Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Lugonda M, M.D
Jumanne, 12 Januari 2021
Kunyonyesha ni kinga kwa mwanamke| ULY CLINIC
Kunyonyesha mtoto huzuia hatari ya mama kupata saratani ya titi na ovari kwa asilimia zaidi ya
Kwanini kunyonyesha hupunguza hatari ya kupata saratani?
Sababu moja wapo kuu ni kwamba, mama anayenyonyesha huwa na kipindi cha mabadiliko ya homoni ambayo husababisha kuchelewa kurejea kwa mzunguko wa hedhi. Hali hii ya kuchelewa kurejea kwa mzunguko wa hedhi hupunguza kujianika kwenye homoni ya mzunguko wa hedhi inayoitwa oestrojen inayodhaniwa na wanasayansi kuhusika na kusababisha saratani ya titi na ovari.
Mbali na kukukinga na saratani, kunyonyesha hupunguza hatari ya mama kupata
Kisukari aina ya pili
Shinikizo la juu la damu
Mama unashauriwa kunyonyesha mwanao ili akue na afya njema pamoja na kujikinga na magonjwa mbalimbali.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
19 Julai 2023 20:43:43
Rejea za mada hii:
1. Breastfeeding for Cancer Prevention. https://blogs.cdc.gov/cancer/2019/08/01/breastfeeding-for-cancer-prevention/. Imechukuliwa 12.01.2021
2. Breastfeeding and the Use of Human Milk. https://pediatrics.aappublications.org/content/129/3/e827. Imechukuliwa 12.01.2021