top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Benjamin L , MD

Jumatano, 13 Januari 2021

Kupasuka kwa chupa ya uzazi kabla ya uchungu

Kupasuka kwa chupa ya uzazi kabla ya uchungu

Kupasuka kwa chupa ya uzazi kabla ya uchungu ni kuchanika kwa kuta za chupa ya uzazi kabla uchungu kuanzana baada ya ujauzito kutimiza wiki 37, hali hii ni kawaida kutokea kwenye ujauzito 10 kati ya 100.


Nini husababisha kupasuka kwa chupa ya uzazi kabla ya uchungu?


Kupasuka kwa chupa ya uzazi karibia na mwishoni mwa ujauzito huweza kusababishwa na udhaifu asilia wa kuta za mfuko wa uzazi kutokana na mwili kujiandaa kutoa kujifungua na madhara ya nguvu za ujongevu wa misuli ya uzazi. Baadhi ya sababu zinazoambatana na kupasuka kwa chupa ya uzazi kabla ya uchungu ni;


  • Hali duni ya kimaisha, inayoambatana na kukosa huduma njema kliniki

  • Maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama klamidia na kisonono

  • Historia ya kupasuka kwa chupa ya uzazi kabla ya uchungu

  • Kutokwa na damu ukeni

  • Uvutaji wa sigara wakati wa ujauzito

  • Sababu zisizojulikana


Kwanini uhofie kuhusu kupasuka kwa chupa ya uzazi kabla ya uchugnu?


Kupasuka kwa chupa ya uzazi kabla ya uchungu huongeza hatari ya;


  • Kupata maambukizi kwenye mji wa uzazi na chupa ya uzazi

  • Kujifungua kabla ya wakati

  • Kunyofoka kwa kondo la nyuma kabla ya wakati

  • Kubanwa kwa kitovu cha mtoto

  • Kujifungua kwa upasuaji

  • Maambukizi kwenye kizazi baada ya kujifungua


Dalili za kupasuka kwa chupa ya uzazi kabla ya wakati


Dalili za kupasuka kwa chupa ya uzazi kabla ya wakati ni;


  • Kumwagika au kuvuja kwa maji ya chupa ya uzazi ukeni

  • Kuloanisha nguo za ndani

  • Kuloanisha mapaja au magoti kwa maji ya chupa ya uzazi


Utambuzi wa chupa ya uzazi iliyopasuka kabla ya uchungu


Mbali na daktari kukuchukua historia ya kiasi na wakati maji yalipoanza kutoka utafanyiwa mambo yafuatayo ili kutambua kama maji yanayotoka ukeni ni maji ya chupa ya uzazi;


  • Uchunguzi wa shingo ya uzazi ili kuangalia maji kama yanatoka kupitia tundu la shingo ya uzazi

  • Kupima PH ya maji yanayotoka ndani ya kizazi

  • Uchunguzi wa maji yaliyokaushwa kwenye hadubini

  • Kipimo cha ultrasound kuangalia kiasi cha maji kilichopotea


Matibabu na kinga ya kupasuka kwa chupa ya uzazi


  • Matibabu Matibabu ya kupasuka kwa chupa ya uzazi kabla ya uchungu hutegemea vitu vifuatavyo;

  • Afya yako, ujauzito na mtoto tumboni

  • Ukubwa wa tatizo ( kiasi cha maji yaliyomwagika

  • Uvumilivu wa mwili wako kwenye dawa na tiba unayopatiwa

  • Matarajio ya matibabu

  • Uchaguzi wako


Matibabu huhusisha


Kulazwa

  • Matibabu ya kusubiria( inategemewa kwamba endapo chupa ya uzazi itapewa muda kwa mama kutulia kitandani, chupa hiyo inaweza kuziba yenyewe. Hata hivyo ni mara chache kwa chupa ya uzazi kujifunga yenyewe isipokuwa kama imetobolewa wakati wa kuchukua maji kwenye chupa ya uzazi au imetokea mwanzoni mwa ujauzito.

  • Uchunguzi wa viashiria vya uhai vya mtoto na mama. Mfano maumivu, mapigo ya moyo, joto la mwili n.k


Vipimo vya maabara


  • Matumizi ya dawa jamii ya corticosteroid ili kukomaza mapafu ya mtoto

  • Matumizi ya antibayotiki kuzuia maambukizi ndnai ya chupa ya uzazi

  • Dawa za kulegeza uzazi ili uchungu usitokee


Namna ya kukinga kupasuka kwa chupa ya uzazi kabla ya wakati


Hakuna njia ya moja kwa moja ya kujikinga na kupasuka kwa chupa ya uzazi kabla ya uchungu, hata hivyo tatizo kwa kuwa tatizo hili hutokea sana kwa wajawazito wanaovuta sigara na tumbaku, ni vema kuacha matumizi ya mazao haya kabla ya kuwa mjamzito na mapema zaidi wakati wa ujauzito.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

6 Oktoba 2021 16:05:29

Rejea za mada hii:

1. Natnael Etsay Assefa, et al. Risk factors of premature rupture of membranes in public hospitals at Mekele city, Tigray, a case control study. https://bmcpregnancychildbirth.biomedcentral.com/articles/10.1186/s12884-018-2016-6. Imechukuliwa 14.08.2021

2. Premature-rupture-membranes-prompreterm-premature-rupture-membranes-pprom . https://www.chop.edu/conditions-diseases/premature-rupture-membranes-prompreterm-premature-rupture-membranes-pprom. Imechukuliwa 14.08.2021

3. Premature Rupture of Membranes. https://emedicine.medscape.com/article/261137-overview. Imechukuliwa 14.08.2021

4. What to Expect When Your Water Breaks. https://www.webmd.com/baby/fluid-leakage. Imechukuliwa 14.08.2021

5. Nava Flores JEMM, et al. Maternal and fetal morbidity in patients with premature rupture of the membrane after 27-week gestation. Causes and Costs.

6. Wanda NKF, et al. Economic burden of hospitalizations for preterm labor in the United States. American College of obstetricians and Gynecologists. 2000;96(1):97–8. 6.

7. Sirak B, et al. Maternal and perinatal outcome of pregnancies with PROM at Tikur Anbesa specialized teaching hospital. Ehtiop Med J. 2014;(4):52.

bottom of page