top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Salome A, MD

Jumapili, 18 Aprili 2021

Namna ya kufanya mtoto ale na kukua vema

Namna ya kufanya mtoto ale na kukua vema

Ili mtoto ale na kukua vema, muandalie chakula kutoka kwenye makundi mbalimbali, kula pamoja naye, usimlazimishe kula endapo ameshiba au hana njaa, mpe maji ya kunywa katika kiwango kinachoshauriwa kwa siku, usimpe vinywaji vya sukari, kama soda, mbadala wake mpatie maziwa mgando au juisi halisi, mpe milo midogo ya kiafya katikati ya milo mikuu mitatu ya siku, baadhi ya nyakati usihofu mtoto anapokataa kulana Kuwa mfano wa kuigwa kwa kula mlo kamili.


Nini cha kufanya ili mtoto ale zaidi?


Ili mtoto ale na kukua vema kumbuka kufanya mambo yafuatayo;


 • Muandalie chakula kutoka kwenye makundi mbalimbali

 • Kula pamoja na mtoto chakula cha familia

 • Usimlazimishe mtoto kula endapo ameshiba au hana njaa

 • Mpatie maji ya kunywa katika kiwango kinachoshauriwa kwa siku

 • Usimpatie vinywaji vya sukari, kama soda, mbadala wake mpatie maziwa mgando au juisi halisi

 • Mpe milo midogo ya kiafya katikati ya milo mikuu mitatu ya siku

 • Muhusishe mtoto kwenye uandaaji wa chakula

 • Baadhi ya nyakati usihofu mtoto anapokataa kula

 • Mpe nafasi mtoto acheze na wenzake, hii itaongeza njaa na hamu ya kula

 • Mpangie muda wa kuangalia TV au kucheza michezo kwenye vifaa tekinolojia

 • Kuwa mfano wa kuigwa kwa kula mlo kamili

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

19 Julai 2023 20:40:43

Rejea za mada hii:

bottom of page