Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Salome A, MD
Alhamisi, 4 Machi 2021
Oxytocin na Prolactin huongezeka kwenye damu baada ya kujifungua
Baada ya kujifungua, kiwango cha homoni estrogen na progesterone hupungua, wakati huo homoni prolactin na oxytocin huongezeka zaidi ili kuongeza uzalishaji wa maziwa na kufanya kizazi kirejee kwenye umbo lake asilia.
Mabadiliko ya homoni baada ya kujingua
Homoni Prolactin, huchochea matiti kuzalisha maziwa. Homoni hii huwa kwa wingi sana kipindi cha mwanzo sana baada ya kujifungua ili kufanya usisimuaji wa matiti kuzalisha maziwa ya awali. Kiwango chake huanza kupungua tena mara mbili hadi tatu ya kawaida wiki ya pili hadi ya nne baada ya kujifungua, kisha kufuatiwa na kuongezeka kwa homoni hiyo kuitikia hisia za kuguswa kwa ziwa wakati wa kunyonyesha.
Homoni prolactin huasha hisia za kisaikolojia za mama, mama anayenyonyesha huwa na mzigo mkubwa wa kumjali na kumnyonyesha mtoto kutokana na madhara ya homoni hii. Mzigo huu unaweza kuwa kama ule wa kutaka kunyonyesha mtoto mara kwa mara na kutaka kumbeba au kuwa karibu na mtoto wake wakati wote
Homoni Oxytocin, huwa na kazi mbili kuu zinazohusiaana na unyonyeshaji, kwanza hufanya kazi ya kusinyaza kizazi cha mama ili kirejee kwenye umbo lake la awali wakati wa kunyonyesha na pili huchochea matiti yatoe maziwa kutoka kwenye tezi za kuzalisha maziwa.
Homoni Oxytocin hufanya kazi za kifiziolojia zilizo kinyume na zile zinazofanywa na prolactin. Hufanya mama aondokane na msongo,atosheke na kuridhika mapenzi aliyonaye na mwanawe anapokuwa ananyonyesha mtoto. Hii ni kawaida kwa binadamu. Matokeo ya ufanyaji kazi wa homoni hizi mbili ni kuongeza mahusiano makubwa ya mama na mtoto wake na kusahau kuhusu watu wengine ikiwa pamoja na mpenzi wake.
Mama na mpenzi wa mama anayenyonyesha wote wanatakiwa kufahamu ni nini kinachotokea mwilini mwa mama anayenyonyesha ili ili waweze kusaidiana kwenye masuaa ya mahusiano yao ya kimapenzi wakati huo mtoto pia apate chakula chake na kukua vema. Isipofanyika hivyo, mpenzi anaweza ona kuwa ametengwa na kumpa nafasi ya kutafuta mapenzi kutoka kwa mtu mwingine mar atakapohisi kuwa mama hana mapenzi naye tena.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
19 Julai 2023 20:40:48
Rejea za mada hii:
1. Alder E, et al. The relationship between breastfeeding persistence, sexuality and mood in postpartum women. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/3399590/. Imechukuliwa 4.03.2021
2. Viola Polomeno, et al. Sex and Breastfeeding: An Educational Perspective. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3431754/. Imechukuliwa 4.03.2021
3. Dettwyler K,et al. Sexuality and breastfeeding. Journal of Human Lactation. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/8634100/. Imechukuliwa 4.03.2021
4. Gamble D, et al. Postponing and types of involvement. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/8410435/. Imechukuliwa 4.03.2021
5. Hotchner T. Pregnancy and childbirth. 1990. Imechukuliwa 4.03.2021
6. Huggins, et al. The Nursing Mother's Guide to Weaning-Revised: How to Bring Breastfeeding to a Gentle Close, and How to Decide When the Time Is Right. Harvard Common Press, 2007. Imechukuliwa 4.03.2021
7. Lawrence R. Breastfeeding: A guide for the medical profession. CV Mosby Company; St. Louis, MO. 1989. Imechukuliwa 4.03.2021
8. Polomeno V. Sex and breastfeeding: An educational perspective. The Journal of perinatal education. 1999;8(1):30. Imechukuliwa 4.03.2021
9. Lethbridge DJ. The use of breastfeeding as a contraceptive. Journal of Obstetric, Gynecologic, & Neonatal Nursing. 1989 Jan;18(1):31-7. Imechukuliwa 4.03.2021