top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Jumanne, 20 Julai 2021

Njia za dawa kuingia mwilini

Njia za dawa kuingia mwilini

Ili kufanikiwa kwa tiba, unapaswa kutumia dawa kwa njia sahihi uliyoelekezwa na daktari au mtoa dawa. Kwa ufanisi wa dawa, tumia kama ulivyoelekezwa na daktari wako.


Njia ya mdomo

Njia ya kuweka mdomoni


Matumizi ya dawa kwa njia ya mdomo ni njia salama na inayofaa, dawa huingia mwilini kupitia kinywa na inaweza kutumiwa kwa njia kuu tatu ambazo ni 1. Kumeza 2. Kuweka chini ya ulimi au 3. Kusukutua kisha kutema


Faida ya matumizi ya dawa kwa njia ya mdomo

 • Ni rahisi kutumia

 • Inakubalika kwa watu wengi

 • Mara nyingi haihitaji uangalizi wa kitaalamu


Mapungufu ya matumizi ya dawa kwa njia ya mdomo

 • Uchokozi wa tumbo kwa baadhi ya dawa

 • Kufyonzwa kwa dawa kwenda mwilini kunategemea na hali ya tumboni (hakuna au kuna chakula)

 • Dawa inaweza kuharibika kikemikali kabla haijafyonzwa kutokana na vimeng’enyo vilivyomo tumboni

 • Siyo dawa zote zinaweza kupitia mdomoni

 • Ufyonzaji unaweza usiwe kamilifu


Njia ya matone


Njia hutumika kutibu magonjwa ya macho, pua na masikio au mdomoni.


Faida ya matumizi ya dawa kwa njia ya matone

 • Rahisi kutumia

 • Huwekwa na kutumika katika sehemu iliyoathirika


Mapungufu ya matumizi ya dawa kwa njia ya matone

 • Upungufu wa njia hii ni kuwa ni vigumu kwa watumiaji wengi kukadiria kipimo (dozi) sahihi na hivyo huweza kusababisha kifo.

 • Inaweza kusababisha muwasho


Njia ya sindano


Kuna aina nyingi za matumizi ya dawa kwa njia ya kuchoma sindano ambazo ni;


 • Kuchomwa chini ya ngozi

 • Kuchoma kwenye ngozi

 • Kuchoma ndani ya msuli/mnofu

 • Kuchoma ndani ya mshipa wa damu


Faida ya matumizi ya dawa kwa njia y sindano

 • Hufanya kazi haraka hasa katika kuokoa maisha

 • Inatumika kwa wanaotapika sana

 • Hutumika kwa wagonjwa waliopoteza fahamu


Mapungufu ya matumizi ya dawa kwa njia ya sindano

 • Inahitaji mtaalamu anayejua kuchoma sindano

 • Inaumiza/inauma

 • Kama haikuchomwa inavyotakiwa inaweza kusababisha madhara makubwa kama vile kupooza.

 • Inaogopesha kwa watoto na baadhi ya wakubwa

 • Kama sindano iliyotumika si salama yaweza kuambukiza magonjwa mfano virusi vya UKIMWI


Njia ya haja kubwa


Hufahamika kwa jina jingine la 'njia ya puru' huhusisha kuingizwa dawa ndani ya njia ya haja kubwa ili baadaye zifyonzwe na damu na kupelekwa sehemu nyingine ya mwili au kutibu magonjwa ya sehemu hiyo ilipowekwa. Dawa hizo hutengenezwa kwa umbo la sapozitori au katika hali ya maji maji


Faida ya kutumia dawa kwa njia ya haja kubwa

 • Inafaa kwa dawa ambazo zinaweza kuleta usumbufu tumboni, kwa mfano aspirini, Aminophylline, indomethacin

 • Inafaa kwa mgonjwa anayetapika

 • Inafaa kama unataka kutibu baadhi ya magonjwa ya sehemu ya haja kubwa

 • Inafaa kwa mgonjwa mwenye matatizo katika kumeza (swallowing) au hajitambui.

 • Watoto wanaokataa kunywa dawa


Mapungufu ya kutumia dawa kwa njia ya haja kubwa

 • Mgonjwa kuona aibu wakati wa kupewa maelekezo ya jinsi ya kutumia

 • Kama mgonjwa anatumia njia hii mara kwa mara, kuna uwezekano wa kusababisha maumivu na uvimbe katika sehemu hiyo.

 • Kufyonzwa kwa dawa kwenda sehemu nyingine za mwili kunaweza kuathiriwa na kinyesikilichoko kwenye sehemu hiyo.


Njia ya ukeni


Matumizi ya dawa kwa kuweka ukeni, hutumika kutibu magonjwa yaliyo katika mfumo wa uzazi wa kike mfano Clotrimazole na nystatin katika kutibu fangasi ukeni.


Faida ya matumizi ya dawa kwa kuweka ukeni

Ni rahisi kutumia

Huwekwa na kutumika katika sehemu iliyoathirika


Mapungufu ya matumizi ya dawa kwa kuweka ukeni

Mgonjwa kuona aibu wakati wa kupewa maelekezo ya jinsi ya kutumia

Kama mgonjwa anatumia njia hii mara kwa mara, kuna uwezekano wa kusababisha maumivu


Njia ya kuvuta pumzi


Njia hii hutumika kwa kuvuta dawa kwenye pumzi na hutumika zaidi kwa wagonjwa wenye matatizo ya pumu yakifua na matatizo ya dharura ya mfumo wa hewa kutokana na kuziba kwa njia za hewa yanayoweza kutibiwa kwa kutumia njia hii.


Dawa zinazotumiwa kwa njia hii, hufanya kazi ya kutanua njia zinazopitisha hewa kupeleka kwenye mapafu zenye jina la bronkodaileta kama vile dawa ya salbutamol.


Faida ya matumizi ya dawa kwa kuvuta pumzi

Dawa hufanya kazi kwa haraka


Mapungufu ya matumizi ya dawa kwa kuvuta pumzi

 • Ni vigumu kwa watumiaji wengi kukadiria kipimo (Dose) sahihi na hivyo huweza

 • kuzidisha au kupunguza kipimo.

 • Kiwango cha dawa kikizidi sana mgonjwa anaweza kupata madhara yanayoweza kusababisha kifo.


Njia ya kupakaa


Mara nyingi njia hii hutumika kutibu magonjwa ya ngozi. Aidha, inaweza kutumika kutibu magonjwa yaliyoko ndani ya mwili. Dawa hizo huweza kupenya ngozi hadi mfumo wa damu na kusambazwa sehemu mbali mbali za mwili.


Faida ya matumizi ya dawa kwa njia ya kupaka


Rahisi kutumika – mgonjwa anaweza kujipakaa mwenyewe.


 • Dawa hupakwa moja kwa moja kwenye sehemu yenye ugonjwa

 • Kupakwa kwa sehemu kubwa hurahisisha ufyonzaji wa dawa

 • Mapungufu ya matumizi ya dawa kwa njia ya kupaka

 • Baadhi ya dawa zinaweza kusababisha usumbufu au mzio wa ngozi

 • Baadhi ya dawa zinaweza kufyonzwa kwenda ndani ya mwili na kuleta madhara

 • Kutokuwa na uhakika wa kufyonzwa kikamilifu kwa dawa

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

7 Oktoba 2021 04:47:07

Rejea za mada hii:

1. Bancsi A, et al. Shoulder injury related to vaccine administration and other injection site events. Can Fam Physician. 2019 Jan;65(1):40-42.

2. Frid AH, et al. New Insulin Delivery Recommendations. Mayo Clin Proc. 2016 Sep;91(9):1231-55.

3. Gani F, et al. Oral health in asthmatic patients: a review : Asthma and its therapy may impact on oral health. Clin Mol Allergy. 2020 Nov 07;18(1):22.

4. Gonda I. Systemic delivery of drugs to humans via inhalation. J Aerosol Med. 2006 Spring;19(1):47-53.

5. Guarneri AM, et al. Nonglycemic Adverse Effects of Insulin. Curr Diabetes Rev. 2021 Jan 28;

6. Jang TY, et al. Recent Updates on the Systemic and Local Safety of Intranasal Steroids. Curr Drug Metab. 2016;17(10):992-996.

7. Kolikof J, et al. StatPearls [Internet]. StatPearls Publishing; Treasure Island (FL): May 24, 2020. Central Venous Catheter.

8. Levy M , et al. Home-based palliative care for children--Part 1: The institution of a program. J Palliat Care. 1990 Spring;6(1):11-5

9. Lowry M. Rectal drug administration in adults: how, when, why. 2016 Feb 24-Mar 1Nurs Times. 112(8):12-4.

10. Martyn JA, et al. The safe administration of medication: Nursing behaviours beyond the five-rights. Nurse Educ Pract. 2019 May;37:109-114.

11. Mathaes R, et al. Subcutaneous Injection Volume of Biopharmaceuticals-Pushing the Boundaries. J Pharm Sci. 2016 Aug;105(8):2255-9.

12. Mathias NR, et al. Non-invasive systemic drug delivery: developability considerations for alternate routes of administration. J Pharm Sci. 2010 Jan;99(1):1-20.

13. Nicoll LH, et al. Intramuscular injection: an integrative research review and guideline for evidence-based practice. Appl Nurs Res. 2002 Aug;15(3):149-62.

14. Park CW, et al. Iatrogenic Injury to the Sciatic Nerve due to Intramuscular Injection: A Case Report. Korean J Neurotrauma. 2019 Apr;15(1):61-66.

15. Perin DC, et al. Evidence-based measures to prevent central line-associated bloodstream infections: a systematic review. Rev Lat Am Enfermagem. 2016 Sep 01;24:e2787.

16. Salari M, et al. Comparison of skin traction, pressure, and rapid muscle release with conventional method on intramuscular injection pain: A randomized clinical trial. J Educ Health Promot. 2018;7:172.

17. Sisson H. Aspirating during the intramuscular injection procedure: a systematic literature review. J Clin Nurs. 2015 Sep;24(17-18):2368-75.

18. Srikrishna S, et al. The vagina as a route for drug delivery: a review. Int Urogynecol J. 2013 Apr;24(4):537-43.

19. van Hoogdalem E, et al. Pharmacokinetics of rectal drug administration, Part I. General considerations and clinical applications of centrally acting drugs. Clin Pharmacokinet. 1991 Jul;21(1):11-26.

20. Warren BL. Intramuscular injection angle: evidence for practice? Nurs Prax N Z. 2002 Jul;18(2):42-51.

bottom of page