Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Benjamin L, Dkt. AdolfS, MD
Jumamosi, 28 Agosti 2021
Kuongezewa damu
Ni tendo la kitiba la kuongeza ujazo wa damu iliyotolewa kwa mtu mwenye afya kwenda kwa muhitaji kupitia mishipa ya damu. Sababu zinazopelekea kuongezewa damu mara nyingi hutokana na ajali, upasuaji na magonjwa yanayomaliza damu. Kuna njia zingine za kuongeza damu, hata hivyo si rahisi kutumika kama mbadala wa kuongezewa damu.
Sababu za kuongezewa damu
Kuongezewa damu kunapaswa kufanyika kwa mtu ambaye hakuna namna nyingine yeyote ya kitabibu inayoweza kumsaidia ili kupandisha kiwango cha damu kwa haraka. Sababu mbalimbali zinazoweza pelekea mtu kuongezewa damu ili kuokoa maisha ni;
Upungufu wa damu unaotokea na dalili kama vile (kuishiwa pumzi, kizunguzungu, moyo kuferu na kupungua uwezo wa kufanya mazoezi)
Dalili kali za seli mundu
Kuvuja zaidi ya asilimia 30 ya damu mwilini
Aina za damu zinazoongezwa
Kuna aina kadhaa ya kuonezewa damu kutokana na sehemu gani ya damu unayoingiziwa kwenye mishipa. Aina hizo ni;
Kuongezewa plazima
Kuongezewa chembe sahani za damu
Kuongezewa chembe nyekundu za damu
Ni nani anayehitaji kuongezewa damu ?
Mtu aliyevuja sana damu kutokana na
Ajali
Upasuaji
Kutoa mimba
Madhara makubwa ya kujifungua
Mtu aliyeishiwa damu kutokana na maradhi mbalimbali kama
Seli mundu
Saratani ya damu
Vijisumu vya bakteria kwenye damu
Maradhi ya moyo
Madhara na maudhi ya kuongezewa damu
Kuna madhara ya muda mfupi na yale ya uda mrefu kama yalivyoelezewa hapa chini
Maudhi ya muda mfupi
Ugonjwa mkali wa kuvija damu
Mwitikio wa mzio
Mzio wa anafailaksia
Kuganda kwa damu kama umeongezewa damu nyingi
Homa isiyotokana na kuvunjwa kwa damu
Uharibifu wa kimetabolizimu
Kuonegzewa damu isiyo sahihi
Kupata maradhi ya bakteria kwenye damu kama damu imechanganyika na vimelea wakati wa kuongezewa
Kuzidiwa kwa moyo na damu
Majeraha kutokana na mchakato wa kuongezewa damu
Mwitikio wa kuvimba mwili
Maudhi yanayotokea baadaye
Kuvunjwa kwa damu
Kuzidi kwa madini chuma kwenye damu
Damu kuwa nyingi kuliko kawaida
Harara za kuongezewa damu
Ugonjwa wa mwitikio wa kukataana kwa damu mpya uliyoongezewa
Magonjwa yanayoambukizwa kwa kuongezewa damu
Magonjwa haya huweza ambukizwa kwa nadra sana na endapo damu haijapimwa
Kurusi cha Hepatitis B
Kirusi cha Hepatitis C
Kirusi 1 na 2 cha Human T-lymphotropic
Kirusi cha UKIMWI
Ugonjwa wa Creutzfeldt-Jakob
Kirusi cha Human herpesvirus 8
Ugonjwa wa Malaria
Ugonjwa wa babesiosis
Mafua ya mlipuko
Kirusi cha West Nile
Njia zingine za kuongeza damu mwilini
Ikitegemea na kisababishi, kuna njia zingine unaweza kuchukua ili kuongeza uzalishaji wa chembe nyekundu za damu, hata hivyo njia hizi zinatumika kwa muda zaidi ya miezi mitatu ili kuwa na kiwango cha damu kinachokidhi mahitaji ya mwili. Mambo hayo ni;
Kula vyakula vyenye madini chuma kwa wingi
Kula vyakula vyenye madini ya folic acd kwa wingi
Vyakula vyenye madini chuma kwa wingi;
Nyama nyekundu au nyeupe
Rozera
Vyakula vya baharini
Maharagwe
Mboga za ukijani uliokolea kama spinachi
Matunda yaliyokaushwa kama aprikoti
Peasi
Vyakula vinavyoongeza ufyonzaji wa madini chuma
Licha ya kula chakula au vidonge vya madini chuma, ni kiasi kidogo kitafyonzwa na kuingia mwilini. Kula vyakula vifuatavyo( vina vitamin C kwa wingi) vitaongeza ufyonzaji wa madini hayo na kupelekea kuwepo kwenye damu na mifupa kwa ajili ya kufanikisha utengenezaji wa damu;
Brokoli
Zabibu
Kiwi
Mboga za majani
Tikiti maji
Machungwa
Pilipili
Nyanya
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
6 Oktoba 2021 16:03:51
Rejea za mada hii:
Hébert PC, et al. A multicenter, randomized, controlled clinical trial of transfusion requirements in critical care. Transfusion Requirements in Critical Care Investigators, Canadian Critical Care Trials Group [published correction appears in N Engl J Med. 1999;340(13):1056]. N Engl J Med. 1999;340(6):409–417
Transfusion of Blood and Blood Products: Indications and Complications. https://www.aafp.org/afp/2011/0315/p719.html. Imechukuliwa 18/8/2021
WHO. Blood Donation. Clinical transfusion practice. Imechukuliwa 18/8/2021https://www.who.int/bloodsafety/transfusion_services/ClinicalTransfusionPracticeGuidelinesforMedicalInternsBangladesh.pdf. Imechukuliwa 18/8/2021
Blood Donation,Mayo Clinic, https://www.mayoclinic.org/tests-procedures/blood-transfusion/about/pac-20385168. Imechukuliwa 18/8/2021
CDC. Blood safety basic, https://www.cdc.gov/bloodsafety/basics.html. Imechukuliwa. 18/8/2021
PubMed. Blood transfusion. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/26632625/ , Imechukuliwa 18/8/2021
Blood transfusion, Medscape, https://emedicine.medscape.com/article/434176-overview , Imechukuliwa 18/8/2021