Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Helen L, M.D
Jumamosi, 6 Februari 2021
Osha na chemsha mayai kujikinga na Taifod
Viumbe jamii ya ndege wenye maambukizi ya kimelea cha ‘salmonella’ kinachosababisha taifodi, huzalisha mayai yenye vimelea hao. Hata hivyo pia yai huweza kubeba vimelea kwa nje endapo litagusa kinyesi chenye vimelea. Osha na chemsha mayai yako kuepuka maambukizi hayo
Viumbe jamii ya ndege kama kuku, bata n.k wenye maambukizi ya taifod, huweza kuzalisha mayai yenye vimelea hao. Vimelea vya maradhi huingia kwenye mayai wakati wa kutengenezwa, kabla ya yai kupata ganda lake gumu. Hata hivyo pia mayai endapo yatakutana na kinyesi cha ndege chenye maambukizi, vimelea hao hubakia kwenye magamba ya yai. Endapo utatumia mayai haya bila kuzingatia kanuni za kiafya, utapata maambukizi hayo.
Namna ya kuandaa mayai ili kuepuka maabukizi ya taifod
Chemsha yai lako mpaka liwe gumu kwa ndani au pasua na kukaanga liive mpaka kupata rangi ya kahawia
Kama unataka kutengeneza chakula cha mayai mabichi, tumia mayai yaliyotakaswa kwa kuondolewa vimelea vya maradhi
Kula au weka kwenye jokofu chakula chako mara moja baada ya kupika.
Nawa mikono na safisha vyomba ambavyo vimegusa mayai mabichi ikiwa pamoja na sufuria, sahani n.k
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
19 Julai 2023 20:41:55
Rejea za mada hii:
1.Salmonella and Eggs. https://www.cdc.gov/foodsafety/communication/salmonella-and-eggs.html. Imechukuliwa 07.02.2021
2.FDA. What You Need to Know About Egg Safety. https://www.fda.gov/food/buy-store-serve-safe-food/what-you-need-know-about-egg-safety. Imechukuliwa 07.02.2021
3.Egg Products and Food Safety. https://www.fsis.usda.gov/wps/portal/fsis/topics/food-safety-education/get-answers/food-safety-fact-sheets/egg-products-preparation/egg-products-and-food-safety/CT_Index. Imechukuliwa 07.02.2021