top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Sospeter L, MD

Jumatatu, 6 Septemba 2021

Majibu chanya ya VVU pasipo VVU

Majibu chanya ya VVU pasipo VVU

Majibu chanya ya kipimo cha HIV SD bioline licha ya kushuku maambukizi ya VVU, huweza kuwa chanya kwa mwenye kaswende, kichocho, minyoo, shambulio binafsi la kinga, ujauzito n.k. Majibu chanya yanapaswa kuthibitishwa kwa kipimo cha HIV Uni-Gold au vingine vyenye ufanisi zaidi.


Inawezekana kuwa na majibu chanya ya VVU wakati huna VVU?


Ndio unawezekana kuwa na majibu chanya( positive) kwa kipimo cha SD bioline wakati huna maambukizi hayo


Majibu chanya ya kipimo cha HIV SD bioline huweza kuwa chanya kwenye baadhi ya maambukizi ya virusi, bakteria, minyoo na baadhi ya hali kama ujauzito n.k


Magonjwa yanayoweza kuleta majibu chanya wakati huna VVU


Kuna magonjwa mbalimbali yanaweza kupelekea kupata majibu chanya ya VVU wakati huna VVU ambayo ni;


 • Maambukizi ya kirusi cha Epstein-Barr

 • Kiasi kibubwa cha bilirubin kwenye damu

 • Magonjwa shambulio bonafsi la mfumo wa kinga

 • Ugonjwa wa kaswende

 • Ugonjwa wa lupus

 • Ugonjwa wa lyme

 • Ugonjwa wa kichocho kutokana na kimelea schitosoma mansoni


Hali zinazoweza pelekea kupata majibu chanya wakati huna VVU


Hali zifuatazo zinaweza kupelekea kupata majibu chanya wakati huna maambukizi ya VVU;


 • Kuchanganya sampuli

 • Kusoma vibaya majibu ya kipimo ( mfano kusoma baada ya muda unaotakiwa)

 • Ujauzito

 • Kuchoma chanjo ya virusi mfano chanjo ya kirusi cha influenza

 • Kuchoma chanjo ya VVU

 • Kuamshwa kwa chembe B na CD5 za mfumo wa kinga ya mwili kuitikia maambukizi ya malaria


Vipimo vya kuthibitisha uwepo wa maambukizi wa VVU


Vipimo vya kuthibitisha uwepo wa maambukizi wa VVU ni


 • Kipimo cha HIV culture

 • Kipimo cha Western Blot (kilikuwa kinatumika sana zamani)

 • Neutralization Test

 • NAT

 • Kipimo cha HIV antijen Test


Je Kipimo cha HIV Uni-Gold hutosha kuthibitisha majibu chanya ya HIV


Kipimo cha Uni- Gold hupima antibodi zinazozalishwa na mwili dhibi ya kirusi, licha ya kuwa na ufanisi wa asilimia 98.8 kinaweza kutotoa majibu ya ukweli kwa baadhi ya nyakati hivyo vipimo vilivyoandikwa hapo juu ni vipimo vya kuthibitisha uhalari wa majibu chanya. Kwa sababu kwa nchi nyingi zinazoendelea hakuna uwezo wa kufanya vipimo hivyo kutokana na gharama, kipimo cha Uni-Gold hutosha kutoa majibu ya uthibitisho kwamba una mambukizi ya VVU baada ya kuwa na majibu chanya kwenye kipimo cha HIV SD bioline.


Ushauri kwako


Mara baada ya kujipima nyumbani au kupimwa hospitali na kujikuta kuwa na maambukizi ya VVU, unapswa kwenda hospitali kwa ajili ya uthibitisho wa majibu hayo kwa vipimo vingine muhimu kama HIV Uni-Gold au Culture pamoja na western blot.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

6 Oktoba 2021 16:17:37

Rejea za mada hii:

Sharon Coleman, et al. False-positive HIV diagnoses: lessons from Ugandan and Russian research cohorts. https://www.researchgate.net/publication/322844920_False-positive_HIV_diagnoses_lessons_from_Ugandan_and_Russian_research_cohorts. Imechukuliwa 06.09.2021

Derryck Klarkowski, et al. Causes of false-positive HIV rapid diagnostic test results. https://www.tandfonline.com/doi/abs/10.1586/14787210.2014.866516?journalCode=ierz20. Imechukuliwa 06.09.2021

UCSF Health. HIV Diagnosis. https://www.ucsfhealth.org/conditions/hiv/diagnosis#. Imechukuliwa 06.09.2021

HIV Testing. https://www.cdc.gov/hiv/testing/index.html. Imechukuliwa 06.09.2021

Xiaojie Huang, et al. Evaluation of Blood-Based Antibody Rapid Testing for HIV Early Therapy: A Meta-Analysis of the Evidence. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC6036269/. Imechukuliwa 06.09.2021

Western Blot Test. https://stanfordhealthcare.org/medical-conditions/sexual-and-reproductive-health/hiv-aids/diagnosis/western-blot-test.html#. Imechukuliwa 06.09.2021

Interpretation and Use of the Western Blot Assay for Serodiagnosis of Human Immunodeficiency Virus Type 1 Infections. https://www.cdc.gov/mmwr/preview/mmwrhtml/00001431.htm. Imechukuliwa 06.09.2021

Jin-Sook Wang, et al Effect of a confirmatory testing algorithm on early acute HIV diagnosis in Korea. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC8084021/. Imechukuliwa 06.09.2021

How accurate are rapid, point-of-care tests for HIV?. https://www.aidsmap.com/about-hiv/how-accurate-are-rapid-point-care-tests-hiv. Imechukuliwa 06.09.2021

WHO Prequalification of In Vitro Diagnostics Programme. PUBLIC REPORT. Product: Uni-Gold™ HIV
Number: PQDx 0149-052-00. https://www.who.int/diagnostics_laboratory/evaluations/pq-list/hiv-rdts/170726_amended_final_pqpr_0149_052_00_v5.pdf. Imechukuliwa 06.09.2021

bottom of page