top of page

Mwandishi:

Dkt. Lugonda B, MD

Mhariri:

Dkt. Mangwella S, MD

Jumamosi, 10 Juni 2023

Nguvu za kiume

Nguvu za kiume

Upungufu wa nguvu za kiume ni nini?


Upungufu wa Nguvu za kiume huweza kuelezewa kama kukosa uwezo wa kudumisha uume kusimama katika muda unaotosheleza mahitaji ya kujamiiana.

Upungufu wa nguvu za kiume unaweza kuwa ishara ya tatizo la kimwili au kisaikolojia. Msongo, matatizo katika mahusiano, na kutojiamini kunaweza kusababisha tatizo la kuishiwa nguvu za kiume. Ishara kuu ni kutokuwa na uwezo wa mwanaume kufikia au kudumisha kusimamisha uume kwa muda wa kutosheka kwa kwa ngono.


Visababishi

Kusisimka kingono kwa wanaume ni mchakato mgumu unaohusisha ubongo, homoni, hisia, neva, misuli na mishipa ya damu. Upungufu wa nguvu za kiume unaweza kutokea kutokana na tatizo lolote katika maeneo hayo. Vivyo hivyo, mafadhaiko na wasiwasi wa afya ya akili unaweza kusababisha au kuzidisha shida ya kusimamisha uume.


Wakati mwingine mchanganyiko wa masuala ya kimwili na kisaikolojia husababisha upungufu wa nguvu za kiume. Kwa mfano, hali ndogo ya kimwili ambayo inapunguza mwitikio wako wa ngono inaweza kusababisha wasiwasi kuhusu kudumisha uume kusimama. Wasiwasi unaosababishwa unaweza kusababisha au kuzidisha shida ya kusimamisha uume.


Sababu za Kimwili za Upungufu wa Nguvu za Kiume

Visababishi vya ugonjwa wa upungufu wa nguvu za kiume kutokana na magonjwa huwa pamoja na:

  • Ugonjwa wa moyo

  • Obeziti

  • Atherosclerosis

  • Kiwango cha juu cha lehemu

  • Shinikizo la damu la juu

  • Kisukari


  • Ugonjwa wa metaboli

  • Ugonjwa wa Parkinson

  • Sklerosisi iliyosambaa

  • Dawa aina fulani

  • Matumizi ya mazao ya tumbaku (sigara)

  • Ugonjwa wa Peyronie

  • Ulevi na aina zingine za matumizi mabaya ya dawa za kulevya

  • Matatizo ya usingizi

  • Matibabu ya saratani ya Prostate au Prostate iliyopanuliwa

  • Upasuaji au majeraha yanayoathiri eneo la sakafu ya nyonga au uti wa mgongo

  • Upungufu wa homoni testosterone


Sababu za Kisaikolojia za Ukosefu wa Nguvu za Kiume

Ubongo una jukumu muhimu katika kuchochea mfululizo wa matukio ya kimwili ambayo husababisha kusimama, kuanzia na hisia za msisimko wa ngono. Sababu kadhaa zinaweza kuingilia kati hisia za ngono na kusababisha au kuzorota kwa nguvu za kiume. Sababu hizo ni pamoja na

  • Unyogovu

  • Wasiwasi

  • Hali nyingine za afya ya akili

  • Msongo wa mawazo


Matatizo ya uhusiano kutokana na msongo wa mawazo, mawasiliano duni, au mambo mengine


Utambuzi

Uchunguzi wa afya na historia ya ngono


Hii inaweza kufichua hali zinazosababisha kukosa kwa nguvu za kiume. Inaweza pia kusaidia mtaalamu wako wa afya kutofautisha kati ya matatizo ya kusimama, kumwaga manii, kutofika kileleni au kukosa hamu ya ngono.


Uchunguzi wa kimwili

Kutafuta tatizo la msingi, kama vile:


Tatizo katika mfumo wa neva: Hii inaweza kuhusisha ikiwa uume wako hausimami kama inavyotarajiwa kwa anwani fulani.

Kubarehe: Viashieia kama vile madhaifu ya nywele maeneo ya siri n.k vinaweza kuonyesha matatizo ya homoni, ambayo yanahusisha mfumo wa endokrini.

Madhaifu ya uume: Haya yanaweza kupelekea kutosimama kwa uume kwa muda unaotakiwa.


Vipimo vya maabara

Hivi vinaweza kujumuisha wingi wa damu, vipimo vya mkojo, vipimo vya lehemu, na vipimo vya kreetinine na vimeng'enya vya ini. Wakati hamu ya ngono ipo, kupima kiwango cha testosterone katika damu kunaweza kugundua matatizo katika mfumo wa endokrini.


Ultrosound ya Ume

Kipimo hiki huweza kugundua matatizo katika mishipa ya damu ya uume


Matibabu ya Upungufu wa nguvu za kiume

Matibabu ya Upungufu wa nguvu za kiume hutokana na kisababishi. Huweza kuwa kutumia dawa, mazungumzo tiba na dawa.


ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

10 Juni 2023 18:41:01

Rejea za mada hii:

1. Erectile Dysfunction. https://www.nature.com/articles/nrdp20163. Imechukuliwa 10.06.2023
2. Erectile dysfunction. https://www.sciencedirect.com/science/article/abs/pii/S0140673612605200. Imechukuliwa 10.06.2023
3. Erectile Dysfunction. https://www.nejm.org/doi/full/10.1056/NEJM200006153422407. Imechukuliwa 10.06.2023

bottom of page