top of page

Mwandishi:

Dkt. Lugonda S, MD

Mhariri:

Dkt. Peter R, MD

Alhamisi, 16 Desemba 2021

Maziwa ya mimea

Maziwa ya mimea

Ni majimaji meupe ambayo thamani ya virutubishi vyake ni sawa na maziwa ya ng’ombe, lakini huandaliwa kwa kutumia nafaka, mbegu na viazi.


Namna ya kutengeneza maziwa asili ya mmea


  • Loweka nafaka, mbegu au viazi (gramu 150 hadi 250 kupata lita 1 ya maziwa ) kwa usiku mmoja. Kiasi cha kutosha kinakadiriwa kuwa gramu 250.

  • Chuja maji yaliyotumika kuloweka nafaka

  • Vinginevyo, ongeza tende au zabibu kavu kama chanzo cha sukari ya afya (wastani wa kiganja kimoja kwa lita ya maji ya maziwa)

  • Weka maji ya kutosha ili kufunika nafaka, mbegu au viazi, kisha pondaponda hadi ute laini upatikane

  • Chuja kwa kutumia kitambaa au chujio la chuma

  • Kama unataka kuweka sukari, tumia stevia (sukari isiyo na kalori) au pengine molasi, sukari isiyosafishwa, panela au pilonsillo (chenga za sukari ya kahawia). Kama itapendeza, ongeza mchoto wa mdalasini au vanilla.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

16 Desemba 2021, 16:17:00

Rejea za mada hii:

1. Roselló-Soto, et al. “Enhancing Bioactive Antioxidants' Extraction from "Horchata de Chufa" By-Products.” Foods (Basel, Switzerland) vol. 7,10 161. 1 Oct. 2018, doi:10.3390/foods7100161.

2. Sethi, et al. “Plant-based milk alternatives an emerging segment of functional beverages: a review.” Journal of food science and technology vol. 53,9 (2016): 3408-3423. doi:10.1007/s13197-016-2328-3

bottom of page