Mwandishi:
DKt. Adolf S, M.D
Mhariri:
Dkt. Sospeter B, M.D
Jumamosi, 22 Julai 2023
Maziwa ya ng'ombe kwa mtoto chini ya miezi 12
Imekuwa ni jambo la kawaida kwa watoto kupewa maziwa ya ng’ombe kama mbadala wa maziwa ya mama. Ukweli ni kwamba maziwa ya ng’ombe yana virutubisho vingi zaidi ya maziwa ya binadamu, lakini virutubisho hivi vimelenga zaidi kwa ndama na wala si kwa binadamu. Hivyo pamoja na virutubisho vingi katika maziwa haya hayapendekezwi kitiba kama mbadala wa maziwa ya binadamu.
Watoto wenye umri chini ya miezi 12 hawapaswi kupewa maziwa ya ng’ombe kwani mfumo wa umeng’enyaji wa chakula katika umri huu huwa haujaanza kufanya kazi vema.
Madahara maziwa ya ng’ombe kwa watoto chini ya miezi 12
Zifuatazo ni changamoto zinazoweza kutokea endapo mtoto atapewa maziwa ya ng’ombe chini ya umri wa miezi 12;
Upungufu wa damu
Kupungukiwa maji mwilini endapo mtoto ana vihatarishi vingine mafano kuharisha na kutapika
Magonjwa ya kuhara
Kushindwa kustahimili laktosiÂ
Kuongezeka kwa hatari ya kupata changoÂ
Kukosa choo
Mzio
Kuongezeka kwa hatari ya kupata kisukari aina ya 1
Kuongezeka kwa hatari ya kupata magojwa ya mfumo wa umeng’enyaji wa chakula mfano inflamesheni ya matumbo nk.
Mambo ya kuzingatia
Endapo kuna ulazima sana wa kutonyonyesha ni vema kumpa mtoto maziwa ya fomula yaliyoongezwa vitaminiÂ
Madhara ya maziwa ya ng’ombe hupungua endapo mtoto ataanza kunywa baada ya miezi 12.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
22 Julai 2023 18:30:07
Rejea za mada hii:
1. Whole cow's milk in infancy - PMC – NCBI.https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC2791650/. Imechukuliwa 20.07.2023
2. Cow's milk-induced gastrointestinal disorders: From infancy to adulthood. NCBI. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC9685681/. Imechukuliwa 20.07.2023
3. Fortified Cow’s Milk and Milk Alternatives – Nutrition – CDC. https://www.cdc.gov/nutrition/infantandtoddlernutrition/foods-and-drinks/cows-milk-and-milk-alternatives.html. Imechukuliwa 20.07.2023