Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD
Mhariri:
Dkt. Sospeter B, MD
Alhamisi, 16 Septemba 2021
Madini chuma kwa mjamzito
Wakati wa ujauzito, kiwango cha damu hupungua kiasi cha kuhatarisha maisha ya mama na mtoto. Licha ya msisitizo wa kutumia dawa yenye madini chuma ya ziada ili kuongeza damu, epuka kula vyakula vinavyopunguza ufyozwaji wake kama mayai, maziwa na mazao yake, nafaka zisizokobolewa na chai ya kahawa masaa mawili kabla ya kunywa dawa.
Ufyonzwaji wa madini chuma
Kiwango cha ufyonzwaji wa madini chuma kwa mtu mwenye afya kawaida hurandanana kiwango chamadini chuma mwilini. Kama mwili una upungufu wa madini chuma, kiwango cha ufyonzwaji huongezeka ili kuhakikisha kuwa mwili unapata kiasi cha kutosha. Magonjwa au chakula mbalimbali huathiri uwezo wa mfumo wa tumbo kufyonza madini chuma. Ni muhimu mjamzito akafahamu vyakula na magonjwa yanayoathiri ufyonzwaji wa madini chuma. Kidokezo kimezungumzia magonjwa na vyakula vinavyopunguza ufyonzwaji na nini ufanya ilikuongeza uvyozwaji wa madini haya. Kiwango cha damu chini ya 11 g/dL kipindi chochote cha ujauzito hufahamika kama upungufu wa damu.
Umuhimu wa madini chuma kwa mjamzito
Inafahamika kuwa, wakati wa ujauzitokiwango cha damu hupungua kiasi cha kuwezakuathiri afya ya mama na mtoto. Kiasi hiki hupungua kutokana na ongezeko la matumizi ya madini haya kati ya mama na mtoto, hii ndio maana mama mjamzito anasisitizwa kutumia madini chuma mara anapokuwa mjamzito. Kupata kiwango cha madini chuma ya kutosha takribani miligramu 200 kila siku, huupa mwili uwezo wa kutengeneza chembe nyekundu za damu na hivyo kuzuia madhara yanayoweza kutokea kwa mama na mtoto kama;
Kupatwa na uchungu kabla ya wakati
Kujifungua mtoto mwenye uzito kidogo (mtoto njiti)
Maambukizi ya via vya uzazi baada ya kujifungua
Dalili za upungufu wa damu kwa mjamzito
Uchovu
Udhaifu wamwili
Kupauka kwa ngozi au kuwa ya njano
Kuishiwa pumzi
Maumivu ya kifua
Mapigo ya moyo kwenda tofauti na kawaida
Maumivu ya kichwa
Kizunguzungu au hisia ya kutaka zimia
Miishio ya miguu na mikono kuwa yabaridi
Vyakula vinavyoongeza uzalishajiufyonzwaji wa madini chuma
Kula vyakula vifuatavyo huongeza uzalishaji wa madini chuma;
Nyama
Maharagwe ya soya
Vitamin C kutoka kwenye machungwa, maembe, limao n .k
Vyakula vilivyochachushwa
Vitamin A
Unaweza kutumia vyakula hivi wakati unakunywa dawa ili kuongeza ufyonzwaji wake
Vyakula vinavyopunguza ufyonzwaji wa madini chuma
Maziwa
Mazao yatokanayo na maziwa (maziwa mgando n.k)
Dawa zenye madini nyongeza ya calcium
Nafaka zisizokobolewa ( mkate , cereal,
Mimea jamii ya kunde
Karanga
Mbegu za vyakula na matunda
Chai ya kahawa
Matunda
Mboga za majani
Dawa za madini nyongeza ya zinc, manganese na zebaki
Je haupaswi kutumia vyakula hivi kabisa?
Hapana!
Vykula hivi vina umuhimu kwa mama mjamzito, inashauriwa vitumike masaa mawili kabla ya kunywa dawa au kunywa dawa masaa mawili baada ya kula vyakula hivi.
Magonjwa yanayopunguza uzalishaji wa madini chuma
Magonjwa ya michomo ya tumbo kama kolaitizi
Magonjwa ya kuharisha
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
6 Oktoba 2021 16:13:36
Rejea za mada hii:
Haemopoietic factors. Iron absorption. https://jcp.bmj.com/content/jclinpath/s3-5/1/55.full.pdf. Imechukuliwa 16/09/2021
A Short Review of Iron Metabolism and Pathophysiology of Iron Disorders. https://www.mdpi.com/2305-6320/6/3/85/pdf. Imechukuliwa 16/09/2021
Nancy C. Andrews. Iron Absorption. https://www.sciencedirect.com/topics/medicine-and-dentistry/iron-absorption. Imechukuliwa 16/09/2021
Dietary supplement fact sheet: Iron. National Institutes of Health. http://ods.od.nih.gov/factsheets/Iron-HealthProfessional/. Imechukuliwa 16/09/2021
Bauer KA. Hematologic changes during pregnancy. http://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 16/09/2021
American Society of Hematology. Anemia & pregnancy. http://www.hematology.org/Patients/Anemia/Pregnancy.aspx. Imechukuliwa 16/09/2021
National Heart, Lung, and Blood Institute. What is anemia?. https://www.nhlbi.nih.gov/health/health-topics/topics/anemia. Imechukuliwa 16/09/2021
American College of Obstetricians and Gynecologists (ACOG) Committee on Practice Bulletins — Obstetrics. ACOG Practice Bulletin No. 95: Anemia in pregnancy. Obstetrics & Gynecology. 2008;112:201. Reaffirmed 2015.
Abu-Ouf, et al. “The impact of maternal iron deficiency and iron deficiency anemia on child's health.” Saudi medical journal vol. 36,2 (2015): 146-9. doi:10.15537/smj.2015.2.10289
Anemia in Pregnancy. https://www.msdmanuals.com/professional/gynecology-and-obstetrics/pregnancy-complicated-by-disease/anemia-in-pregnancy. Imechukuliwa 16/09/2021