Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Charles W, M.D
Jumatano, 3 Machi 2021
Magonjwa 10 yanayoongoza kuua watu Tanzania
Magonjwa 10 yanayoongoza kuua watoto na watu wazima Tanzania ni Malaria, Magonjwa ya mfumo wa chini wa upumuaji, UKIMWI, Upungufu wa damu, Magonjwa ya moyo na misipa ya damu, Majeraha, Saratani, Kusambaa kwa sumu ya bakteria kwenye damu, Madhaifu ya kiuumbaji na Kiharusi. Chukua tahadhari, fahamu kuhusu magonjwa hayo, jifunze na jikinge endapo inawezekana.
Kutokana na tafiti ya afya kuangalia magonjwa yanayoongoza kuua watu kwenye hospitali za Tanzania, tafiti ya kuanzia mwaka 2006 hadi 2015 yenye jina la ‘Cause-specific mortality patterns among hospital deaths in Tanzania, 2006-2015’ ilofanywa na Leonard E. G. Mboera na wengine inaonyesha taarifa zinazofuata hapa chini
Magonjwa 10 yanayoongoza kuua watoto na watu wazima Tanzania
Malaria
Magonjwa ya mfumo wa upumuaji wa chini
Ukimwi HIV/AIDS
Upungufu wa damu
Magonjwa ya moyo na misipa ya damu
Ajali
Saratani
Kusambaa kwa sumu ya bakteria kwenye damu
Madhaifu ya kiuumbaji
Kiharusi
Magonjwa 10 yanayoongoza kuua watu wazima Tanzania
Malaria
HIV/AIDS
Magonjwa ya moyo na mishipa ya damu
Magonjwa ya mfumo wa upumuaji
Saratani
Upungufu wa damu
Majeraha
Kiharusi
Kifua kikuu
Kusambaa kwa sumu ya bakteria kwenye damu
Magonjwa 10 yanayoongoza kuua watoto Tanzania
Malaria
Magonjwa ya mfumo wa upumuaji
Magonjwa ya madhaifu ya watoto
Upungufu wa damu
Magonjwa kutokana na kujifungua kabla ya wakato
Kusambaa kwa sumu ya bakteria kwenye damu
Madhaifu ya upumuaji kutokana na kuzaliwa kabla ya mapafu kukomaa
Matatizo wakati wa kujifungua
Utapiamlo
Matatizo ya mama au mtoto wakati wa ujauzito
Kumbuka
Baadhi ya magonjwa yanayoongoza kuua watu yanaweza kuzuilika. ULY CLINIC Inakushauri upende kufahamu kuhusu magonjwa hayo na namna ya kuchukua hatua za kujikinga. Soma zaidi kuhusu magonjwa hayo kwenye makala zilizopo ndani ya tovuti hii.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
19 Julai 2023 20:41:21
Rejea za mada hii:
1. Leonard E. G. Mboera et al. Cause-specific mortality patterns among hospital deaths in Tanzania, 2006-2015. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC6209209/#. Imechukuliwa 03.03.2021
2. CDC Impact in Tanzania. https://www.cdc.gov/globalhealth/countries/tanzania/default.htm. Imechukuliwa 03.03.2021