Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Helen L, M.D
Jumamosi, 23 Januari 2021
Mazingira ya kijani hupunguza msongo wa mawazo
Tafiti nyingi zinaonyesha, kutembelea na au kuishi mazingira yenye ukijani na vitu vya asili ya binadamu, hupunguza msongo wa mawazo na kuimarisha afya kwa ujumla. Tembelea na angalia mazingira ya kijani mara kwa mara kupunguza msongo wa mawazo na kuimarisha afya yako.
Namna gani unaweza kutumia mazingira ya kijani kupunguza msongo mwilini?
Endapo unataka kutumia mazingira ya asili ya binadamu kupunguza msongo wa mawazo fanya mambo yafuatayo;
Mimea mingi ya rangi ya kijani
Elekeza macho yako kwenye mazingira hayo, pumua kwa kina, huku ukifikiria namna hewa ianvyoingia na kutoka nje ya mapafu yako. Fanya hivi kwa jinsi utakavyoweza.
Endapo una mkeka, zuria au godoro dogo na eneo ulilopo ni salama, tandika mkeka wako chini, lala kwenye mkeka kisha angalia juu kwenye matawi ya miti, angalia miti na majani jinsi zinavyoitikia upepo unaopita, na sikiliza sauti nzuri ya miti na ndege wanaoimba kwa sauti nzuri, na ruhusu uhisi upepo asilia unaotokea kwenye miti huku ukivuta pumzi kwa kina na kuitoa taratibu.
Ukiwa umechoka kulala, tembea kwenye bustani au kwenye msitu na kisha ruhusu mikono yako iguse matawi na maua mazuri, fikiria namna gani mimea hiyo ilivyoumbwa kwa namna ya kipekee, namna gani inapata chakula, kwanini ina rangi ya kijani n.k
Namna ya kutengezeza mazingira yako kupunguza msongo wa mawaza
Tengeneza mazingira ya nyumbani kwako kwa;
Kupanda bustani ya maua
Kupanda miti mingi
Kupanda majani mafupi
Kubandika, kuning'iniza au kuchora picha zenye mazingira asilia ya yenye ukijani kwenye kuta za nyumba yako
Kufuga samaki asili wa baharini kwenye boksi la kioo, huku ukiweka mazingira yao asilia
Kutumia taa zenye mwanga asili au usio mkali
Endapo unatatizo sugu la msongo wa mawazo unatakiwa fanya nini?
Tafiti nyingi zimefanyika na kuonyesha kuwa, watu wenye tatizo sugu la msongo wa mawazo, endapo watatengeneza mazingira asili nyumbani au maeneo ya kazini, tatizo la msongo wa mawazo hupungua kwa kiasi kikubwa.
Baadhi ya hospitali pia katika nchi za bara la amerika na ulaya, zimeanza kuweka mazingira asili ili kuchangia ufanisi katika matibabu ya wagonjwa kwa kuwakutanisha kwenye mazingira asilia.
Maeneo gani unaweza tembelea ukapunguza msongo wa mawazo?
Yapo maeneo mengi ambayo unaweza tembelea, baadhi ya mazingira unayoweza tembelea ni pamoja na;
Bustani
Shambani
Msituni
Mbuga za wanyama
Maeneo ya hifadhi ya misitu
N.k
Kuwa na mazoea ya kutembelea au kuishi mazingira asilia mara kwa mara, tunza asili ili ikupe afya njema.
Njia zingine za kupunguza msongo wa mawazo zipo?
Ndio. Unaweza fahamu pia kuhusu njia zingine za kupunguza msongo wa mawazo, soma katika makala zingine zilizo ndani ya tovuti hii.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
19 Julai 2023 20:41:55
Rejea za mada hii:
1.Mihyang An, etal. Why We Need More Nature at Work: Effects of Natural Elements and Sunlight on Employee Mental Health and Work Attitudes. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC4877070/. Imechukuliwa 22.01.2021
2.New center to advance health and nature research and education. Https://vitalrecord.tamhsc.edu/new-center-to-advance-health-and-nature-research-and-education/. Imechukuliwa 22.01.2021
3.Green is good for you. https://www.apa.org/monitor/apr01/greengood. Imechukuliwa 22.01.2021
4.Levels of Nature and Stress Response. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC5981243/. Imechukuliwa 22.01.2021