top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Helen L, M.D

Jumatano, 27 Januari 2021

Lala muda wa kutosha, imarisha afya yako

Lala muda wa kutosha, imarisha afya yako

Kulala muda wa kutosha huongeza ufanisi wa mwili na akili, pia ni kinga ya magonjwa sugu kama kisukari aina ya 2, magonjwa ya moyo, uzito mkubwa kupita kiasi na sonona. Jali afya yako, lala masaa yanayoshauriwa kiafya kulingana na umri wako.


Faida za kulala muda wa kutosha


Kuna faida nyingi za kulala muda wa kutosha unaoshauriwa kulingana na umri wako. Tafiti nyingi zinaonyesha kwamba kulala muda wa kutosha wakati wa usiku;


 • Huamsha chembe za ulinzi wa mwili na 'antibodies' zinazopambana na maradhi mbalimbali ndani ya mwili wako

 • Huamsha kemikali mbalimbali za ulinzi mwilini zenye jina la 'cytokine' ambazo huzuia uvimbe unaosababishwa na kuamka kwa kinga za mwili pia huimarisha usingizi na kupambana na maradhi

 • Hupunguza kiwango cha homoni ya 'cortisol' inayochangia kwa kiasi kukubwa ongezeko la uzito mkubwa kupita kiasi na msongo.

 • Hupunguza upinzani wa mwili dhidi ya homoni inayorekebisha kiwango cha sukari kwenye damu yenye jina la 'insulin'

 • Huamsha homoni ya ukuaji yenye jina la 'growth hormone' inayosaidia kuponya majeraha na kurejesha seli mbalimbali zilizokufa

 • Hutuliza mfumo wa neva wa 'sympathetic' ili kushusha shinikizo la damu wakati umelala

 • Hufanya ubongo uweze kuchakata taarifa mbalimbali ulizozipokea muda mfupi kabla ya kulala na hivyo kukusababisha uwe na kumbukumbu nzuri


Endapo utalala muda wa kutosha wakati wa usiku, utaweza kujikinga na:

 • Magonjwa ya moyo kama shinikizo la juu la damu, kiharusi, magonjwa ya mishipa ya moyo na mapigo ya moyo kwenda isivyo kawaida

 • Uzito mkubwa kupita kaisi (ugonjwa wa obeziti)

 • Sonona

 • Kisukari aina ya 2


Ni masaa mangapi unatakiwa kulala kwa siku?


Kwa watu wazima wanatakiwa kulala angalau masaa 7 hadi 8 mfululizo wakati wa usiku

Vijana wa miaka 13 hadi 19 wanatakiwa kulala angalau masaa 9 hadi 10 mfululizo wakati wa usiku

Watoto wadogo chini ya miaka 13 wanatakiwa kulala masaa 10 au zaidi wakati wa usiku.


Kumbuka


Kulala zaidi ya muda unaoshauriwa huweza kuambatana na tatizo la kukosa usingizi, kupata usingizi usio bora na kushindwa kuanza au kuendelea kulala.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

19 Julai 2023 20:41:55

Rejea za mada hii:

1.K Spiegel, etal. Impact of sleep debt on metabolic and endocrine function https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/10543671/. Imechukuliwa 27.01.2021
2.Lorrie Magee, etal. Longitudinal associations between sleep duration and subsequent weight gain: A systematic review. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3202683/. Imechukuliwa 27.01.2021
3.Suzanne E Goldman, etal. Poor sleep is associated with poorer physical performance and greater functional limitations in older women. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/17969465/. Imechukuliwa 27.01.2021
4.A M Williamson, etal. Moderate sleep deprivation produces impairments in cognitive and motor performance equivalent to legally prescribed levels of alcohol intoxication. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/10984335/. Imechukuliwa 27.01.2021
5.Francesco P. Cappuccio, etal. Meta-Analysis of Short Sleep Duration and Obesity in Children and Adults. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC2398753/. Imechukuliwa 27.01.2021
6.CDC. Sleep and Chronic Disease. https://www.cdc.gov/sleep/about_sleep/chronic_disease.html. Imechukuliwa 27.01.2021
7.Kristen L Knutson, etal. Role of sleep duration and quality in the risk and severity of type 2 diabetes mellitus. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/16983057/. Imechukuliwa 27.01.2021
8.E Kasasbeh, etal. Inflammatory aspects of sleep apnea and their cardiovascular consequences. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/16466124/. Imechukuliwa 27.01.2021
9.James M Parish, etal. Obstructive sleep apnea and cardiovascular disease. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/15301332/. Imechukuliwa 27.01.2021
10.Daniel J Schwartz, etal. Symptoms of depression in individuals with obstructive sleep apnea may be amenable to treatment with continuous positive airway pressure. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/16162722/. Imechukuliwa 27.01.2021
11.S Taheri. The link between short sleep duration and obesity: we should recommend more sleep to prevent obesity. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC2082964/. Imechukuliwa 27.01.2021
12.James E Gangwisch, etal. Short sleep duration as a risk factor for hypertension: analyses of the first National Health and Nutrition Examination Survey. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/16585410/. Imechukuliwa 27.01.2021
13.How Sleep Helps Memory. https://www.psychologytoday.com/intl/blog/memory-medic/201103/how-sleep-helps-memory. Imechukuliwa 27.01.2021

bottom of page