Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Mangwella S, MD
Jumanne, 12 Januari 2021

Kupasuka chupa ya uzazi kabla ya wakati
Kupasuka kwa chupa ya uzazi kabla ya kutimiza wiki 37 kamili za ujauzito hujulikana kama 'kupasuka kwa chupa ya uzazi kabla ya wakati'. Tatizo hili hutokea kwa ujauzito 3 kati ya 100, kuwahi pata matibabu sahihi hukinga madhara ya kujifungua mtoto njiti, maambukizi ndani ya mfuko wa uzazi na magonjwa kwa mtoto.
Maelezo ya undani
Kabla ya mtoto kuzaliwa, chupa ya uzazi hupasuka na kuruhusu maji kumwagika kwa kasi nje ya uzazi na mara chache sana huchuruzika taratibu. Uchungu huanza muda mfupi mara baada ya chupa ya uzazi kupasuka, kama utatokea wakati huu utapelekea kujifungua kabla ya wakati na hatari ya kupata mtoto njiti.
Visababishi vya kupasuka chupa ya uzazi kabla ya wakati
Mara nyingi visababishi vya kupasuka chupa ya uzazi kabla ya wakati huwa havifahamiki, hata hivyo visababishi vikuu ni;
Maambukizi ndnai ya mfuko wa uzazi
Kutanuka kupita kiasi kwa mfuko wa uzazi kutokana na kuwa na ujauzito wa mapacha au maji mengi kwenye chupa ya uzazi
Mgandamizo tumboni kutokanana ajali au kupigwa
Matokeo ya kupasuka chupa ya uzazi kabla ya wakati
Mara nyingi mara baada ya kupasuka kwa chupa ya uzazi, uchungu huanza. Baadhi ya nyakati endapo kuna maambukizi ndani ya mfuko wa uzazi, uchungu huchelewa kuanza kuanza kwa siku kadhaa. Kama chupa ya uzazi itapasuka karibu zaidi na mwisho wa ujauzito, mara nyingi.
Baadhi ya nyakati chupa ya uzazi iliyopasuka huweza kuziba yenyewe na kuzuia uchungu kuanza. Kwa nadra sana, ujauzito unaweza kubebwa mpaka mwishoni mwa kipindi cha ujauzito kama chupa imepasuka katika kipindi cha pili cha ujauzito. Maatokeo zaidi ya kupasuka kwa chupa ya uzazi kabla ya wakati ni;
Shida ya upumuaji kwa mdodo- sindromu ya upumuaji wa shida ( asilimia 35 ya ujauzito)
Maambukizi kwa mtoto ( asilimia 13 hadi 60 ya ujauzito)
Kujitanguliza kwa kitovu cha mtoto
Kunyofoka kwa kondo la nyuma( asilimia 4 hadi 12 ya ujauzito)
Kufa kwa kichanga( asilima 1 hadi 2 ya ujauzito)
Kujifungua ndani ya wiki moja (asilimi 50 hadi 75 ya ujauzito)
Mgandamizo kwenye kitovu cha mtoto ( asilimia 32 hadi 76 ya ujauzito)
Matibabu ya kupasuka kwa chupa ya uzazi kabla ya wakati
Matibabu ya kupasuka kwa chupa ya uzazi kabla ya wakati huhusisha;
Kupatiwa dawa jamii ya corticosteroid kwa ajili ya kukomaza mapafu kwenye umri wa wiki 34 au kabla
Matibabu ya subilifu ili kuipa muda chupa ya uzazi kujifunga
Dawa za antibayotiki kuzuia maambukizi kwenye kuta za uzazi
Kuanzishiwa uchungu kwa dawa kama uchungu hautaanza wenyewe. Uchungu huanzishwa endapo kuna hatari ya maambukizi au mtoto tayari ameshakomaa mapafu
Matibabu mengine kusubilisha uchungu kwa muda
Baada ya kupasuka kwa chupa ya uzazi, matumizi ya dawa za kuzuia uchungu mara nyingi huwa hazina mafanikio makubwa, hata hivyo zinaweza kutumika kuzuia uchungu kuanza kabla ya wakati ndani ya masaa 24 baada ya kutumia dawa za corticosteroid ili kukomaza mapafu ya mtoto au kwa nia ya kumsafirisha mama mpaka kituo cha afya chenye huduma ya watoto njiti kabla ya kujifungua.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
6 Oktoba 2021, 16:04:19
Rejea za mada hii:
1. Preterm Prelabor Rupture of Membranes (pPROM). https://www.mottchildren.org/health-library/hw221349. Imechukuliwa 14.08.2021
2. TANYA M. MEDINA, M.D, et al. American family of physician. Preterm Premature Rupture of Membranes: Diagnosis and Management. https://www.aafp.org/afp/2006/0215/p659.html. Imechukuliwa 14.08.2021
3. Premature Rupture of Membranes (PROM)/Preterm Premature Rupture of Membranes (PPROM). https://www.chop.edu/conditions-diseases/premature-rupture-membranes-prompreterm-premature-rupture-membranes-pprom#. Imechukuliwa 14.08.2021