Mwandishi:
Dkt. Sara H, MD
Mhariri:
Dkt. Mangwella S, MD
Jumatano, 20 Oktoba 2021
Maji ya mwanamke aliyekojozwa
Mkojo unaotoka kwa mwanamke aliyekojozwa huwa mweupe kama maziwa, mtamu, usio na harufu ya mkojo na ujazo wa kijiko kimoja cha chai. Maji yasiyofanana na hayo si maji ya kukojozwa bali ni mkojo wa kawaida tu.
Maji ya kukojozwa hutokea wapi?
Maji ya kukojozwa huzalishwa kwenye tezi ndogo inayofana na tezi dume, tezi hii inaitwa tezi jike au prostate ya kike.
Sifa za maji ya kukojozwa
Maji yanayotolewa na mwanamke aliyekojozwa wakati wa kujamiana huwa na sifa zifuatazo;
Meeupe kama maziwa yasiyo na mafuta
Yana ladha tamu
Hayana harufu ya mkojo
Vipimo vya maji hayo vimethibitisha kuwa maji haya huwa na muundo wa kikemikali ulio tofauti kabsia na mkojo.
Vilivyomo kwenye maji ya kukojozwa
Maji ya mwanamke aliyekojozwa umetengenezwa na;
Prostatic acid phosphatase
Prostatic specific antigen
Glucose
Fructose
Kiasi kidogo cha urea na creatinine
Mkojo wa mwanamke asiyeugua
Mkojo wa mwanamke mweye afya njema umetengenezwa na;
Kiasi kikubwa cha urea
Kiasi kikubwa cha creatinine
Mkojo wa mwanamke mwenye kisukari huwa na glucose na huwa mtamu pia lakini mkojo huo si wa kukojozwa bali unatokana na ugonjwa.
Kukojozwa hutokeaje?
Kukojozwa kwa mwanamke hutokea kama atapata msisimuko mkali kwenye eneo G na hutokea mara nyingi wakati wa kufika kileleni na wanawake wachache hukojoa wakati wa kusisimuliwa kingono.
Tafiti zinaonyesha wanawake wenye misuli imara ya sakafu ya nyongo hukojoa kirahisi kuliko wenye misuli dhaifu, kufanya mazoezi ya kegel huweza kuimarisha misuli ya sakafu ya nyonga.
Wanawake waliokojozwa walilipoti pia kuwa wana eneo lenye hisia nyingi maeneo karibia na nje ya uke. Kusisimuliwa kwa maeneo hayo kulisababisha kutokwa na maji kutoka kwenye njia ya mkojo na kwa baadhi ya wanawake walipata mshindo wa kufika kileleni ulio tofauti na kufika kileleni kwa kusisimuliwa kinembe.
Wanawake walilipoti pia kuwa hisia za kufika kileleni kwa kukojozwa huhisiwa via vilivyo ndani zaidi ya mwili na huleta utamu mubwa sana unaoambatana na kusukumwa kwa kizazi kuelekea kwenye uke na si kuvutwa ndani kwa kizazi na kutanuka kwa uke kama ilivyoripotiwa kwa wanawake waliofika kileleni kutokana na kusisimuliwa kinembe.
Mkia wa eneo G unapatikana milimita 3 kutoka kwenye mpaka wa pembeni wakati kichwa chake hupatikana milimita 15 kutoka kwenye mpaka wa pembeni wa mrija wa mkojo.
Maelezo zaidi kwenye picha
Eneo G lipo wapi?
Eneo G kwa mwanamke hupatikana sehemu ya juu ya ukuta wa periniamu, milimita 16.5 kutoka sehemu ya juu ya tundu la mkojo na hutengeneza pembe ya nyuzi za 35 na mpaka wa pembeni wa mrija wa mkojo.
Eneo G pia huelezewa kupatikana sentimita 5 hadi 8 kutoka nje ya tundu la uke. Maelezo zaidi yanapatikana kwenye picha hapa chini.
Hitimisho
Ni vema mtu na mpenzi wake wakatambua kuwa, mwanamke kutoa mkojo wa kukojozwa ni kawaida na huwa si udhaifu au kitu cha kuhofiwa. Hata hivyo haitakiwi kuwa lengo la kwanza la kufanya ngono kwa kuwa hisia za utamu wat endo zinaweza kupotea endapo hali hii haitatokea.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
20 Oktoba 2021 18:31:52
Rejea za mada hii:
1. Addiego, F., et al. 1981. Female Ejaculation: A Case Study. The Journal of Sex Research, 17: 13– 21
2. Belzer, E. G., et al. 1984. On Female Ejaculation. The Journal of Sex Research, 20: 403– 406.
3. Cabello, F. 1997. Female Ejaculation: Myths and Reality, pp. 1–8. In J. J. Borras-Vall and M. Perez-Conchillo, eds., Sexuality and Human Rights. Valencia: Nau Llibres.
4. De Graff, R. 1672. New Treatise Concerning the Generative Organs of Women. Journal of Reproduction and Fertility, 17: 77– 232, edited by H. D. Jocelyn and B. P. Setchell. Oxford: Blackwell Scientific Publications, 1972.
5. Perry, J. D., et al. 1981. Pelvic Muscle Strength of Ejaculators: Evidence in Support of a New Theory of Orgasm. The Journal of Sex Research, 17: 22– 39.
6. Sevely, et al. 1978. Concerning Female Ejaculation and the Female Prostate. The Journal of Sex Research, 14: 1– 20.
7. Ostrzenski A. G-spot anatomy: a new discovery. J Sex Med. 2012 May;9(5):1355-9. doi: 10.1111/j.1743-6109.2012.02668.x. PMID: 22781083.