top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Helen L, M.D

Jumapili, 17 Januari 2021

Jali afya yako, fanya ngono salama

Jali afya yako, fanya ngono salama

Kufanya ngono salama itakulinda dhidi ya mimba zisizotarajiwa na maradhi ya VVU, kaswende, kisonono n.k. Ili ufanye ngono salama, fahamu na tumia kinga zilizopo, mfano PrEP itakukinga kupata VVU, kondomu itakukinga kupata mimba, magonjwa ya zinaa ikiwa pamoja na VVU. Jali afya yako kwanza.


Kwanini nijali kuhusu kinga?


Kufahamu kuhusu kinga itakusaidia kuwa na afya njema na uweze kutumiza malengo yako katika maisha. Kuna magonjwa mengi yanayoambukizwa kwa njia ya ngono, mengi yanaweza kuzuilika kwa kutumia kinga zinazofahamika.


Endapo utatumia kondomu utazuia kupata maradhi yafuatayo;

  • Kisonono

  • Kaswende

  • Pangusa

  • Trichomoniasis

  • Sunzua maeneo ya siri( genital warts)

  • Vidonda vya magonjwa ya zinaa sehemu za siri

  • Maambukizi ya virusi vya UKIMWI

  • Saratani ya shingo ya kizazi


Je kondomu ina uwezo wa kukukinga kwa asilimia ngapi?


Licha ya kondomu kuwa na uwezo wa kukukinga na magonjwa ya zinaa, tafiti zinaonyesha si kwa asilimia 100. Hii inaweza kuchangiwa na mambo mbalimbali ikiwa pamoja na matumizi yasiyo sahihi au kutotumia mara zote. Unashauriwa kufahamu namna sahihi ya kutumia kondomu ili kupata ulinzi wake mkubwa.


Virusi vya UKIMWI havizuiliki kwa asilimia 100 kwa kutumia kondomu, endapo hufahamu matumizi sahihi ya kondomu, tumia dawa za kinga dhidi ya maambukizi kama PrEP kwa usalama zaidi.


Zingatia njia zingine pia za kujikinga na maambukizi ya magonjwa ya zinaa, ikiwa pamoja na kuacha kufanya ngono au kuwa na mpenzi mwaminifu aliyepima magonjwa ya zinaa ikiwa pamoja na UKIMWI.


Taarifa zingine unazipata wapi?


Kwa uelewa zaidi kuhusu PrEP, soma zaidi kwenye linki zilizo ndani ya tovuti hii.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

19 Julai 2023 20:41:55

Rejea za mada hii:

1.Health New York Government. Frequently Asked Questions (FAQs) About Condoms. https://www.health.ny.gov/diseases/aids/consumers/condoms/faqs.htm#. Imechukuliwa 16.01.2021

2.CDC. Condom Fact Sheet In Brief. https://www.cdc.gov/condomeffectiveness/brief.html. Imechukuliwa 16.01.2021

3.Male Latex Condoms and Sexually Transmitted Diseases. https://health.williams.edu/medical-diagnoses/sexual-and-reproductive-health/male-latex-condoms-and-sexually-transmitted-diseases/. Imechukuliwa 16.01.2021

bottom of page