top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Charles W, M.D

Alhamisi, 4 Machi 2021

Kipindi cha kunyonyesha, mwanamke huwa na uke mkavu

Kipindi cha kunyonyesha, mwanamke huwa na uke mkavu

Mwanamke anayenyonyesha huzalisha kwa kiasi kidogo sana au kutozalisha kabisa ute ute ukeni licha ya kuandaliwa vya kutosha kabla ya kujamiana. Wakati wa kunyonesha inashauriwa kutumia vilainisha uke ili kuepuka maumivu.


Unakabiliana vipi na uke mkavu kwa mama anayenyonyesha?


Mama anayenyonyesha kwa kawaida huwa na uke mkavu, hii ni kwa sababu ya mabadiliko ya homoni yanayotokea kipindi cha kunyonyesha. Mama anayenyonyesha atapata maumivu makali akishiriki ngono kipindi cha kunyonyesha kwa sababu ya kuzalishwa kwa kiasi kidogo au kutozalishwa kabisa. Kipindi hiki ni muhimu mama akatumia vilainishi vingine vinavyofahamika ili kuweza kushiriki ngono bila maumivu.


Vilainishi hivi vinapaswa kutumiwa na mama kwa kupaka kwenye mashavu ya uke na ndani ya tundu la uke pamoja na mpenzi kupaka kwenye maeneo ya uume. Matumizi ya mate yanaweza yasisaidie na hivyo maumivu kuendelea.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

19 Julai 2023 20:41:12

Rejea za mada hii:

1. Alder E, et al. The relationship between breastfeeding persistence, sexuality and mood in postpartum women. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/3399590/. Imechukuliwa 4.03.2021

2. Viola Polomeno, et al. Sex and Breastfeeding: An Educational Perspective. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3431754/. Imechukuliwa 4.03.2021

3. Dettwyler K,et al. Sexuality and breastfeeding. Journal of Human Lactation. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/8634100/. Imechukuliwa 4.03.2021

4. Gamble D, et al. Postponing and types of involvement. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/8410435/. Imechukuliwa 4.03.2021

5. Hotchner T. Pregnancy and childbirth. 1990. Imechukuliwa 4.03.2021

6. Huggins, et al. The Nursing Mother's Guide to Weaning-Revised: How to Bring Breastfeeding to a Gentle Close, and How to Decide When the Time Is Right. Harvard Common Press, 2007. Imechukuliwa 4.03.2021

7. Lawrence R. Breastfeeding: A guide for the medical profession. CV Mosby Company; St. Louis, MO. 1989. Imechukuliwa 4.03.2021

8. Polomeno V. Sex and breastfeeding: An educational perspective. The Journal of perinatal education. 1999;8(1):30. Imechukuliwa 4.03.2021

9. Lethbridge DJ. The use of breastfeeding as a contraceptive. Journal of Obstetric, Gynecologic, & Neonatal Nursing. 1989 Jan;18(1):31-7. Imechukuliwa 4.03.2021

bottom of page