top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Benjamin L, MD

Jumanne, 20 Julai 2021

Matumizi sahihi ya dawa

Matumizi sahihi ya dawa

Matumizi sahihi ya dawa hujumuisha mgonjwa kupokea dawa sahihi kulingana na mahitaji yake ya kiafya, katika dozi sahihi, muda sahihi wa matibabu na kwa bei anayoweza kumudu. Epuka madhara na gharama kwa kuzingatia matumizi sahihi ya dawa.


Matumizi sahihi ya Dawa ni nini?


Ili matibabu yafanikiwe, ni lazima mtoa dawa na mtumiaji waweze kupeana maelekezo sahihi ya matumizi ya dawa. Kutumia dawa sahihi kwa usahihi, hupunguza madhara ya dawa na gharama kwa mgonjwa.


Matumizi sahihi ya dawa hujumuisha mgonjwa kupokea dawa sahihi kulingana na mahitaji yake ya kiafya, katika dozi sahihi, muda sahihi wa matibabu na kwa bei anayoweza kumudu. Ishara za matumizi sahihi ya dawa ni;


 • Kutumia dozi sahihi

 • Kumaliza kozi

 • Kutumia dawa sahihi katika kutibu ugonjwa

 • Kutumia dawa kwa njia sahihi

 • Kununua na kutumia dawa baada tu ya kufanyiwa uchunguzi

 • Kutumia dawa yenye kiwango cha ubora

 • Kutumia dawa zisizoingiliana kiutendaji

 • Kutumia viuajisumu( antibayotiki) kutibu magonjwa yanayotokana na bakteria

 • Kutumia dawa za viuajivirusi kutibu magonjwa yanayotokana na virusi

 • Kutumia dawa bila pombe au vyakula vyenye muingiliano na dawa

 • Kutumia dawa zinazoruhusiwa wakati wa ujauzito


Sababu zinazochangia matumizi yasiyo sahihi ya dawa


Kuna sababu mbalimbali zinazoweza kuchangia matumizi sahihi ya dawa ambazo ni;


 • Kugundua ugonjwa

 • Uandikaji sahihi wa dawa

 • Utoaji sahihi wa dawa

 • Kumudu gharama za dawa

 • Mgonjwa kutumia dawa kwa usahihi

 • Mgonjwa kutumia dawa baada ya kupata ushauri wa daktari


Faida za matumizi sahihi ya dawa


 • Kuboresha afya ya mtumiaji wa dawa

 • Kutimiza Lengo sahihi la matumizi ya dawa husika

 • Kupunguza uwezekano wa kujenga usugu wa vimelea vya magonjwa


Kupunguza madhara/Maudhi ya dawa


 • Kupunguza gharama zisizo za lazima kwa mgonjwa na Serikali

 • Kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa yatokanayo na utumiaji sugu wa dawa

 • Jamii kuwa na Imani na dawa pamoja na mifumo ya kutolea huduma za afya


Athari zitokanazo na matumizi yasiyo sahihi ya dawa


Mgonjwa asipotumia dawa kwa usahihi yafuatayo yanaweza kutokea;


 • Mgonjwa hatapata tiba sahihi na hivyo kuendelea kuugua au kufa

 • Uwezekano wa kupata madhara ya dawa


Wajibu wa Mtoa Dawa na mgonjwa katika kuchangia matumizi sahihi ya dawa


Ili kuhakikisha dawa zinatumika kwa usahihi, Mtoa Dawa na mgonjwa wanapaswa;


 • Kugundua kwa usahihi dalili za ugonjwa na kufanya uchunguzi kabla ya kutumia dawa

 • Kutoa rufaa kwa mgonjwa kwenda ngazi inayohusika kulingana na mahitaji ya kiafya

 • Kumpa na kutumia dawa sahihi kulingana na cheti cha daktari au maelezo ya mgonjwa (dawa inatakiwa kuandikwa na daktari kabla ya kutumia)

 • Kutoa na kupokea maelekezo juu ya matumizi na uhifadhi sahihi wa dawa.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

6 Oktoba 2021 19:05:35

Rejea za mada hii:

1. World Health Organization. The rational use of drugs. Report of the conference of experts. Geneva: World Health Organization; 1985. http://www.apps.who.int/medicinedocs/en/m/abstract/Js17054e/. Imechukuliwa 20.07.2021

2. Holloway K, et al. Rational Use of Medicines. World Medicines Situation Report. World Health Organization; 2011. Report No. WHO/EMP/MIE/2011.2.2. from: http://www.who.int/medicines/areas/policy/world_medicines_situation/WMS_ch14_wRational.pdf. Imechukuliwa 20.07.2021

3. Holloway K. Rational use of drugs: an overview. Technical briefing seminar. Department of Essential Medicines and Pharmaceutical Policy TBS 2009. Geneva: World Health Organization.

4. Dele A. Background paper, Essential medicines for non-communicable diseases. Geneva: World Health Organization; 2011. [accessed on October 19, 2015]. Available from: http://www.who.int/medicines/areas/policy/access_noncommunicable/Essential MedicinesforNCDs.pdf.

5. Phadke A. Drug supply and use: towards a rational drug policy in India. New Delhi: Sage Publications; 1998. p. 184.

6. World Health Organization. Promoting rational use of medicines: core components-WHO policy perspectives on medicine no. 005 September 2002. Assessing the problem of irrational use. http://apps.who.int/medicinedocs/en/d/Jh3011e/3.html. Imechukuliwa 20.07.2021

7. Gagnon MA, Lexchin J. The cost of pushing pills: A new estimate of pharmaceutical promotion expenditure in the United States. PLoS Med. 2008;5:e1.

8. Institute for Safe Medication Practices, FDA. US drug shortages Frustration and safety concerns. Generics and Biosimilars Initiative. 2011. http://www.gabionline.net/Reports/US-drug-shortages-frustration-and-safety-concerns. Imechukuliwa 20.07.2021

9. Godman B, et al. Policies to enhance prescribing efficiency in Europe: findings and future implications. Front Pharmacol. 2011;1:141.

10. Generics and Biosimilars Initiative. Generics save US 1.2 trillion over last 10 years. http://www.gabionline.net/Reports/Generics-save-US-12-trillion-over-last-10-years. Imechukuliwa 20.07.2021

11. Generics and Biosimilars Initiative. Brand name drugs show huge price increases. Generics and Biosimilars Initiative http://www.gabionline.net/Reports/Brand-name-drugs-show-huge-price-increases. Imechukuliwa 20.07.2021

12. Nilima A. Kshirsagar. Rational use of medicines: Cost consideration & way forward. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC5345295/#:. Imechukuliwa 20.07.2021

bottom of page