top of page

Mwandishi:

Dkt. Mangwella S, MD

Mhariri:

Dkt. Benjamin L, MD

Alhamisi, 16 Septemba 2021

Maumivu ya fantomu

Maumivu ya fantomu

Fantomu ni hisia ya maumivu kutoka kwenye kiungo cha mkono au mguu kilichotengwa na mwili kwa upasuaji baada ya kuharibiwa na ugonjwa au ajali. Hutokea sana kwa wagonjwa waliokuwa na maumivu makali kabla ya upasuaji, tiba yake hutofautiana baina ya mtu na mtu na huhusisha matumizi ya dawa mbalimbali kabla ya kufahamu ipi inayofaa zaidi.


Historia ya maumivu ya Fantamu


Hapo zamani ilifahamika kuwa maumivu ya fantomu yanahusiana na matatizo ya kisaikolojia yanayotokea kwa wagonjwa baada ya kukatwa kiungo cha mwili kutokana na maumivu makali hata hivyo wanasayansi kwa sasa wanafahamu kuwa maumivu haya huanzia kwenye mfumo wa kati wa fahamu. Maumivu ya fantomu hufahamika kwa majina mengine ya;


 • 'Mguu wa fantamu'

 • 'Mkono wa fantomu'

 • 'Maumivu makali baada ya kukatwa mkono',

 • 'Maumivu makali baada ya kukatwa mguu'


Na kwa lugha ya kiingereza hufahamika kama;

'phantom pain'

'phantom limb;'


Vihatarishi


Si kila mtu atapata maumivu ya fantomu baada ya kuondolewa kiungo cha mwili, baadhi ya watu wenye vihatarishi vifuatavyo huwa na uwezekano mkubwa wa kupata maumivu haya;


Kuwa na maumivu kabla ya kufanyiwa upasuaji wa kuondolewa kiungo cha mwili. Hii inaweza kutokana na ubongo kutofuta kumbukumbu za kiungo cha mwili na hivyo kuendelea kutuma ishara za maumivu hata baada ya kiungo kuondolewa.


Maumivu ya sehemu ya kiungo kilichobaki baada ya upasuaji. Watu wenye maumivu ya kiungo kilichobaki baada ya upasuaji mara nyingi hupata maumivu ya fantomu. Maumivu ya kiungo kilichobaki huwza tokana na majeraha yaliyotokea kwenye mshipa wa fahamu wakati wa kukata kiungo au kukua vibaya kwa mshipa wa fahamu.


Dalili


Mbali na maumivu, sifa za maumivu ya fantomu ni;


 • Huanza ndani ya wiki la kuondolewa kiungo cha mwili hata hivyo yanaweza kutokea baada ya mwezi toka kufanyiwa upasuaji

 • Maumivu huja na kutoka

 • Maumivu huathiri sehemu ya mguu iliyo mbali na kiungo cha mwili mfano kanyagio ambalo limetolewa

 • Maumivu huelezewa kama ya kuchoma mithiri yam shale, kubana, kuchoma kama sindanol kuchanachana na kuungua


Matibabu


Ingawa hakuna dawa maalumu kwa kila mtu kwa ajili ya maumivu ya fantomu, dawa zinazotumika katika matibabu ya maumivu mbalimbali zinaweza kumsaidia mgonjwa. Hata hivyo dawa hizi huwa hazina ufanisi kwa kila mtu yaani kila mtu anaweza kunufaika na dawa ambayo haijamsaidia mwingine. Dawa zinazotumika kwenye matibabu ya maumivu ya fantomu ni pamoja na;


 • Dawa za maumivu mfano . Acetaminophen, ibuprofen, naproxen sodium

 • Dawa za jamii ya Antidepressants mfano amitriptyline, nortriptyline, tramadol

 • Dawa za kutibu degedege mfano; gabapentin, Neurontin, pregabalin

 • Dawa jamii ya Narcotiki mfano. codeine na morphine

 • Dawa jamii ya N-methyl-d-aspartate (NMDA) risepta agnonisti mfano dextromethorphan


Kinga ya maumivu ya fantomu


Kutokana na kuwa na hatari kubwa ya kupata maumivu ya fantomu kwa wagonjwa waliokuwana na maumivu kabla ya kukatwa kiungo cha mwili, Daktari atachukua hatua ya kukupa ganzi ya nusu kaputi masaa au siku chache kabla ya kufanyiwa upasuaji. Hii itapunguza maumivu haraka baada ya upasuaji na kuondoa hatari ya kupata maumivu ya muda mrefu ya fantomu.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

7 Oktoba 2021 04:36:51

Rejea za mada hii:

Alviar MJM, et al. Pharmacologic interventions for treating phantom limb pain. Cochrane Database of Systematic Reviews. http://www.thecochranelibrary.com. Imechukuliwa 16/09/2021

Ambron E, et al. Immersive low-cost virtual reality treatment for phantom limb pain: Evidence from two cases. Frontiers in Neuroscience. 2018;9:1.

Amputee Coalition. Managing phantom pain. https://www.amputee-coalition.org/limb-loss-resource-center/resources-for-pain-management/managing-phantom-pain/. Imechukuliwa 16/09/2021

Barbin J, et al. The effects of mirror therapy on pain and motor control of phantom limb in amputees: A systematic review. Annals of Physical and Rehabilitation Medicine. 2016;59:270.

Benzon HT, et al. Phantom limb pain. In: Practical Management of Pain. 5th ed. Philadelphia, Pa.: Mosby Elsevier; 2014. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 16/09/2021

Fuchs X, et al. Psychological factors associated with phantom limb pain: A review of recent findings. Pain and Research Management. https://www.hindawi.com/journals/prm/2018/5080123/. Imechukuliwa 16/09/2021

Kalapatapu V. Lower extremity amputation. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 16/09/2021

Merck Manual Professional Version. Pain in the residual limb. https://www.merckmanuals.com/professional/special-subjects/limb-prosthetics/pain-in-the-residual-limb#v21361465. Imechukuliwa 16/09/2021

National Institute of Mental Health. Brain stimulation therapies. https://www.nimh.nih.gov/health/topics/brain-stimulation-therapies/brain-stimulation-therapies.shtml. Imechukuliwa 16/09/2021

Ortiz-Catalan M, et al. Phantom motor execution facilitated by machine learning and augmented reality as treatment for phantom limb pain: A single group, clinical trial in patients with chronic intractable phantom limb pain. The Lancet. 2016;388:2885.

Pain: Hope through research. National Institute of Neurological Disorders and Stroke. https://www.ninds.nih.gov/Disorders/Patient-Caregiver-Education/Hope-Through-Research/Pain-Hope-Through-Research. Imechukuliwa 16/09/2021

Raffin E, et al. Primary motor cortex changes after amputation correlate with phantom limb pain and the ability to move the phantom limb. NeuroImage. 2016;130:134.

Rosenquist EWK. Overview of the treatment of chronic non-cancer pain. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 16/09/2021

Thieme H, et al. The efficacy of movement representation techniques for treatment of limb pain — A systematic review and meta-analysis. The Journal of Pain. 2016;17:167.

bottom of page