Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
Jumapili, 8 Agosti 2021
Mara ngapi utumie dawa ya minyoo?
Watoto wenye umri wa miezi 12 au zaidi na watu wazima wanaoishi mikoa yenye hali ya juu ya maambukizi ya minyoo wanashauriwa kunywa albendazole au mebendazole kama kinga mara moja hadi mbili katika mwaka.
Minyoo inaambukizwaje?
Katika historia,minyoo ilishaambukiza zaidi ya nusu ya watu duniani na ulikuwa ni moja ya ugonjwa usiotiliwa umaanani kwa sababu kuu kwamba hauui na hauna madhara makubwa. Hata hivyo kutokana na ongezeko la maambukizi hayo kuwa juu na kuonekana kwa madhara, wataalamu wa kinga wametilia umaanani ugonjwa huu na kuweka mikakati ya kukinga na kutibu. Ugunduzi wa dawa za minyoo miaka ya 1980 ambazo zilikuwa zinatumika kutibu minyoo kwa wanyama, zilifungua njia ya kupambana na ugonjwa huu.
Minyoo huambukizwa kwa njia mbalimbali kama vile kula udongo ambapo mtu atapata minyoo ndoano, minyoo mviringo na mnyoo mjeredi.
Minyoo pia inaweza kuambukizwa kwa njia ya kula chakula kilichochanganyika na kinyesi katika maeneo ambayo utunzaji wa kinyesi ni mbovu. Mfano wa minyoo hiyo ni Ascariasis, minyoo ndoano, naTrichuriasis
Vihatarishi vya kupata minyoo
Vihatarishi vya kupata minyoo ni;
Kula chakula kibichi
Kula chakula ambacho hakijaoshwa na maji safi
Kula matunda au mboga za majani zilichoandaliwa bila kuzingatia usafi
Kunywa maji au vinywaji vyenye vimelea wa minyoo
Kuandaliwa chakula na mtu asiyezingatia usafi wa mwili ( mfano kutonawa mikono baada ya kutoka chooni)
Mikoa yenye hali ya juu ya maambukizi ya minyoo
Maeneo yenye maambukizi makubwa ya minyoo Tanzania
Mwanza
Dodoma
Mbeya
Pemba
Unguja
Morogoro
Dar es salaam
Manyara
Kilimanjaro
Dawa za kukinga ya maambukizi ya minyoo
Dawa za kukinga na maambukizi ya minyoo zinazotumika ni albendazole au mebendazole, dawa hizi hazitumiki kwa ujauzito chini ya wiki 13 na kwa watoto chini ya miezi 12 isipokuwa umeshauriwa na daktari wako. Dozi ya minyoo kwa watoto chini ya miezi 24 ni sawa na nusu ya ile anayopata mtu mzima. Makundi maalumu ya dozi kinga ya minyoo yameorodheshwa hapa chini.
Kinga ya minyoo kwa watoto
Dozi ya kukinga minyoo kwa watoto inaweza kutumika mara moja au mbili kwa mwaka
Dozi itatumika mara moja kama kinga kama hali ya maambikizi ni asilimia 20 au zaidi
Dozi inashauriwa kutumika mara mbili kwa mwaka kama kinga endapo hali ya maambukizi ni asilimia 50 au zaidi
Dozi ya kinga ya minyoo kwa watu wazima
Dozi ya minyoo kwa watu wazima inashauriwa kutumika mara moja kwa mwaka kama kinga ya minyoo ikiwa hali ya maambukizi ni zaidi ya asilimia 20
Dawa za minyoo zitumike mara mbili kwa mwaka kama kinga ya minyoo kwa watu wazima kama hali ya maambukizi katika eneo hilo ni zaidi ya asilimia 50
Kinga ya minyoo kwa mjamzito
Dozi kinga ya minyoo kwa mjamzito inashauriwa kutumika mara moja kwa mwaka kama hali ya maambukizi ni zaidi ya asilimia 20 na kama kuna ugonjwa wa kuishiwa damu kutokana na minyoo kwa zaidi ya asilimia 40 ya wajawazito.
Dawa ya minyoo itumike mara mbili kwa mwaka kama kinga ya minyoo kwa mjamzito endapo hali ya maambukizi katika eneo hilo ni zaidi ya asilimia 50
Njia za kujikinga na minyoo pasipo dawa
Baadhi ya njia za kupunguza maambukizi ya minyoo ni;
Kusafisha kwa maji safi matunda na mboga za majani kabla ya kula
Kuwa na tabia ya kukata kucha na kuzisafisha mara kwa mara
Fanya usafi wa choo na matandiko kila siku( badilisha matandiko yako kila siku)
Jenga tabia ya kunawa mikono kwa sabuni na maji safi baada ya kutoka chooni na kabla au baada ya kula chakula
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
6 Oktoba 2021 16:18:43
Rejea za mada hii:
1. Preventive chemotherapy to control soil-transmitted helminth infections in at-risk population groups. Geneva: World Health Organization; 2017 (http://www.who.int/elena/titles/full_recommendations/deworming/en/). Imechukuliwa 08.08.2021
2. Tanzania General Health Risks: Soil-Transmitted Helminths. https://www.iamat.org/country/tanzania/risk/intestinal-parasites-soil-transmitted-helminths. Imechukuliwa 08.08.2021
3. Azan A. Nyundo, et al. Prevalence and Correlates of Intestinal Parasites among Patients Admitted to Mirembe National Mental Health Hospital, Dodoma, Tanzania. https://www.hindawi.com/journals/jpr/2017/5651717/. Imechukuliwa 08.08.2021
4. Albonico M, et al. Controlling soil transmitted helminthiasis in pre school age children through preventive chemotherapy. PLoS Negl Trop Dis. 2008;2:e126.
5. Brooker S, et al. Global epidemiology, ecology and control of soil-transmitted helminth infections. Adv Parasitol. 2006;62:221–61.
6. Hotez PJ, et al. Control of neglected tropical diseases. N Engl J Med. 2007;357:1018–27.
7. Hotez PJ, et al. Current concepts: hookworm infection. N Engl J Med. 2004;351:799–807.
8. Hotez PJ, et al. Rescuing the bottom billion through control of neglected tropical diseases. Lancet. 2009;373:1570–5.
9. Markus MB, etal. Helminthiasis and HIV vaccine efficacy. Lancet. 2001;357:1799.
10. Ross AGP, et al. Schistosomiasis: a clinical perspective. N Engl J Med. 2002;346(16):1212–20. 2002.
11. World Health Organization. Preventive Chemotherapy in Human Helminthiasis: Coordinated Use of Anthelminthic Drugs in Control Interventions: A Manuel for Health Professionals and Programme Managers. Geneva: World Health Organization Press; 2006.
12.H.D. MAZIGO, et al. Prevalence of intestinal parasitic infections among patients attending Bugando Medical Centre in Mwanza, north‐western Tanzania: a retrospective study . http://www.bioline.org.br/pdf?th10023. Imechukuliwa 08.08.2021
13. Helene Riess, et al. Hookworm Infection and Environmental Factors in Mbeya Region, Tanzania: A Cross-Sectional, Population-Based Study. https://journals.plos.org/plosntds/article?id=10.1371/journal.pntd.0002408. Imechukuliwa 08.08.2021
14. Massa K, et al. The combined effect of the Lymphatic Filariasis Elimination Programme and the Schistosomiasis and Soil-transmitted Helminthiasis Control Programme on soil-transmitted helminthiasis in schoolchildren in Tanzania. Trans R Soc Trop Med Hyg. 2009, 103: 25-30. 10.1016/j.trstmh.2008.07.011. Imechukuliwa 08.08.2021