Mwandishi:
Dkt. Mangwella S, MD
Mhariri:
Dkt. Benjamin L, MD
Jumamosi, 21 Agosti 2021
Matibabu ya dalili Kiasi za UVIKO-19
Homa, kikohozi kikavu, koo chungu na maumivu ya misuli ni miongoni mwa dalili kiasi za UVIKO-19 zinazoweza kutibiwa kwa kumeza Panado na Azithromycin kwa siku tano na Aspirin+ vitamin C + vitamin D + Zinc kwa muda wa siku 14. Usitumie dawa hizi pasipo ushauri wa daktari wako ili kuepuka madhara.
UVIKO-19
UVIKO-19 au COVID-19 ni ugonjwa unaosababishwa na maambukizi ya kirusi cha sindromu kali ya kifua mwenyejina lenye kifupisho cha SARS-CoV-2.
Dalili za UVIKO-19
Dalili kiasi zinazotokea mara nyingi ni;
Homa
Kikohozi kikavu
Uchovu
Dalili za wastani na kali za UVIKO-19
Dalili za wastani zinazotokea kwa nadra ni;
Maumivu ya misuli
Maumivu ya kichwa
Koo chungu
Kuharisha
Michomo kinga kwenye macho
Kupoteza uwezo wa kunusa
Kupotea uwezo wa kutambua ladha ya chakula
Kupatwa na harara kwenye ngozi
Kubadilika rangi kwa vidole vya mikono na miguu
Dalili kali za UVIKO-19
Dalili kali za UVIKO-19 ni;
Kupumua kwa shida
Kuishiwa pumzi
Maumivu ya kifua
Kifua kubana
Kushindwa kuongea
Kushindwa kutembea
Matibabu ya dalili za kiasi za UVIKO-19
Dalili kiasi za UVIKO-19 kwa mtu mzima Tanzania hutibiwa na dawa zifuatazo;
Paracetamol 1gm PO, OD kwa siku 5
Azithromycin 500 PO, OD kwa siku 5
Aspirin 75mg PO, OD kwa siku 14
Vitamin C 1000mg PO, OD kwa siku 14
VItamin D 5000IU PO, OD kwa siku 14
Zinc 40mg PO, OD kwa siku 14
Dawa mbadala
Dawa mbadala wa Azithromycin ni Ivermectin 12mg PO, OD kwa siku 5 au colchicine 500mcg PO, OD kwa siku 5
Dawa mbadala wa Aspirin ni Clopidrogrel 75md PO OD kwa siku 14
Kumbuka
Hupaswi kutumia dawa yoyote le pasipo kupewa ushauri wa daktari, matumizi ya dawa hizi ni kwa hatari yako mwenyewe
Dozi iliyoandikwa hapa si kwa ajili ya watoto chini ya umri wa miaka 18
Tahadhari kwa matumizi ya dawa za dalili kiasi za UVIKO-19
Wagonjwa wanaopaswa kuwa makini dhidi ya matumizi ya dawa zilizoorodheshwa hapo juu ni ;
Wagonjwa wenye matatizo ya damu kuganda
Wagonjwa wenye magonjwa sugu ya Ini na figo
Wagonjwa wenye mzio na dawa zilizoorodheshwa hapo juu
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
6 Oktoba 2021 19:03:33
Rejea za mada hii:
1. Coronavirus disease 2019: Resources. American Academy of Otolaryngology—Head and Neck Surgery. https://www.entnet.org/content/coronavirus-disease-2019-resources. Imechukuliwa 16.08.2020
2. McIntosh K. Coronavirus disease 2019 (COVID-19): Epidemiology, virology, clinical features, diagnosis, and prevention. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 16.08.2020
3. Coronavirus disease 2019 (COVID-19) treatment guidelines. National Institutes of Health. https://covid19treatmentguidelines.nih.gov/introduction/. Imechukuliwa 18.08.2021
4. Emergency use authorization. U.S. Food & Drug Administration. https://www.fda.gov/emergency-preparedness-and-response/mcm-legal-regulatory-and-policy-framework/emergency-use-authorization#coviddrugs. Imechukuliwa 16.08.2020
5. Coronavirus (COVID-19) update: FDA authorizes first standalone at-home sample collection kit that can be used with certain authorized tests. U.S. Food & Drug Administration. https://www.fda.gov/news-events/press-announcements/coronavirus-covid-19-update-fda-authorizes-first-standalone-home-sample-collection-kit-can-be-used. Imechukuliwa 16.08.2020
6. Coronavirus (COVID-19) update: FDA authorizes first diagnostic test using at-home collection of saliva specimens. U.S. Food & Drug Administration. https://www.fda.gov/news-events/press-announcements/coronavirus-covid-19-update-fda-authorizes-first-diagnostic-test-using-home-collection-saliva. Imechukuliwa 16.08.2020
7. Interim guidelines for collecting, handling, and testing clinical specimens for COVID-19. Centers for Disease Control and Prevention. https://www.cdc.gov/coronavirus/2019-nCoV/lab/guidelines-clinical-specimens.html. Imechukuliwa 16.08.2021
8. Speth MM, et al. Olfactory dysfunction and sinonasal symptomatology in COVID-19: Prevalence, severity, timing, and associated characteristics. Otolaryngology-Head and Neck Surgery. 2020; doi:10.1177/0194599820929185.
9. Marshall WM (expert opinion). Mayo Clinic. Accessed Nov. 23, 2020.Vaccines and related biological products advisory committee meeting. U.S. Food and Drug Administration. https://www.fda.gov/media/144245/download. Imechukuliwa 16.08.2021
10. Science Brief: SARS-CoV-2 and surface (fomite) transmission for indoor community environments. Centers for Disease Control and Prevention. https://www.cdc.gov/coronavirus/2019-ncov/more/science-and-research/surface-transmission.html. Imechukuliwa 16.08.2021
11. Interim public health recommendations for fully vaccinated people. Centers for Disease Control and Prevention. https://www.cdc.gov/coronavirus/2019-ncov/vaccines/fully-vaccinated-guidance.html. Imechukuliwa 16.08.2021
12. Coronavirus (COVID-19) update: FDA authorizes additional vaccine dose for certain immunocompromised individuals. U.S. Food and Drug Administration. https://www.fda.gov/news-events/press-announcements/coronavirus-covid-19-update-fda-authorizes-additional-vaccine-dose-certain-immunocompromised. Imechukuliwa 16.08.2021
13. Talking with patients who are immunocompromised. Centers for Disease Control and Prevention. https://www.cdc.gov/vaccines/covid-19/clinical-considerations/immunocompromised-patients.html. Imechukuliwa 16.08.2021
16. KCMC. COvid-19 management guideline 2021
17. Tanzanian COVID-19 management guideline by MoHCDGEC