Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Charles W, M.D
Jumatano, 10 Februari 2021
Imarisha kinga ya mwili wako kwa chakula
Uwezo wa mwili kupambana na maradhi hutegemea kile unachokula. Ongeza uwezo huo kwa kutumia vyakula kama matunda yenye uchachu, pilipili hoho, tangawizi, vitunguu swaumu, spinachi n.k.
Vyakula vyenye uwezo mkubwa wa kuongeza kinga ya mwili
Vyakula hivi huwa na viwango tofauti tofauti ya virutubisho na madini kwa wingi vinavyohusika kuamsha mfumo wa kinga mwilini. Virutubisho na madini kwa wingi viliyo kwenye vyakula vilivyoorodeshwa hapo chini huwa na vitamini B-6,C, D, 'folic acid', madini chuma, kopa na madini zinc. Virutubisho vingi tunavyokula huwa havitengenezwi na mwili, hivyo unahitaji kula vyakula hivyo kila siku ili upate virutubisho hivyo. Kumbuka ni muhimu kula mlo kamili kila siku kutoka kwenye makundi matano ya chakula.
Virutubisho na madini kutoka kwenye vyakula vilivyotajwa hapa chini hufanya kazi zifuatazo ili kuimarisha mfumo wa kinga mwilini
Hupunguza mwitikio wa mwili dhidi ya maradhi ya virusi na vimelea wengine wa magonjwa
Huamsha uboho wa mifupa kuzalisha chembe nyeupe za damu zinazopambana na maradhi mbalimbali
Huamsha mfumo wa kinga za mwili wenye jina la ‘adaptive immunity’ na ‘innate immunity’ unaopambana na maradhi ya virusi, bakteria na fangasi
Vykakula vyenye uwezo wa kuongeza kingazako ya mwili vimeorodheshwa hapa chini.
Vyakula vichachu na matunda
Vyakula vichachu huwa na vitamin C kwa wingi ambayo hufanya kazi kubwa ya kuongeza kinga ya mwili
Vyakula vichachu
Zabibu
Machungwa
Chenza
Limao
Ndimu
Maziwa mgando
Vyakula vingine vilivyochachushwa
Matunda yasiyo na chachu
Papai
Kiwi
Ndizi
Mboga za majani
Baadhi ya mboga za majani zenye uwezo mkubwa wa kuongeza kinga ya mwili ni;
Spinachi
Broccoli
Viungo vya chakula
Kitunguu swaumu
Kitunguu maji
Unga wa mmea wa manjano
Tangawizi
Majani ya chai
Pilipili hoho nyekundu
Karanga
Karanga za alizeti
Karanga za lozi(almondi)
Karanga za maboga
Nyama na viumbe mbalimbali
Nyama yenye uwezo wa kuongeza kinga ya mwili ni pamoja na;
Nyama ya kuku
Viumbe wa baharini wenye madini ya zinc na vitamin C kwa wingi huwa pamoja na;
Kaa
Chaza
Kamba
Kome
Kumbuka
Unashauriwa kula mlo kamili kila siku ili kuimarisha kinga ya mwili wako
Kula vitu vilivyoorosheshwa hapo juu kwa wingi huweza sababisha matatizo mengine mfano, unapotumia limao au tangawizi kwa wingi unahatari ya kupata vidonda vya tumbo n.k. hivyo kula kwa kiasi kinachofaa kiafya au kulingana na ushauri wa daktari wako
Mwili unahitaji kiwango kidogo tu cha madini na vitamini kila siku ili uweze kuimarisha kinga ya mwili.
Soma vidokezo vingine kuhusuana na lishe kwa kubofya hapa
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
19 Julai 2023 20:41:21
Rejea za mada hii:
1.Michele Catanzaro, et al. Immunomodulators Inspired by Nature: A Review on Curcumin and Echinacea. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/30373170/. Imechukuliwa 09.02.2021
2.U.S. DEPARTMENT OF AGRICULTURE. Agricultural Research Servicehttps://fdc.nal.usda.gov/index.html. Imechukuliwa 09.02.2021
3.Garlic. https://www.nccih.nih.gov/health/garlic. Imechukuliwa 09.02.2021
4.William B. Grant, et al. Evidence that Vitamin D Supplementation Could Reduce Risk of Influenza and COVID-19 Infections and Deaths. https://www.mdpi.com/2072-6643/12/4/988. Imechukuliwa 09.02.2021
5.ChowdhuryFaiz Hossain, et al. Analgesic principle from Curcuma amada . https://linkinghub.elsevier.com/retrieve/pii/S0378874115000331. Imechukuliwa 09.02.2021
6.Shaheen E. Lakhan , et al. Zingiberaceae extracts for pain: a systematic review and meta-analysis. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC4436156/. Imechukuliwa 09.02.2021
7.Brian K. McFarlin , et al. Reduced inflammatory and muscle damage biomarkers following oral supplementation with bioavailable curcumin. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC4802396/. Imechukuliwa 09.02.2021
8.The effect of ginger supplementation on lipid profile: A systematic review and meta-analysis of clinical trials
9.Makan Pourmasoumi, et al. The effect of ginger supplementation on lipid profile: A systematic review and meta-analysis of clinical trials. https://linkinghub.elsevier.com/retrieve/pii/S0944711318300783. Imechukuliwa 09.02.2021
10.Saurabh Pandey , et al. Anti-inflammatory and immunomodulatory properties of Carica papaya. https://www.tandfonline.com/doi/full/10.3109/1547691X.2016.1149528. Imechukuliwa 09.02.2021
11.NIH. Vitamin E. https://ods.od.nih.gov/factsheets/VitaminE-Consumer/. Imechukuliwa 09.02.2021
12.NIH. Vitamin B-6. https://ods.od.nih.gov/factsheets/VitaminB6-HealthProfessional/. Imechukuliwa 09.02.2021
13.Gao-feng Yuan , et al. Effects of different cooking methods on health-promoting compounds of broccoli*. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC2722699/. Imechukuliwa 09.02.2021
14.NIH. Zinc. https://ods.od.nih.gov/factsheets/Zinc-Consumer/. Imechukuliwa 09.02.2021
15.Harvard school of public health. Nutrition and Immunity, et al. https://www.hsph.harvard.edu/nutritionsource/nutrition-and-immunity/. Imechukuliwa 09.02.2021