Mwandishi:
Dkt. Mangwella S, MD
Mhariri:
Dkt. Peter A, MD
Jumapili, 28 Novemba 2021
Ngozi ya chungwa
Ngozi ya chungwa hutokeaje?
Kwa sababu ya ushawishi wa homoni za kike na ukusanyaji wa sumu na uchafu hususani maeneo ya makalio, mapaja na kuzunguka kiuno, ngozi huwa na kawaida ya kuhifadhi maji. Mbali na hayo, seli za mafuta chini ya ngozi huanza kuongezeka ukubwa na kujazwa na mafuta yanayohifadhiwa ndani yake. Matokeo yake ni kusababisha mchonyoto wa tishu unganishi unaopelekea mabadiliko katika uzuri wa ngozi hivyo kufanya iwe na mwonekano kama wa ganda la chungwa.
Matibabu
Mchonyoto wa tishu unganishi unapaswa kutibiwa kuanzia ndani yaani kutokea kwenye damu na mazingira ya damu badala ya kutumia krimu na dawa za kupaka.
Zipo sharubati za vyakula asili ambavyo hufanya kazi hii vema na huleta matokeo mazuri ndani ya muda mfupi kuanzia wiki mbili za matibabu. Sharubati hizi huondoa maji mwilini na kusafisha damu, baadhi yake zimetengenezwa kwa matango, figiri na nanasi. Soma zaidi namna ya kuondoa ngozi ya chungwa kwa kutumia sharubati hii kwenye makala ya sharubati ya ngozi ya chungwa.
Faida zingine za sharubati ya ngozi nyororo
Hupunguza maji mwilini
Husafisha damu
Hupunguza uzito
Huondo tatatizo la ngozi ya chungwa
Majina mengine ya makala hii?
Makala hii inaweza kutumika kutoa maelezo ya;
Ngozi ya chungwa matakoni
Ngozi ya chungwa mapajani
Ngozi ya chungwa tumboni
Ngozi ya chungwa kiunoni
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
28 Novemba 2021 12:55:19
Rejea za mada hii:
Lourenço CB, et al. Evaluation of the enzymatic activity and stability of commercial bromelain incorporated in topical formulations. Int J Cosmet Sci. 2016 Oct;38(5):535-40. doi: 10.1111/ics.12308. Epub 2016 Mar 16. PMID: 26833020.