Ritte R eta al. Clavel-Chapelon F, Fournier A, et al. Adiposity, hormone replacement therapy use and breast cancer risk by age and hormone receptor status: a large prospective cohort study. Breast Cancer Res. 2012;14:R76

5.Rosner B et al. Reproductive risk factors in a prospective study of breast cancer: the Nurses’ Health Study. Am J Epidemiol. 1994;139:819–835

6.Collaborative Group on Hormonal Factors in Breast Cancer. Breast cancer and breastfeeding: collaborative reanalysis of individual data from 47 epidemiological studies in 30 countries, including 50302 women with breast cancer and 96973 women without the disease. Lancet. 2002;360:187–195.kiungo. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC4127601/#B26. Imechukuliwa 18.02.2021

7. Sieri S et al. Sex hormone levels, breast cancer risk, and cancer receptor status in postmenopausal women: the ORDET cohort. Cancer Epidemiol Biomarkers Prev. 2009;18:169–176. Kiungo https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/19124495/. Imechukuliwa 18.02.2021

8. Anderson GL, et al. Implementation of the Women’s Health Initiative study design. Ann Epidemiol. 2003;13:S5–17. Kiungo. .https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/14575938/. Imechukuliwa 18.02.2021

9. Colditz GA et al. Cumulative risk of breast cancer to age 70 years according to risk factor status: data from the Nurses’ Health Study. Am J Epidemiol. 2000;152:950–964. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/11092437/. Imechukuliwa 18.02.2021

bottom of page