Mwandishi:
Dkt. Mangwella S, MD
Mhariri:
Dkt. Lameck A, NS
Jumatano, 3 Novemba 2021
Kuyeyusha mawe kwenye njia ya mkojo
Matunda jamii ya citrus huzuia utengenezaji wa mawe kwenye njia ya mkojo kutokana na kuwa na utindikali pamoja na chumvi ya citrate. Citrus mbali na kuzuia utengenezaji wa mawe kwenye njia ya mkojo, huweza kumung’unya vijiwe vilivyokwisha tengenezwa. Matunda yenye faida kubwa zaidi kama ilivyoonekana kwenye tafiti ni chungwa na limau. (2006)
Matunda yasiyo jamii ya citrus yenye uwezo wa kutoa mawe kwenye njia ya mkojo mfano wake ni boga. Boga huwa na uwezo mkubwa wa kuzuia na kuyeyusha mawe ndani ya njia ya mkojo kutokana kuwa na potassium, citrate na malate kwa wingi.
Ili kupata mchanganyiko mzuri unaweza kuchanganya matunda na chakula hiki ili kutengeneza sharubati yenye faida nyingi.
Faida zingine za sharubati ya chungwa, limao na boga
Sharubati ya chungwa, limao na boga mbali na kuwa na uwezo wa kukinga na kuyeyusha mawe kwenye njia ya mkojo, huwa na faida zingine ambazo ni;
Husafisha damu
Huongeza utengenezaji wa mkojo
Huongeza hali ya ualikali kwenye damu
Huondoa sumu mwilini
Najifunza wapi namna ya kuandaa sharubati ya boga, limao na chungwa?
Jifunze namna ya kutengeneza sharubati hii, virutubisho unavyopata na faida zingine kwenye mada ya sharubati ya chungwa, limao na boga.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021 20:02:46
Rejea za mada hii:
1. Odvina CV. Comparative value of orange juice versus lemonade in reducing stone-forming risk. Clin J Am Soc Nephrol. 2006 Nov;1(6):1269-74. doi: 10.2215/CJN.00800306. Epub 2006 Aug 30. PMID: 17699358.
2. Baia Lda C, et al. Noncitrus alkaline fruit: a dietary alternative for the treatment of hypocitraturic stone formers. J Endourol. 2012 Sep;26(9):1221-6. doi: 10.1089/end.2012.0092. Epub 2012 Jun 4. PMID: 22500592.