top of page

Mwandishi:

Dkt. Mangwella S, M.D

Mhariri:

Dkt. AdolfS, MD

Ijumaa, 14 Julai 2023

Nini kinafuata baada ya kuanza PEP?

Nini kinafuata baada ya kuanza PEP?

Mara baada ya kujianika kwenye maambukizi ya VVU na kuanza dawa ya kuzuia mambukizi ya VVU baada ya kujianika, kipimo cha kuangalia maambukizi ya VVU kwenye damu kitafanyika wiki ya 4 baada ya kuanza dawa, yaani wiki ya 6 na wiki ya 12.

 

Enadpo utaonyesha dalili zozote zinazoashiria maambukizi makali ya VVU, kipimo hiko kitafanyika wakati huo pasipo kusubiria muda kufika.

 

Kabla ya kuanza PEP na ifikapo wiki ya 2 ya kutumia PEP utafanyiwa vipimo vya kuchunguza afya ya mwili wako vinavyohusisha kuangalia utendaji kazi wa ini, figo na chembe za damu na ulinzi wa mwili.

 

Uchunguzi pia utafanyika ndani ya masaa 72 kupata taarifa za ziada kuhusu chanzo cha maambukizi, hali yako ya maambukizi ya VVU, kiwango cha virusi kwenye damu na kipimo cha usugu wa virusi kwenye dawa kama vinapatikana.


PEP inatumika kwa muda gani?

PEP itapaswa kutumika kwa muda wa wiki 4 mfululizo kama maudhi ya dawa yatavumilika, ikishindikana kundi la dawa litabadilishwa.

 

Nini kitafanyika nikionyesha dalili?

Utapewa rufaa kwenye CTC kama utaonyesha dalili zozote zinazoashiria VVU masaa 72 au zaidi tangu kuanza PEP kwa matibabu sahihi ya maambukizi ya VVU.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

14 Julai 2023 17:51:17

Rejea za mada hii:

1. MOH Tanzania, NATIONAL GUIDELINES FOR THE MANAGEMENT OF HIV AND AIDS 7th edition 2019

bottom of page