top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Helen L, M.D

Jumanne, 26 Januari 2021

Maji ya bamia huchochea uponyaji wa vidonda vya tumbo

Maji ya bamia huchochea uponyaji wa vidonda vya tumbo

Ukuta wa ndani ya tumbo kwa kawaida umefunikwa kwa ute ute wa mlenda unaozuia kuta za chini zisiunguzwe na tindikali zinazozalishwa tumboni. Kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo, ute huu huwa dhaifu na udhaifu husambaa eneo kubwa zaidi. Matumizi ya maji ya bamia hurejesha kuta hii na kuharakisha uponyaji utokee.


Maji ya bamia yanasaidia vipi?


Maji ya bamia yana ute kwa wingi, ute huu unapoingia tumboni hufunika kuta ya juu ya tumbo na kuleta ulinzi dhidi ya kuunguzwa na tindikali. Kwa kufanya hivyo husaidia kutoendelea kwa tatizo la vidonda na pia kuharakisha uponyaji utokee.


Jinsi ya kuandaa maji ya bamia kwa ajili ya vidonda vya tumbo;

  • Chukua bamia zako tano, zisafishe kwa maji safi kisha kata vipande vidogo vidogo

  • Loweka vipande hivyo kwenye kikombe cha chai chenye maji ya baridi

  • Subiria kwa muda wa masaa 12, kabla ya kunywa maji hayo

  • Kunywa maji hayo kila siku asubuhi kwa muda wa wiki nne au zaidi


Njia nyingine unaweza kutumia bamia


Kuitumia kama mboga, hata hivyo, matumizi ya namna hii huwa hayana matokeo mazuri kama ilivyo kutumia maji ya bamia

Kwa kutafuna bamia mbichi au iliyochemshwa


Kumbuka


Maji ya bamia huwa hayatibu vidonda vya tumbo, bali huchochea kutokea kwa uponyaji. Kabla ya kutumia njia hii ni lazima uwe umefanya vipimo ili kutambua tatizo lako la vidonda limesababishwa na nini. Baada ya kufahamu unatakiwa kupewa tiba inayotakiwa, mfano endapo ni maambukizi ya H.Pyroli, utapewa dawa za kutibu maambukizi hayo. Baada ya kupata matibabu yanayotakiwa, ongeza na matumizi ya maji ya bamia kuharakisha uponyaji kutokea.


Faida zingine za maji ya bamia


Ni kinga ya vidonda vya tumbo kutokana na kuunguzwa na tindikali. Watumiaji wa vinywaji vikali kama mvinyo na pombe ya kawaida wanapaswa kutumia njia hii ili kujikinga na vidonda vya tumbo. Watu wengine pia wanaweza kutumia njia hii kujikinga na vidonda vya tumbo.


Maji ya bamia pia huwa na faida nyingine nyingi kama kushusha shinikizo la juu la damu na kiwango cha sukari kwa watu wenye tatizo la kisukari. Soma zaidi kuhusu bamia katika makala zingine ndani ya tovuti hii.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

19 Julai 2023 20:41:55

Rejea za mada hii:

1.Deniz Ortaç etal. In vivo anti-ulcerogenic effect of okra (Abelmoschus esculentus) on ethanol-induced acute gastric mucosal lesions. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/29513129/. Imechukuliwa 26.01.2021

2.Danial Esmaeilzadeh, etal. Effect of Abelmoschus esculentus (okra) on metabolic syndrome: A review. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/32222004/. Imechukuliwa 26.01.2021

3.Christian Lengsfeld, etal. Glycosylated Compounds from Okra Inhibit Adhesion of Helicobacter pylori to Human Gastric Mucosa. https://www.researchgate.net/publication/8671513_Glycosylated_Compounds_from_Okra_Inhibit_Adhesion_of_Helicobacter_pylori_to_Human_Gastric_Mucosa. Imechukuliwa 26.01.2021

bottom of page