top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Mangwella S, MD

Jumanne, 20 Februari 2024

Nyoa sehemu za siri bila kupata vipele na muwasho

Nyoa sehemu za siri bila kupata vipele na muwasho

Kunyoa nywele sehemu za siri ni jambo linalofanyika kwa sababu ya usafi wa mwili. Muwasho na vipele baada ya kunyoa sehemu za siri huleta hali ambayo humfanya mtu kujihisi vibaya na wakati mwingine kupata maambukizi katika mashina ya nywele. Hali hii huwapata sana wale wanaotumia kiwembe.

Jinsi ya kunyoa sehemu za siri

Zifuatazo ni hatua muhimu za kufuata wakati wa kunyoa nywele za sehemu za siri;

 • Anza kwa kupunguza nywele na mkasi, pia unaweza kuishia katika hatua hii ikiwa hauhitaji kuziondoa kabisa kuacha upara

 • Mwagia maji ya uvuguvugu eneo husika kisha paka sabuni au jeli, au krimu maalumu ya kunyolea

 • Nyoa kwa kufuata uelekeo wa nywele zinavyoota

 • Usirudie rudie kupitisha kinyoleo eneo moja

 • Nyoa taratibu bila kuweka mgandamizo mkubwa

 • Safisha vizuri na maji ya uvuguvugu kuondoa mabaki ya nywele ulizonyoa

 • Paka mafuta ya maji kulainisha ngozi ya eneo hilo


Mambo ya kuzingatia

 • Usitumie kiwembe kitupu kunyoa sehemu za siri kwani huleta marejaha madogo sana yanayoweza leta muwasho na kukuweka katika hatari ya kupata magonjwa ya ngono

 • Usinyoe mara kwa mara kuzuia mkereketo katika ngozi ya sehemu za siri

 • Safisha vifaa vyako kila unapomaliza kunyoa

 • Badili kinyoleo baada ya kutumia walau mara 5

 • Usitumie kinyoleo chenye kiwembe butu

 • Usinyoe kila siku

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

20 Februari 2024 15:27:33

Rejea za mada hii:

1.       How to treat and prevent razor bumps in the pubic area. Medical Newa Today. https://www.medicalnewstoday.com/articles/how-can-people-treat-razor-bumps-in-the-genital-area#vs-st-is. Imechukuliwa 20.01.2024

2.       How to Get Rid of or Prevent Razor Burn and Ingrown Hairs. Healthline. https://www.healthline.com/health/how-to-get-rid-of-razor-burn#takeaway. Imechukuliwa 20.01.2024

3.       Razor Burn Treatment: Effective Remedies and Solutions. WebMd. https://www.webmd.com/skin-problems-and-treatments/remedies-relieve-razor-burn. Imechukuliwa 20.01.2024bottom of page